Kubadili tabia ambayo umeshazoea kuiishi kila siku ni kitu kigumu
mno. Watu wamekuwa wanatumia motisha mbalimbali kwao na hata kwa wengine
ili waweze kubadili tabia. Moja ya motisha ambayo imekuwa inatumika ni
zawadi, kwamba mtu akibadili tabia yake basi anapata zawadi, labda ni
ongezeko la mshahara au kupewa bonasi fulani.
Lakini motisha hii ya zawadi imekuwa haina nguvu sana. Kwa wengi
ambao wameshazoea tabia za zamani, zawadi haiwasukumi kubadilika. Mfano
kama una wafanyakazi ambao wanachelewa kukamilisha majukumu yao, unaweza
kuwapa motisha kwamba atakayewahi kukamilisha anapewa ongezeko la
fedha, lakini wachache sana watakaokamilisha kwa muda.
Ipo motisha nyingine ambayo ina nguvu sana ya kubadili tabia, kwa
sababu ni motisha inayoumiza. Motisha hii ni mtu kupoteza fedha iwapo
ataendelea na tabia ya zamani. Hakuna mtu anayepoteza fedha na hivyo
tishio la kupoteza fedha linawafanya watu walazimike kubadilika. Kwa
mfano huo hapo juu, ukiwaambia wafanyakazi kwamba yule anayechelewa
kukamilisha majukumu yake kwa muda, anakatwa fedha kwenye malipo yake,
utashangaa jinsi ambavyo wote wanakamilisha kwa muda.
Tafiti za kisaikolojia zinaonesha kwamba watu wanasukumwa zaidi pale
panapokuwa na hatari ya kupoteza fedha kuliko panapokuwa na uwezekano wa
kupata kiasi kile kile cha fedha. Hii ni nguvu unayoweza kuitumia kwa
mabadiliko yako mwenyewe.
Kwa mfano kama kuna tabia ambayo umegundua ni sugu kwako, na ambayo
unajitahidi kuibadili huwezi, basi waambie watu wako wa karibu
wakufuatilie kwa karibu na kila utakapofanya tabia hiyo basi wakudai
kiasi fulani cha fedha.
Mfano kama una tabia ya kuwakatisha watu wakiwa wanaongea, waambie
watu wote wa karibu kwamba kila unapomkatisha mtu akiwa anaongea basi
akudai shilingi elfu 10. Ukishalipa watu wawili au watatu,
nakuhakikishia hutarudia tena, kupoteza fedha kutakuumiza na
kukushikisha adabu.
Kadhalika kwenye tabia nyingine kama ulevi au uvutaji wa sigara,
kutokufanya mazoezi, kula hovyo, kutumia maneno ya matusi na kadhalika.
Tabia yoyote inayokupa shida kubadili, ingiza fedha na utabadilika
haraka sana.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment