Moja ya kisingizio cha watu wengi kwenye kushindwa kufanya yale
wanayotaka kufanya kimekua ni muda. Muda unaonekana kuwa mfupi sana na
mambo ya kufanya yakiwa mengi. Hivyo tumekuwa tunatamani kama masaa ya
siku yangeongezwa ili tuweze kufanya zaidi.
Lakini ukweli ni kwamba, masaa ya siku hayataongezeka, ni yale yale
24. Na wale wanaofanikiwa sawa sawa na wanaoshindwa, wana masaa hayo
hayo kwa siku. Sasa kwa nini wachache wafanikiwe kwenye muda huo, wakati
wengi wanashindwa na kuona hawana muda?
Seneca analo jibu zuri sana kwetu kuhusu muda;
Life is long enough, and a sufficiently generous amount has been
given to us for the highest achievements if it were all well invested.
But when it is wasted in heedless luxury and spent on no good activity,
we are forced at last by death’s final constraint to realize that it has
passed away before we knew it was passing. So it is: we are not given a
short life but we make it short, and we are not ill-supplied but
wasteful of it. Just as when ample and princely wealth falls to a bad
owner it is squandered in a moment, but wealth however modest, if
entrusted to a good custodian, increases with use, so our lifetime
extends amply if you manage it properly. – Seneca, On The Shortness Of
Life.
Maisha ni marefu vya kutosha na muda wa kutosha tumepewa kwa kufikia
yale makubwa kama tutauwekeza muda huo vizuri. Lakini tunapopoteza muda
huo kwa anasa zisizo na maana na kushindwa kufanya yale mazuri, tunakuja
kustuka tumepoteza muda na maisha yetu pale tunapofikia kifo. Hivyo
basi, siyo kwamba tuna maisha mafupi, bali tunayafanya kuwa mafupi, siyo
kwamba muda ni mdogo, bali tunao mwingi mpaka tunaupoteza. Kama ambavyo
utajiri ukiwa kwenye mikono ya mtu asiye makini unapotea na ukiwa
kwenye mikono ya mtu makini unakua, ndivyo maisha yetu yalivyo, yanakua
kama yataendeshwa vizuri.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment