RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Ally Yahaya Simba. Bodi ya TCRA imekuwa ikiongozwa na Prof. Haji Semboja.
Taarifa hiyo ilieleza kwamba hatua hiyo ilisababisha Tanzania kupoteza mapato ya takriban sh. bilioni 400 kwa mwaka.
Mamlaka ya Mawasiliano iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu Machi 22, 2013.
Kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano, lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), kwa mujibu wa serikali.
No comments:
Post a Comment