Siri Ambayo Itaharakisha Safari Yako Ya Mafanikio.
Picha linaanzia hapa,
Mstari unachorwa kati ya wale wanaofika mbali na wale ambao hawafiki mbali.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa.
Na kuna mambo mengi sana watu wanajaribu kuyatofautisha katika makundi haya mawili.
Lakini moja ya eneo muhimu sana ambalo linafanya watu wafanikiwe sana na wengine wasifanikiwe ni namna wanavyotumia akili zao kufikiria kufanya mambo na kupata mawazo, lakini kuna aina mbili kisayansi ambazo zinaweza kutofautisha makundi haya ya watu wawili.
Aina ya kwanza tunaita GROWTH MINDSET na aina ya pili tunaita FIXED MINDSET, hizi ni aina mbili za watu wanavyofikiri labda kitu cha kujiuliza MINDSET ni nini?.
MINDSET ni mfumo wa kufikiri ambao umeshajengeka ndani yako na hauitaji kujadiliana nao ili kupata matokeo.
Kwa maneno mengine unapokuwa na FIXED MINDSET, kwenye jambo Fulani ni kwamba jambo lolote linapotokea ubongo wako unakuwa umeshaamua utafanya nini au utachukua hatua gani.
Lakini kwenye GROWTH MINDSET, tunasema ni ile hali ambayo ubongo wako unakuwa umeshajiandaa kupokea taarifa tofauti na zile ambazo hazikuwepo hapo kabla.
Ukweli ni kwamba watu wanaofanikiwa ni wale wenye GROWTH MINDSET.
Watu wenye GROWTH MINDSET, ni kwamba wako tayari kuanza kujifunza , ulishawahi kukutana na mtu ambaye hataki kabisa kujifunza anaamini yeye anajua kila kitu huyo hawezi kufanikiwa.
Mtu ambaye anayefanikiwa kwenye GROWTH MINDSET ni mtu ambaye anasema ni kweli ninajua lakini ninahitaji kujua zaidi, ni mtu ambaye pia yupo tayari kuona watu wengine wanaweza kuliko yeye, mtu anayefanikiwa ni Yule anayesema ni kweli mimi ni mtaalamu kwenye uhandisi lakini ninaamini yupo mtu mtaalamu kwenye jambo la biashara kwa maneno mengine anaamini watu wengine wanaujuzi ambao yeye hana, na anauhitaji kukamilisha kile kitu ambacho anataka kukifanya lakini unapokuwa mtu wa FIXED MINDSET hutofanikiwa.
Watu wa FIXED MINDSET, moja ya sifa yao kubwa ni kwamba kila wakati wanajiona wao ni watu wanaojua sana, wanajiona wao ni watu wenye utaalamu kuliko watu wengine lakini kama kweli unataka kufanikiwa kwenye eneo lako wanasema hivii siku zote unapotaka kufanikiwa tambua kwamba chochote unachokijua sasa hivi ni kidogo sana kuliko kile ambacho unatakiwa kukijua kwa maana nyingine unakuwa tayari kujifunza na kusonga mbele katika kufahamu kile kitu ambacho unakitaka, lakini kuna jambo ambalo unaweza kulifanya kwa haraka sana, ili kutoka kwenye FIXED MINDSET na kuelekea kwenye GROWTH MINDSET.
Jambo la kwanza, Kila siku tenga muda angalau wa nusu saa wa kujifunza kitu kipya katika eneo lako la utaalamu ambalo unaliishi kwa maneno mengine tafuta vitabu vitakavyokusaidia kupiga hatua, au tafuta mtu ambaye utaweza kuzungumza naye lakini hakikisha kila siku kuna jambo jipya ambalo unajifunza katika kukuza ufahamu wako.
Jambo la pili, Jaribu kila siku kujiuliza hivi ninasonga mbele au ninarudi nyuma kwa maneno mengine jaribu kujikagua na kujifanyia review yakuona kama unapiga hatua au haupigi hatua kwenye maisha yako, ukifanya mambo haya mawili kila siku yatakusaidia kutoka kwenye FIXED MINDSET kwenda kwenye GROWTH MINDSET.
Lakini siku zote hasara ya kuwa na FIXED MINDSET, ni kwamba utafanya mambo yale yale kwa namna ile ile bila kupata matokeo tofauti, wataalamu walisema kwamba kama utafanya jambo lile lile kwa namna ile ile utapata matokeo yale yale.
Kwa hiyo GROWTH MINDSET, inasema sijui kama ninavyotakiwa kujua kwa maneno mengine nipo tayari kujifunza, unapomzungumzia WARREN BUFFET, mtaalamu mkubwa kwenye mambo ya uwekezaji, unapomzungumzia BILLGATE hao wote wana operate kwenye GROWTH MINDSET.
Wanajifunza jambo jipya kila siku wanasoma kitu kipya cha kuwakuza .
Je, LEO uko tayari kusoma kitu kipya ili kukuza ubongo wako?
KARIBU UJIUNGE SASA " DARASA LA MAISHA NA MAFANIKIO " ONLINE ILI UJIFUNZE SIRI ZA MAISHA NA MAFANIKIO KWA MAPANA NA MAREFU
WASILIANA NAMI SASA KOCHA MWL. JAPHET MASATU
( WhatsApp + 255 716924136 ) / + 255 755 400128 / + 255 688 361 539
EMAIL : japhetmasatu@gmail.com
No comments:
Post a Comment