Lakini
pia biashara huwa inakuwa na tabia zake, ambazo zinaweza kuifanya
ifanikiwe zaidi au kuizuia isifanikiwe. Tabia hizi za biashara huwa
zinatokana na tabia ambazo mwanzilishi wa biashara hiyo anazo
Na
hii ndiyo maana kwenye kila biashara kuna utaratibu na utamaduni fulani
uliopo, ambao huwa ni mgumu sana kubadilisha. Hata wafanyakazi wapya
wanapokuja kufanya kazi kwenye biashara hiyo, baada ya muda hujikuta
wameshavaa utamaduni huo wa biashara.
Utaratibu
na utamaduni uliojengeka kwenye biashara nyingi huwa ni matokeo ya
tabia za mwanzilishi wa biashara, huwa siyo kitu ambacho kimetengenezwa
kwa makusudi ambacho kinaweza kuwa na msaada kwenye biashara hiyo.
Hivyo
unakuta biashara imejijengea tabia ambazo siyo nzuri na zinakuwa
kikwazo kwa maendeleo ya biashara hiyo. Ukiangalia tabia za biashara
hiyo, zinakuwa zinaendana sana na tabia za mwanzilishi wa biashara hiyo.
Mfano
kama mwanzilishi wa biashara ni mzito kwenye kufanya maamuzi, basi
ufanyaji wa maamuzi wa kila mtu kwenye biashara unakuwa ni mzito sana.
Maamuzi hayafanyiki kwa wakati na biashara inazikosa fursa nzuri za
kukua zaidi.
Kama
mwanzilishi wa biashara hawezi kupangilia vitu vyake vizuri kwenye
maisha yake binafsi, unakuta biashara nayo haina mpangilio mzuri, vitu
vipo hovyo hovyo na hakuna utaratibu wowote unaotumika kwenye kufanya
vitu.
Kama
mwanzilishi wa biashara ana tamaa, biashara nzima inaendeshwa kwa
tamaa, kila aliyepo kwenye biashara hiyo anakuwa na tamaa na kujali
mambo yake zaidi kiliko ya biashara.
Hivyo
popote ambapo biashara imekwama, kwa hakika ndipo ambapo mmiliki wa
biashara hiyo amekwama. Biashara haiwezi kukua zaidi ya ukuaji wa
mmiliki wa biashara hiyo.
Suluhisho pekee la changamoto hii ya biashara kuwa na tabia zinazoizuia kukua, ambazo zimetoka kwa mwanzilishi wa biashara hiyo ni kuwa na mfumo sahihi wa kuendesha biashara.
ReplyDeleteBiashara inapoendeshwa kwa mfumo, inakuwa na tabia zake yenyewe ambazo ni bora na haziathiriwi na tabia binafsi za mmiliki wa biashara au mfanyakazi anayefanya kazi kwenye biashara hiyo.
Mfumo unaweka nafasi za kazi na majukumu ambayo mtu anapaswa kuyatekeleza. Lakini pia mfumo unaeleza jinsi ambavyo mtu anapaswa kutekeleza majukumu hayo.
Hivyo mtu yeyote anapokuwa kwenye biashara hiyo, anategemewa kufanya na kuzalisha matokeo ya aina moja, ambayo yanasimamiwa na mfumo.
Rafiki, kama unataka biashara yako isiathiriwe na tabia zako binafsi, kama unataka kuacha kuwa kikwazo kwenye ukuaji wa biashara yako kama ulivyo sasa, suluhisho ni mfumo.