MKONGWE wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Judithi Wambura ‘Lady Jay Dee’, amesema maana halisi ya wimbo wake wa ‘Ndi ndi ndi’ ni kwamba ‘mimi ni kitu na wewe si chochote’.
Wimbo huo mpya umewapa wakati mgumu mashabiki wake, hivyo ameona ni bora aweke wazi maana halisi ya wimbo huo.
“Wimbo umekuwa ukiwapa wakati mgumu mashabiki wangu, lakini nimeona bora nifumbue fumbo hili, Ndi ndi ndi maana yake ni mimi ni kitu na wewe si chochote,” alisema Jay Dee.
Wimbo huo kwa sasa unafanya vizuri tangu alipouachia hivi karibuni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. Msanii huyo amewashukuru mashabiki wake kwa mapokezi ya wimbo huo.
CHANZO CHA HABARI : GAZETI LA MTANZANIA NA BEATRICE KAIZA , Jumatatu , Aprili 25 , 2016.
No comments:
Post a Comment