Wednesday, September 17, 2014

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI-- UANDISHI NA UTUNZI WA VITABU NA MASHAIRI

UANDISHI  na  UTUNZI   wa       VITABU , MASHAIRI , RIWAYA , VITABU   VYA   KITAALUMA ( MASOMO )     ni    njia    na    sanaa     ya   kukupatia   PESA.   Waandishi   maarufu   kama   akina   CHINUO    ACHEBE ,  SOCRATES ,  SHAABAN    ROBERT   , NAPOLEON   HILL ,  CARL   MAX ,  HERODOTUS   na    PINDAR   wanakumbukwa   na   kuenziwa   hadi  dakika  hii   kwa    kazi  zao. Hata  sasa  wapo   waandishi   wengi  tu ,  ukipenda  hata  wewe   unaweza   kuwa  mmoja  wao.

Unaweza   kutunga   kitabu  kuhusu suala   lolote   ambalo  linaweza   kuelimisha   jamii  au    kuburudisha   jamii.  Kwa   mfano  unaweza   kutunga  kitabu   cha   hadithi  na   unaweza    kueleza kuhusu   jambo   lolote   lile.


KUANDIKA   KITABU   inagharimu   sana    MUDA   na   KICHWA ---   AKILI.  UNAWAZA   NA    KUWAZUA.  UANDIKE  NINI  /  KIPI  UACHE   KIPI  !  NI   SANAA    NGUMU   LAKINI    MWISHO   WA   SIKU   INALIPA.   TAFUTA    mada --- kitu   unachoona   kitaifaa   jamii    yako   ya  sasa    na    vizazi   vijavyo   kisha    kiweke    katika    MAANDISHI.

No comments:

Post a Comment