Friday, November 30, 2018

SAFARI YA MAFANIKIO INAANZA NA WATU WENGI SANA. WENGI HUISHIA NJIANI, KWANINI ??


Watu wengi wanakata tamaa kwenye safari ya mafanikio kwa sababu ya kutokujua kwamba mafanikioo yanataka muda mrefu. Katika kipindi cha kutafuta mafanikio yako unatakiwa ujitoe hasa, kuvumilia na kutoa kila ulichonacho hadi ufanikiwe.
Kwa mfano, ilichukua muda wa miaka 11 hadi program ya ‘Microsoft’ ya bilionea mkubwa duniani kuanza kufanya kazi na kuleta mafanikio makubwa. Mafanikio yake hayakutokea tu ghafla kuna miaka ilikataika hapa katikati.
Pia ilimchukua miaka 29 kwa Abraham Lincoln hadi kuweza kuwa Rais wa marekani. Ipo mifano mingi inayoonyesha kwamba mafanikio si kitu cha mara moja tu, unatakiwa kuwekeza muda ili uweze kufanikiwa kwenye mafanikio hayo uyatakayo.
Kwenye akili yako sasa weka wazi, mafanikio ni safari ya muda mrefu. Unatakiwa kabisa utenge miaka angalau kuanzia 5 hadi 15 ya kutafafuta mafanikio yako ya kweli na ya kudumu. Ukikurupuka na kutaka mafanikio ya chapu chapu utakwama.
Kama utakuwa ni mtu wa kutaka mafanikio na halafu ukategemea mafanikio hayo yakatokea ghafla ghafla kwa muda mchache ni rahisi sana kwako kuweza kukata tamaa na kuona ni kitu ambacho hakiwezekani au mafanikio ni ya watu wa aina fulani tu lakini si wewe.

2 comments:

  1. Kwenye akili yako sasa weka wazi, mafanikio ni safari ya muda mrefu. Unatakiwa kabisa utenge miaka angalau kuanzia 5 hadi 15 ya kutafafuta mafanikio yako ya kweli na ya kudumu. Ukikurupuka na kutaka mafanikio ya chapu chapu utakwama.

    ReplyDelete
  2. Watu wengi wanakata tamaa kwenye safari ya mafanikio kwa sababu ya kutokujua kwamba mafanikioo yanataka muda mrefu. Katika kipindi cha kutafuta mafanikio yako unatakiwa ujitoe hasa, kuvumilia na kutoa kila ulichonacho hadi ufanikiwe.

    ReplyDelete