Neno KUJITAMBUA linatokana na neno TAMBUA lenye maana ya KUJUA UKWELI WA KITU FULANI KWA KINA , kwahiyo KUJITAMBUA ni hali ya KUJIJUA VILIVYO KWA KINA . Ingawa watu wengi sana WANAISHI lakini HAWAJITAMBUI KWA KINA.
HUWEZI kuwa MJASIRIAMALI mwenye MAFANIKIO bila ya KUJITAMBUA. Wakati huo huo HUWEZI KUJITAMBUA BILA KUMJUA MUNGU.
JIULIZE MASWALI HAYA :--
{1}. Kwanini Ulizaliwa ?
{2}.Umekuja hapa duniani kufanya nini ?
{3}.Umetokea wapi na unaenda wapi ?
AMINI USIAMINI MATAJIRI ( Watu wenye MAFANIKIO ) duniani kote wanajua kwanini walizaliwa ? Kwa nini Wanaishi lakini pia wanajua wanakokwenda.
Kwahiyo ili UFANIKIWE ni lazima UJUE UMETOKA WAPI ? NA UNAKWENDA WAPI ? NA KWANINI UPO HAPA DUNIANI ?
Katika MAISHA YA MAFANIKIO ni lazima SIO OMBI kuwa ili Uweze KUFANIKIWA katika kiwango kikubwa ni lazima uwe umeyapata majibu ya maswali ya hapo juu.