Huwa tunayaona maisha yetu ni magumu na tuna mengi ya kukabiliana
nayo, lakini hebu fikiria jinsi ulimwengu unavyojiendesha. Fikiria jinsi
ambavyo sayari yetu ya dunia inalizunguka jua mwaka mzima, na kutupatia
majira ya mwaka. Fikiria jinsi sayari hii inajizungusha kwenye mhimili
wake kila siku na kutupatia usiku na mchana. Asili imeyapangilia mambo
yake ambayo yanajiendesha vizuri.
Sisi pia tunapaswa kuishi kwa msingi wa asili, kujua kile ambacho
tunapaswa kufanya, kujipanga kukifanya na kukifanya kwa ubora na msimamo
kama ambavyo asili inafanya mambo yake. Kwa kuishi kulingana na asili,
hata matatizo yetu yanayotusumbua yanaonekana ni madogo sana
ukilinganisha na jinsi ulimwengu mzima unavyojiendesha.
Kazi za Mungu ndiyo zinatupa sisi riziki, na kazi za asili
hazitofautiani na asili yenyewe. Kila kitu kinatokana na asili. Kila
kitu ambacho ni muhimu na kinachohitajika na ulimwengu mzima kinatokana
na asili. Kila kinachotokana na asili na kila kinachoitunza asili ni
kizuri kwa kila sehemu ya asili. Mabadiliko ya kipengele chochote kwenye
asili, ndiyo yanaufanya ulimwengu kuwa kama ulivyo.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
No comments:
Post a Comment