Sunday, August 31, 2014

PIGA HATUA MOJA KWA WAKATI

Katika  SAFARI  YA   MAISHA , hakuna  zulia   la    kimuujiza.Tunapaswa    kutembea   wenyewe  kwa  miguu  yetu   miwili, hatua   moja  kwa   wakati . Inaweza   kuonekana  kuwa  ni  vigumu  kuweza  kufika  UMBALI   MREFU  kwa    kutumia   njia  hii  ya    kwenda  polepole  na  ya   makusudi. Unaweza  ukaanza  kuamini    kuwa   hutaweza  kupata  MAFANIKIO  yoyote   makubwa    kwa   mwendo  wa  aina   hiyo , lakini    inakupasa    kuwa     na  SUBIRA.

VIJANA  wengi wana  NDOTO   za   kukamilisha  mambo  makubwa   katika   MAISHA   yao.Inatubidi tuwahimize   kujifunza  pia  kwamba   MAMBO  MAKUBWA  yanaweza  kukamilishwa   tu   kwa   kufanya   KAZI   KWA  BIDII   kila   siku.

HATUA   zako   ndogondogo  zikijumlishwa   pamoja  zina   matokeo    ya    kudumu. JITIHADA   za  kila  siku  huleta   USHINDI   mdogomdogo  unaokusukuma   WEWE  KUFANYA   JITIHADA  KUBWA  zaidi.  JITIHADA  hizo  kubwa   zaidi   huleta  USHINDI  MKUBWA  zaidi  ,  na  MATOKEO   YA   KUDUMU  huweza   kukupandisha    chati   hadi    kwenye  viwango    vya   ajabu   ENDAPO  UTAZIDI  KUSONGA    MBELE.
   Katika  maisha  yetu   binafsi  au  katika  kusimamia   biashara  yoyote , hatua   moja   kwa   wakati  ndio  njia    pekee   ya  uhakika   ya  kubadili   NDOTO   kuwa   jambo  la   ukweli.
   KWA  KUHITIMISHA  nasema   bila   JITIHADA ,  DIRA  NZURI SANA  itabakia   kuwa    NDOTO  isiyokamilishwa. Hakuna   LENGO  lolote  bora  lililowahi  KUFANIKISHWA  bila   KUFANYA   KAZI  KWA JUHUDI  KUBWA  na   kwa   njia    inayokubalika.

No comments:

Post a Comment