Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, hatuwezi kuishi kwa kujitegemea
wenyewe kwa kila kitu. Hivyo mahusiano yetu na wengine ni moja ya vitu
muhimu sana kwetu ili kuweza kuwa na maisha bora.
Falsafa ya ustoa inatufundisha jinsi ya kutengeneza mahusiano bora na
wale wanaotuzunguka kwa kuimarisha mahusiano yetu na ushirikiano kwenye
mambo mbalimbali.
Njia bora ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano ni kuangalia tabia
nzuri zilizopo ndani ya wengine badala ya kuangalia mabaya pekee. Pia
kuangalia namna ya kushirikiana na siyo kupingana.
Marcus ana maneno mazuri ya kutuambia kuhusu mahusiano;
Say to yourself first thing in the morning: I shall meet with people
who are meddling, ungrateful, violent, treacherous, envious, and
unsociable. They are subject to these faults because of their ignorance
of what is good and bad. But I have recognised the nature of the good
and seen that it is the right, and the nature of the bad and seen that
it is the wrong, and the nature of the wrongdoer himself, and seen that
he is related to me, not because he has the same blood or seed, but
because he shares in the same mind and portion of divinity. So I cannot
be harmed by any of them, as no one will involve me in what is wrong.
Nor can I be angry with my relative or hate him. We were born for
cooperation, like feet, like hands, like eyelids, like the rows of upper
and lower teeth. So to work against each other is contrary to nature;
and resentment and rejection count as working against someone. – Marcus
Aurelius, Meditations, 2.1
Jiambie hili kitu cha kwanza asubuhi: Leo nakwenda kukutana na watu
ambao ni waovu, wasio na shukrani, wenye fujo, wasaliti, wenye wivu na
wasiojali. Watu hao wako hivyo kwa sababu hawajui kipi kizuri na kipi
kibaya. Lakini mimi natambua asili ya uzuri na nimeona kipi sahihi na
asili ya ubaya na kuona kipi kisicho sahihi na asili ya wanaofanya ubaya
na kuona wana uhusiano na mimi, kwa sababu wana damu sawa na yangu na
tunashirikiana mawazo yetu. Siwezi kuumizwa na yeyote kwa sababu hakuna
anayeweza kunihusisha kwenye ubaya wake. Pia siwezi kuwa na hasira au
kumchukia ndugu yangu. Sote tumezaliwa kwa ushirikiano, kama miguu,
mikono, kope za macho, meno ya juu na ya chini. Hivyo kufanya kazi kwa
kupingana ni kinyume na asili na chuki na kukataana ni kufanya kazi
kinyume na wengine.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
No comments:
Post a Comment