Biashara
nyingi hazifai kuuza kwa sababu zinaendeshwa kwa vurugu. Kwa nje
biashara inaweza kuonekana inakwenda vizuri, lakini kwa ndani mambo ni
vurugu. Hakuna mpangilio wowote wala mfumo ambao unafuatwa. Kila kitu
kinafanywa kwa namna ambavyo mtu anajisikia kufanya. Hakuna viwango
vyovyote vinavyofanyiwa kazi.
Wateja
wanaokuja kupata huduma kwenye biashara, hawaji kwa sababu ya biashara,
bali wanakuja kwa sababu ya mtu. Na wengine wanasema wazi kwamba
wanataka kuhudumiwa na fulani tu.
Wafanyabiashara
wengi hufurahia pale wateja wanapotaka wahudumiwe na wao tu, wakiona ni
wateja wanawaamini na kuwakubali sana. Lakini wasijue kama hicho ndiyo
kifungo chao.
Huwezi kuuza biashara ambayo haiendeshwi kwa mfumo na kila kitu kinamtegemea mmiliki wa biashara hiyo.
Na biashara ya aina hii inakuwa mzigo kwa mmiliki na kumnyima uhuru.
Karibu
tujifunze jinsi ya kutengeneza biashara inayokupa uhuru na unayoweza
kuiuza muda wowote na hili litakuwezesha kuwa na biashara bora na
isiyokutegemea kwa kila kitu. Na hata kama hutaki kuuza biashara yako,
kitendo cha biashara kuweza kujiendesha yenyewe bila ya wewe kuwepo,
utakuwa ushindi mkubwa sana kwako.
No comments:
Post a Comment