Tuesday, November 3, 2015

FALSAFA ( PHILOSOPHY ) NI NINI ?



 Neno fasalfa si neno geni masikioni mwentu, kwani tumekuwa tukilisikia au kilitumia mara kwa mara katika mazungumzo yetu ya kila siku. Katika mada hii nitaelezea elimu ya Falsafa muhtasari.
Neno FALSAFA, linatokana na neno la kigiriki PHILOSOPHIA. Ambapo ni muunganiko wa maneno mawawili: PHILO na SOPHIA.
Neno PHILO linamaanisha UPENDO na neno SOPHIA lina maansiha HEKIMA.
Hivyo basi neno PHILOSOPHIA au FALSAFA linamaanisha upendo wa hekima.
Kwa kuzingatia maana ya neno Falsafa, tunakuta kuwa neno hili lina maana tofauti kabisa na ile ambayo sisi huitumia katika mazungumzo yetu ya kila siku.
Katika mazungumzo yetu ya kila siku neno Falsafa hutumika kuelezea itikadi, imani au mwenendo wa mtu au kundi fulani.
Mfano: Falsafa ya maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w) au falsafa ya chama fulani.
Katika makala hii ninazungumzia Falsafa kwa maana ya Upendo wa hekima, nasio ile maana iliyozoeleka katika mazungumzo yetu ya kila siku.
  • Historia ya neno Falsafa:
wataalamu katika kuelezea histori ya neno falsafa wamegawanyika katika makundi matatu:
1. Kundi la kwanza linasema kuwa: mtu wa kwanza kutumia neno falsafa alikuwa ni Fithagoras (Pythagoras) ambaye aliishi karne ya sita kabla ya kuzaliwa kristo. Fithagoras anaitikadia kuwa Hekima ni katika sifa mahsusi za Mwenyezi Mungu na  hii ndio sababu ya yeye kujiita Philosopher (Mpenda hekima).

2. Kundi la pili linasema kuwa: mtu wa kwanza kutumia neno hili alikuwa ni Haruduut ambapo alilitumia neno hili katika Tarekhe yake mnamo karne ya tano kabla ya kristo.

3. Kundi la tatu linasema kuwa: mtu wa kwanza kutumia neno hili alikuwa ni (Sokrets) Socrates ambapo alilitumia neno hili  dhidi ya kikundi cha Sophist ambao walikuwa wakitumia hoja potofu na dalili za udanganyifu na ulaghai katika maisha yao ya kila siku na kujikuta wakiifanya haki kuwa batili na mengineyo mengi.



 

No comments:

Post a Comment