Je, Ungependa Kupata Utulivu Wa Akili?
Wahenga waliwahi kusema“ Usipoziba Ufa Utajenga Ukuta”.
Hakuna anayeweza kubisha kwamba kumekuwa na ukuaji mkubwa sana wa teknolojia kwenye zama tunazoishi sasa.
Kuna maendeleo makubwa ambayo yametokea tangu kuanza kwa karne ya 21 ambayo hakuna aliyetegemea yangetokea kwa kasi kubwa hivyo.
Nani alidhani angeweza kuwasiliana na mtu aliye bara la mbali kwa kuonana uso kwa uso bila hata ya kutumia gharama kubwa?
Nani alifikiri vitabu vyote duniani vingeweza kuweka mtandaoni na ikawa rahisi mtu kuvipata na kuvisoma?
Nani alifikiri kungekuja simu za mkononi (simu janja) ambazo unaweza kuzitumia kufanya kila kitu kama unavyotumia kompyuta, kuanzia kuwasiliana, kutunza kumbukumbu, kupiga picha, kurekodi sauti na video, kuuza na kununua na hata kujifunza?
Haya ni maendeleo makubwa, ambayo mtu aliyefariki kwenye karne ya 20, akifufuliwa leo atashangaa mno kwa maendeleo haya na angetegemea kuona maisha ya watu yakiwa bora kutokana na maendeleo haya makubwa.
Lakini hapo ndipo atakaposhangazwa zaidi, kwani licha ya maendeleo makubwa ya teknolojia atakayokuwa ameyaona, atagundua maisha ya watu yako hovyo kuliko kipindi ambacho teknolojia hizo hazikuwepo.
Atashangaa kuona watu wakiwa wamechoka, wana msongo na hawana muda kabisa.
Atashangaa kuona watu wakitumia muda wao mwingi kwenye simu zao, kwa mambo ambayo hayana manufaa kwao.
Atashangaa jinsi watu wanaonena wivu kwa mambo ambayo wanayaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Ujumbe atakaokuwa ameupata ni mmoja, kwamba teknolojia hizi mpya ambazo zina nguvu ya kufanya maisha ya wengi kuwa bora, zimegeuka kuwa gereza lililowafungia wengi na hawana tena uhuru wa kuyaishi maisha yao.
Ni dhahiri kwamba teknolojia mpya, hasa simu janja na mitandao ya kijamii, vimekuwa tatizo kubwa kwa wengi. Kila mtu analalamika jinsi vitu hivyo vinavyochukua muda mwingi, kuleta uchovu na hata msongo.
Wanaotengeneza na kuendesha teknolojia hizo hawajali kuhusu hilo, kwani kadiri unavyozitumia kwa muda mrefu, ndivyo wao wanavyopata faida. Hivyo wamejipanga kuhakikisha watumiaji wanaendelea kuwa wafungwa kwenye teknolojia hizo.
Na kwa kuwa teknolojia hizi ni mpya, hakuna mwenye uzoefu wa jinsi ya kukabiliana nazo, hivyo watu wanaingia kwenye teknolojia hizo mpya kwa kuhadaiwa watanufaika sana, lakini kinachotokea ni wanageuzwa kuwa wafungwa.
Leo nina habari njema mdau wangu , habari hizo ni kupatikana kwa mwongozo wa kuzitumia teknolojia hizi mpya vizuri na ukombozi wa ufungwa ambao teknolojia hizo zimetengeneza kwako.
Kupitia " DARASA ONLINE " MAISHA NA MAFANIKIO utajifunza jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo.
Mungu akubariki sana.
WASILIANA NAMI HARAKA NIKUUNGE
( WhatsApp + 255 716924136 ) / + 255 755400 128 / + 255 688 361539 / + 255
No comments:
Post a Comment