Thursday, September 4, 2014

HESHIMU HISIA ZAKO.

HISIA   NI  NINI ?  Kuna   tofauti  gani  kati  ya   HISIA   na   MATAMANIO ?
  BINADAMU  ana   NAFSI   MBILI.   Nafsi    ya   kumuelekeza    MAZURI   na   Nafsi   ya  kumuelekeza    MABAYA.
      KWA  MFANO ,  unaweza   kuwa   unataka  kutenda  JAMBO   BAYA. Bila   shaka kuna   sauti    nafsini    kwako   inakunong"oneza ,  USIFANYE  JAMBO  HILI , nyingine   inakwambia  FANYA ! Inayokwambia  "USIFANYE  NI   HISIA " inayokwambia  " FANYA" ni  MATAMANIO.
     Bila  shaka   umewahi  kusikia    MTU   akimwambia    mwenzake ,  "  UNA   MACHALE  SANA , VINGINEVYO  UNGEIBIWA ! " Je, unafikiri   hii   inamaanisha  NINI ? Hii   ni    " HISIA "  ndiyo  iliyomwongoza  na   kumwepusha   na   balaa  la   kuibiwa .
    AU  unaweza  kuwa   umezungukwa   na   watu , unasikia   SAUTI  INAKUNONG"ONEZA , " KIMBIA  HARAKA !  Hawa   watu    ni   HATARI   kwako. " Lakini   sauti   hiyo  haiwezi   kusikika  kwa   mtu   mwingine   yeyote  zaidi   yako. JE ,  UNAFIKIRI  HUYU  ANAYEKUNONG"ONEZA NI  NANI ?  NI  " HISIA "  NDIYO   INAYOONGEA   NA   WEWE ! Watu   wengi   hudharau   "HISIA"  zao  na   mwishowe  hupata    MATATIZO.
      KILA   MTU   ANA  HISIA.  Watu  hutumia  lugha:  " CHALE  ZILIMCHEZA ",  wakimaanisha :  "  HISIA   ZILIMWAMBIA."
      HISIA   ni  NGUVU   iliyo    ndani  ya    mwili   wako  ambayo   HUKUONGOZA. Zimewekwa  katika   mwili  wako  kwa   malengo   maalumu   KUKUSAIDIA. PINDI   unapotawaliwa  na   MATAMANIO ,  ni hakika  kwamba  baadaye   UTAWEZA    KUKOSA   FURAHA.  HISIA   hujaribu  KUKUTAARIFU kuwa  JAMBO   FULANI   SI   ZURI .  HUKUSISITIZA  ZAIDI   NA  ZAIDI.
   UKIONA  HISIA  zinakuzuia    KUFANYA  JAMBO , LIACHE    MARA   MOJA.  KISHA ,  TOKA   UTAFAKARI   AU  UWAULIZE   WENGINE.  Kwa   kufnya   hivyo ,  itakusaidia  KUPAMBANUA   MWELEKEO  WA  HISIA  ZAKO.WANAOHESHIMU  HISIA  ZAO  HAWAJUTI.
   ANZA  KUHESHIMU  HISIA ZAKO ,  si  kwamba  UTAPATA   PESA  TU , BALI kuna   mambo   mengi   ambayo  UTAWEZA  KUFANIKIWA  MAISHANI  KUTOKANA   NA  KUHESHIMU  HISIA  ZAKO.
   HISIA  zinavutia. WAPELELEZI  hutumia   HISIA. HISIA  Zinapowambia  JAMBO   HUSIMAMA. HUZISIKILIZA.  kisha   huzifanyia  kazi.Vivyo  hivyo ,  hata   WANASAYANSI , WATABIRI ,MADAKTARI  N.K.
    KILA  SIKU   HISIA   ZINAZUNGUMZA  NA   SISI . KINACHOTAKIWA  NI KUZIHESHIMU.
HISIA   NI  KIONGOZI   NA  MSHAURI  WETU  TUMHESHIMU   ILI   TUEPUKANE   NA  MATATIZO  MBALIMBALI.

No comments:

Post a Comment