EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.



Ni masaa mangapi unatumia kila siku kuzurura kwenye mitandao ya kijamii?

Unapaswa ufahamu hili miaka 20 iliyopita, kabla ya mitandao ya kijamii na simu janja hazijaingia kwenye maisha ya watu, mtandao ulipewa nafasi ya kufanya makubwa  na hakuna aliyeweza kufikiri ingekuja na madhara makubwa kwa watumiaji wake.

Lakini miaka 10 baadaye, mambo yakawa yamebadilika kabisa.

Simu janja zikawa sehemu ya maisha ya kawaida ya watu na mitandao ya kijamii ikawa njia kuu ya mawasiliano na kupashana habari.

Hatari kubwa ambayo imeibuka ni usumbufu mkubwa ambao umeletwa kwenye maisha yako na simu hizi janja pamoja na mitandao ya kijamii.

Imekuwa vigumu sana kupata utulivu na umakini wa kuweka kwenye yale mambo muhimu ya maisha yako.

Kila mara unapata msukumo wa kuingia kwenye mitandao hii, kushirikisha kuhusu maisha yako au kuangalia nini kinaendelea kwenye maisha ya wengine.

Imefikia hatua ambayo unajishangaa mwenyewe, una akili kubwa sana ya utambuzi na kufanya maamuzi lakini unashindwa kujizuia kutumia simu janja na mitandao ya kijamii bila kikomo.

Tatizo hili limezidi kukua na sasa madhara yake yanakwenda zaidi kwa vijana wanaokulia katika kizazi hiki, wengi wanakosa muda wa kutengeneza mahusiano imara ya kijamii, ya kuwa na watu ana kwa ana kwa sababu muda wao mwingi wanautumia kwenye mitandao ya kijamii.

Kazi pia zimeathirika sana na mitandao hii, wewe ni mmoja kati ya wengi mnaokiri ufanisi na uzalishaji wako kushuka kutokana na matumizi makubwa ya mitandao hii ya kijamii.

Imegundulika njia bora ya kutatua changamoto hii, ni kutumia falsafa bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii, ambayo ina manufaa kutokana na madhara ya mitandao hii.

 Falsafa hii haibadili kitu kimoja kwenye matumizi yako ya simu janja na mitandao ya kijamii, bali inabadili mfumo wako mzima wa maisha na jinsi unavyoichukulia na kuitumia mitandao hii.

Rafiki unaifahamu falsafa bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii iliyonisaidia mimi na maelfu ya watu?

Rafiki kama hauifahamu  na hujaanza kuitumia nakushauri usome ya kitabu kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.

 

 

No comments:

Post a Comment