Kwenye fizikia, kuna kanuni tatu kuu za mwendo ambazo mwanasayansi Isaac Newton alizigundua.
Kanuni ya kwanza inasema kitu kilichopo kwenye mwendo kinaendelea kuwa kwenye mwendo mpaka nguvu ya nje itakapotumika kukizuia.
Kanuni ya pili inasema nguvu ya kitu kilichopo kwenye mwendo inategemea uzito wake na mwendokasi wake.
Na kanuni ya tatu inasema kila mwendo huwa unazalisha upinzani.
Ni
kanuni ya tatu ambayo tunakwenda kuijadili hapa kwenye dakika moja ili
uelewe kwa nini baadhi ya vitu vinatokea kwenye maisha yako na hatua
sahihi kwako kuchukua.
Kila mwendo unaoanzisha, kuna mwendo mwingine utakaoanzishwa kuzuia mwendo huo.
Unapojaribu kwenda mbele, kuna mtu atajitokeza kukurudisha nyuma.
Hii ndiyo inasababisha mafanikio kuwa magumu. Kwa
sababu siku unayoamua kwamba unataka kufanikiwa, zitaibuka kila aina ya
nguvu kukupinga, kutaibuka kila kikwazo kwenye njia yako ya mafanikio.
Unapojua
hili, unajipanga kwa upinzani kwa kila hatua unayopanga kupiga na
hujidanganyi kwamba mambo yataenda vizuri yenyewe kama wengi
wanavyofanya.
Usishangae pale ambapo marafiki ulionao sasa watageuka kuwa maadui zako pale unapotangaza kwamba unataka kufanikiwa sana. ulipokuwa
kawaida mlikuwa marafiki, unapopanga kupiga hatua zaidi wanakuwa
maadui, hiyo ni kanuni ya asili, huwezi kupingana nayo.
Usikubali
kipingamizi chochote kikuzuie wewe kupiga hatua zaidi kwenye maisha
yako, jua kwa kila hatua utakayopanga kuchukua kuna kipingamizi
kitaibuka na hivyo jiandae kukivuka.
No comments:
Post a Comment