Tabia njema ni moja ya misingi muhimu sana kwenye falsafa ya ustoa.
Kadiri unavyojijengea na kuishi kwa tabia njema, ndivyo
unavyojitengenezea maisha bora na yenye furaha wakati wote. Tabia njema
ndiyo zao la furaha. Kwenye ustoa, tabia njema ni pale unapoishi na
kusimamia yale yenye maana kwako na kwa wengine, na kuachana na yale
yasiyo na maana.
Kwenye ustoa kuna tabia njema kuu nne;
HEKIMA; Ubora katika kufikiri na kufanya maamuzi.
UJASIRI; Uwezo wa kukabiliana na hatari kwa usahihi.
HAKI; Ubora katika mahusiano yetu na wengine.
KIASI; Uwezo wa kudhibiti hisia na tamaa.
Marcus ana haya ya kutuambia kuhusu tabia njema;
If you can find anything in human life better than justice,
truthfulness, selfcontrol, courage […] turn to it with all your heart
and enjoy the supreme good that you have found […] but if you find all
other things to be trivial and valueless in comparison with virtue, give
no room to anything else, since, once you turn towards that and divert
from your proper path, you will no longer be able without inner conflict
to give the highest honour to what is properly good. It is not right to
set up as a rival to the rational and social good anything alien to its
nature, such as the praise of the many, or positions of power, wealth,
or enjoyment of pleasures. – Marcus Aurelius, Meditations, 3.6
Kama unaweza kupata kitu bora kwenye maisha ya mtu zaidi ya haki,
ukweli, kujidhibiti na ujasiri, kishikilie sana kitu hicho. Lakini kama
utakuta vitu vingine ni visivyo na maana ukilinganisha na tabia njema,
usitoe nafasi kwa kitu kingine bali tabia hizo njema. Kwa sababu
utakapoacha njia yako sahihi hutaweza tena kuzingatia yale ambayo ni
mazuri kwako. Siyo sahihi kuleta upinzani kati ya fikra sahihi na vitu
vya nje kama sifa kutoka kwa wengine, nafasi za madaraka, utajiri na
kufurahia raha.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
No comments:
Post a Comment