- Ipo njia moja ya kupata chochote unachotaka na njia hiyo ni kuomba. Ombeni na mtapewa ni siri muhimu ya mafanikio kwenye biashara. Kama kuna kitu unataka, omba, na wengine watakuwa tayari kukupa. Huwezi kupata kitu bila kuomba.
- Unapoomba kazi, badala ya kutuma maombi kama wengine wanavyofanya, tafuta mikutano na wahusika wa eneo unalotaka kufanya kazi. Kwa kutumia mtandao wa kijamii wa LinkedIn, unaweza kukutana na mtu yeyote na ukaongeza nafasi zako za kupata kazi unayotaka.
- Biashara ni watu, haijalishi unajua nini, bali unamjua nani na nani anakujua wewe. Hivyo kazana kukuza zaidi mtandao wako wa watu unaowajua na wanaokujua.
- Mchukulie kila mtu unayekutana naye kama mtu mashuhuri, jua ni mtu muhimu, muoneshe umuhimu na watu watapenda kukutana na wewe. Ili kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kutengeneza marafiki wengi.
- Kutana na watu, furahia na jifunze. Weka kipaumbele chako katika kujenga mahusiano imara kwenye biashara yako na kazi yako, fanya kile ambacho unapenda ukiwa umezungukwa na watu unaowapenda. Pia jifunze kupitia wale ambao unafanya nao kazi na wanaokuzunguka.
- Kuwa mtu wa shukrani, kila unapokutana na mtu, au mtu anapokufanyia kazi, chukua muda wa kumwandikia ujumbe wa shukrani, inaimarisha zaidi mahusiano yako.
- Wale uliosoma nao shule moja au chuo kimoja ni watu muhimu sana kwenye mafanikio yako. Kuwa nao karibu na tengenezeni mahusiano bora, kila mtu anaweza kunufaika kupitia kazi za wengine. Kama hakuna umoja wa wale mliosoma pamoja, una fursa nzuri ya kuuanzisha.
- Wafuatilie watu baada ya kukutana nao. Unapokutana na kujuana na mtu mara ya kwanza, endelea kuwafuatilia kwa mawasiliano, hili linaimarisha mahusiano mnayokuwa mmeanzisha.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Thursday, June 27, 2019
MAHUSIANO NI MUHIMU KULIKO BIDHAA KATIKA BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment