- THE SCIENCE OF GETTING RICH Kilichoandikwa Na Wallace D. Wattles; Kila mtu anaweza kuwa tajiri bila ya kujali mazingira, kipato, kipaji au hata shughuli anayofanya. Ipo namna ya kufikiria na kufanya ambayo kila mtu anaweza kuitumia na akapata utajiri mkubwa kwenye maisha yake.
- THE MASTER KEY SYSTEM Kilichoandikwa Na Charles Haanel. Hiki ni kitabu ambacho kinatufundisha jinsi ya kutumia nguvu kubwa iliyopo ndani yetu kuweza kupata chochote tunachotaka kwenye maisha yetu. Nguvu hii kubwa iliyopo ndani yetu, ni fikra zetu.
- THE 5 AM CLUB; Own Your Morning, Elevate Your Life kilichoandikwa na Robin Sharma ambaye anatushirikisha umuhimu wa kuianza siku yako asubuhi na mapema, wakati watu wengine bado wamelala. Anasema kwa kuimiliki asubuhi yako, utaweza kuyainua zaidi maisha yako.
- MILLIONAIRE SUCCESS HABITS: The Gateway To Wealth & Prosperity Ambacho Kimeandikwa Na Milionea Dean Graziosi. Kitu pekee kinachokuzia wewe usipate yale matokeo ambayo wengine wanayapata, ni tabia ambazo unaziishi sasa. Kama ukijua tabia za waliofanikiwa na ukaziishi, basi utaweza kupata matokeo ambayo wanayapata.
- HABITS OF A HAPPY BRAIN: Retrain Your Brain to Boost Your Serotonin, Dopamine, Oxytocin, & Endorphin Levels ambacho kimeandikwa na Loretta Graziano Breuning. Ubongo unazalisha kemikali nne ambazo ndizo zinaleta furaha kwenye maisha yetu. Kemikali hizi zinatofautiana kwa ufanyaji wake wa kazi, lakini mwisho wa siku zote zinaishia kuleta furaha. Kemikali hizo ni dopamini, serotonini, oksitosini na endofini.
- THE BLUE ZONES; Lessons For Living Longer From The People Who’ve Lived The Longest ambacho kimeandikwa na Dan Buettner. Kupitia utafiti wa mwandishi wa kitabu cha THE BLUE ZONES, yapo maeneo manne duniani ambayo yameonesha kuwa na watu wanaoishi miaka mingi kuliko maeneo mengine. Maeneo hayo ni Sardinia nchini Italy, Okinawa nchini Japan, Loma Linda Calfornia nchini Marekani na Nicoya nchini Costa Rica. Mwandishi ameshirikisha masomo ambayo ameondoka nayo kwenye kila eneo na jinsi ya kuyatumia kwenye maisha yetu ili tuweze kuishi miaka mingi.
- FLOW: The Psychology of Optimal Experience kilichoandikwa na Mihaly Csikszentmihalyi. Kitabu hichi kinatufundisha jinsi ambavyo tunaweza kufikia ufanisi mkubwa na furaha kwenye chochote ambacho tunafanya, iwe kikubwa au kidogo, tunakipenda au hatukipendi.
- PEAK; Secrets from the New Science of Expertise kilichoandikwa na Anders Ericsson. Kitabu hiki kinatupa siri za kisayansi za kuweza kufikia ubobezi mkubwa kwenye kitu chochote tunachochagua kufanya kwenye maisha yetu. Kitabu hiki kimetokana na tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa kwenye eneo la ubobezi na hivyo kimekuja na majibu sahihi ya hatua unazopaswa kuchukua ili kufikia ubobezi.
- 21 LESSONS FOR THE 21ST CENTURY ambacho kimeandikwa na mwanahistoria Yuval Noah Harari. Kwenye kitabu hiki, Yuval amezichambua changamoto kubwa 21 zinazotukabili kwenye karne hii ya 21 na kupendekeza hatua tunazopaswa kuchukua ili tusiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.
- BECOMING SUPERNATURAL: How Common People Are Doing the Uncommon kilichoandikwa na Dr. Joe Dispenza. Hiki ni kitabu ambacho kinatufundisha namna ya kutumia nguvu kubwa iliyopo ndani ya kila mmoja wetu kufanya makubwa na miujiza kwenye maisha yetu.
- STEALING FIRE: How Silicon Valley, the Navy SEALs, and Maverick Scientists Are Revolutionizing the Way We Live and Work kilichoandikwa na waandishi Steven Kotler na Jamie Wheal. Hiki ni kitabu kinachotuonesha mapinduzi makubwa ya kiutambuzi yanayoendelea duniani, ambayo wachache wanaoyaelewa wanayatumia kufanya makubwa sana kwenye kazi zao na hata maisha yao kwa ujumla.
- THE CODE OF THE EXTRAORDINARY MIND: 10 Unconventional Laws to Redefine Your Life and Succeed On Your Own Terms ambacho kimeandikwa na Vishen Lakhiani. Hiki ni kitabu ambacho kinatupa mtazamo wa tofauti kabisa wa namna tunavyoyachukulia maisha yetu. Katika kitabu hiki tunajifunza kwa nini sheria na kanuni nyingi tunazoziishi siyo sahihi au zimepitwa na wakati. Na muhimu zaidi, kitabu kinatufundisha jinsi ya kuwa na maisha yasiyo ya kawaida, yaani kuwa na maisha ya kipekee kwetu, kwa namna tunavyotaka sisi wenyewe.
- CAN’T HURT ME: Master Your Mind and Defy the Odds ambacho kimeandikwa na Mwanajeshi mstaafu David Goggins. Kupitia historia na magumu aliyopitia kwenye maisha yake mpaka kufikia ukomando, Goggins anatushirikisha jinsi ya kutangaza vita na maisha yetu wenyewe ili kufanikiwa. Kwenye kitabu hiki tunajifunza jinsi ya kwenda kwenye vita dhidi yetu wenyewe, yaani tunakwenda kupambana na sisi wenyewe, ili tuache kujihujumu na kujirudisha nyuma, tufungue uwezo wetu mkubwa na kuutumia kufanikiwa zaidi.
- SEEKING WISDOM; From Darwin to Munger kilichoandikwa na Peter Bevelin. Mwandishi amefanya kazi kubwa ya kukusanya hekima za watu mbalimbali walioweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yao na kwenda kinyume na mazoea. Kuanzia mwanabaiolojia Charles Darwin ambaye alileta mapinduzi makubwa kwenye baiolojia kwa kufikiri tofauti, mpaka kwa mwanafalsafa mwekezaji Charles Munger ambaye pamoja na mshirika wake Warren Buffett wameweza kupata mafanikio makubwa sana kwenye uwekezaji, kuliko wawekezaji wengine wote.
- THE LAWS OF HUMAN NATURE ambacho kimeandikwa na Robert Greene. Kwenye kitabu hiki, Green ametupa sheria 18 za kuijua asili ya binadamu, akitupa mifano halisi iliyowahi kutokea kwa watu waliozingatia sheria hizi na wakafanikiwa au walizipuuza na kushindwa.
- HOW TO GET RICH: One of the World’s Greatest Entrepreneurs Shares His Secrets ambacho kimeandikwa na Felix Dennis. Felix Dennis alikuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa sana katika sekta ya uchapishaji wa majarida. Felix alianzia chini kabisa, bila ya elimu kubwa wala mtaji, lakini aliweza kuingia kwenye biashara ya uchapishaji wa majarida na kuweza kuwa tajiri mkubwa sana nchini Uingereza. Katika kitabu hiki, Felix anatushirikisha safari ya mafanikio yake, makosa aliyofanya, bahati alizopata na ushauri muhimu kwa wote ambao wanataka kupata utajiri kwenye maisha yao.
- YOUR BRAIN AT WORK: Strategies for Overcoming Distraction, Regaining Focus, and Working Smarter All Day Long ambacho kimeandikwa na David Rock. Kwenye kitabu hiki, David ametushirikisha yale muhimu unayopaswa kujua kuhusu ubongo wako, jinsi unavyofanya kazi na njia bora ya kuutumia ili kuondokana na usumbufu, kuongeza umakini na kufanya kazi zako vizuri pamoja na kuwa na utulivu siku nzima.
- TRACTION; Get A Grip On Your Business kilichoandikwa na Gino Wickman. Kwenye kitabu hiki, Gino anatuambia kama tutazingatia maeneo sita muhimu ya biashara ambayo ameyafundisha, biashara zetu zitakua na kuwa huru, kiasi kwamba hazitegemei uwepo wetu wa moja kwa moja ndiyo ziweze kwenda.
- THE BULLETPROOF DIET: Lose Up to a Pound a Day, Reclaim Energy and Focus, Upgrade Your Life, Kilichoandikwa na Dave Asprey. Kwenye kitabu hiki, Dave siyo tu anatupa dayati ya kufuata, bali anatusaidia kujenga mfumo mpya wa maisha kwenye ulaji. Huu ni mfumo ambao mtu ukiufuata, unapunguza uzito wa mwili bila ya shida, unakuwa na nguvu muda wote na afya yako inakuwa bora. Mpangilio wa ulaji aliouweka kwenye kitabu hiki unaupatia mwili virutubisho sahihi unavyohitaji na kuzuia mwili kwenda kwenye hali ya uhitaji mkubwa ambao unawasukuma wengi kula zaidi na kuongeza uzito.
- THE E-MYTH REVISITED: Why Most Small Businesses Don’t Work and What to Do About It, mwandishi Michael E. Gerber anatupa maarifa sahihi ya kutuwezesha kuanzisha na kuendesha biashara zetu kwa mfumo ambao zinafanya vizuri na kutupa uhuru mkubwa. Michael anasema uhuru kwenye biashara upo kwenye mfumo. Kama unaendesha biashara na huna mfumo, huna biashara, bali una kazi, na hiyo ni kazi mbaya kuliko zote.
- WHAT GOT YOU HERE WON’T GET YOU THERE: How Successful People Become Even More Successful mwandishi Marshall Goldsmith anatuonesha jinsi ambavyo tabia zetu zinatuzuia kufanikiwa zaidi. Anaanza kwa kutuonesha jinsi ambavyo tabia zetu zinakuwa kikwazo kwetu, kisha anatupa hatua saba za kujenga tabia bora kwa mafanikio yetu.
- DIGITAL MINIMALISM: Choosing a Focused Life in a Noisy World ambacho kimeandikwa na Cal Newport. Mwandishi Cal Newport baada ya kuona changamoto kubwa ya simu janja na mitandao ya kijamii kwa wengi, amekuja na falsafa bora ya matumizi mazuri ya mitandao hii, ambayo itakuwa na manufaa kwetu na kuondokana na madhara ya mitandao hii. Falsafa hii haibadili kitu kimoja kwenye matumizi yetu ya simu janja na mitandao ya kijamii, bali inabadili mfumo wetu mzima wa maisha na jinsi tunavyoichukulia na kuitumia mitandao hii. Falsafa hii anaiitwa DIGITAL MINIMALISM na ameieleza kwenye kitabu hiki.
- THE URBAN MONK: Eastern Wisdom and Modern Hacks to Stop Time and Find Success, Happiness, and Peace ambacho kimeandikwa na Pedram Shojai. Pedram amekuwa mtawa wa falsafa ya Taoism na pia daktari wa tiba za mashariki. Kupitia uzoefu wake wa utawa na kutibu watu, amegundua kuna changamoto kubwa kumi ambacho tunazipitia binadamu kwa zama tunazoishi. Changamoto hizo ni msongo, muda, nguvu, usingizi, mtindo wa maisha wa kukaa, ulaji, kutengana na asili, upweke, fedha na kukosa kusudi la maisha. Kupitia kitabu chake, Pedream amejadili kila changamoto na kutupa hekima za kuzikabili changamoto hizo kutoka kwenye falsafa za mashariki.
- HIGH PERFORMANCE HABITS: How Extraordinary People Become That Way ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Brendon Burchard. Kwenye kitabu hiki, Brendon ametushirikisha hatua sita za kujijengea kama tunataka kufanikiwa zaidi. Pia ametutahadharisha na tabia tatu zinazoharibu kabisa mafanikio yetu na tabia moja kuu inayobeba tabia zote za mafanikio.
- BUILT TO SELL: Creating a Business That Can Thrive Without You ambacho kimeandikwa na mwandishi John Warrillow. Kupitia kitabu hiki, John ametushirikisha hatua nane za kutengeneza biashara inayoweza kujiendesha bila ya uwepo wako na pia unayoweza kuiuza na kupata fedha zaidi.
- THE CHECKLIST MANIFESTO: How to Get Things Right ambacho kimeandikwa na Daktari bingwa wa upasuaji Atul Gawande. Kwenye kitabu hiki, Atul ametuonesha jinsi ambavyo sisi binadamu tunafanya makosa kwenye kazi zetu za kila siku, na njia rahisi ya kupunguza makosa hayo ambayo ni kutumia orodha (checklist).
- 101 CRUCIAL LESSONS THEY DON’T TEACH YOU IN BUSINESS SCHOOL kilichoandikwa na Chris Haroun. Kwenye kitabu hiki tumejifunza siri 101 za mafanikio kwenye biashara na maisha kwa ujumla ambazo hazifundishwi kwenye shule ya biashara.
- JUST RUN IT!: Running an Exceptional Business is Easier Than You Think kilichoandikwa na Dick Cross. Kupitia kitabu hiki tunajifunza mfumo rahisi wa kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa huku ukiwa na uhuru.
- THE MIRACLE MORNING: The Not-So-Obvious Secret Guaranteed to Transform Your Life: Before 8AM, ambacho kimeandikwa na Hal Elrod. Kupitia kitabu hiki, Hal anatuonesha kwamba nguvu ya kuyabadili maisha yetu, kutoka umasikini na ukawaida mpaka kufika utajiri na mafanikio ipo ndani yetu. Na kwa kuwa kila mtu analalamika kwamba hana muda, Hal ametuonesha jinsi ambavyo kwa kutenga saa moja tu kila siku na kufanya vitu sita muhimu sana, maisha yako yanaweza kubadilika.
- STAND OUT: How to Find Your Breakthrough Idea and Build a Following Around It ambacho kimeandikwa na Dorie Clark. Kwenye kitabu hiki mwandishi anatushirikisha jinsi ambavyo tunaweza kujitofautisha na wengine kwa kile tunachofanya. Mwandishi anatufundisha njia ya kubobea sana kwenye kile tunachofanya kwa namna ambayo tutakuwa viongozi ambao wengine wanatuangalia na kujifunza kutoka kwetu (thought leader).
- GETTING EVERYTHING YOU CAN OUT OF ALL YOU’VE GOT: 21 Ways You Can Out-Think, Out-Perform, and Out-Earn the Competition ambacho kimeandikwa na kocha wa biashara Jay Abraham. Kwenye kitabu hiki, Jay ametushirikisha njia 21 za kuweza kufikiri, kufanya na kutengeneza kipato zaidi kuliko wengine kupitia kazi au biashara tunazofanya.
- THE ART OF PUBLIC SPEAKING ambacho kimeandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein. Kwenye kitabu hiki, waandishi wametushirikisha maarifa na mbinu sahihi za kuweza kuongea mbele ya wengine kwa kujiamini na kwa ushawishi ili tuweze kupata kile tunachotaka na hata kuwanufaisha wengine pia.
- HOW TO WRITE COPY THAT SELLS; The Step-By-Step System For More Sales, to More Customers, More Often kilichoandikwa na Ray Edwards. Mwandishi Ray ni mmoja wa waandishi mashuhuri wa matangazo na nakala za mauzo. Kupitia kitabu hiki anatushirikisha siri na mbinu muhimu ambazo tukizielewa na kuzitumia tutaweza kuandika nakala bora kabisa za kuuza chochote tunachouza.
- TO SELL IS HUMAN: The Surprising Truth About Moving Others kilichoandikwa na Daniel H. Pink. Kwenye kitabu hiki, mwandishi anatuonesha kwamba kila mtu sasa yupo kwenye mauzo na kwamba mauzo kwa sasa yamebadilika sana. Anatushirikisha misingi mipya ya kufanikiwa kwenye uuzaji pamoja na mbinu sahihi za kupata ushawishi kwa wengine.
- HOW TO BE A STOIC: Using Ancient Philosophy to Live a Modern Life kilichoandikwa na mmoja wa wastoa wa zama zetu Massimo Pigliucci. Ustoa ni Falsafa ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka elfu mbili sasa, ambayo lengo lake kubwa limekuwa kuwafanya watu kuwa na maisha bora, kwa kuishi kwa misingi sahihi. Hii ni falsafa ambayo kila mtu akiweza kuielewa na kuiishi basi lazima atakuwa na maisha bora.
- RICH DAD’S BEFORE YOU QUIT YOUR JOB: 10 Real-Life Lessons Every Entrepreneur Should Know About Building a Multimillion-Dollar Business ambacho kimeandikwa na Robert Kiyosaki. Kwenye kitabu hiki, Kiyosaki ametushirikisha mambo 10 ambayo mtu anapaswa kuwa na maandalizi nayo kabla hajatoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye ajira, wanatamani sana kutoka na kwenda kujiajiri, lakini wakiwaangalia wale waliowahi kutoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri, wanapatwa na hofu kubwa. Kwa sababu wengi wanakuwa hawajapiga hatua kubwa. Sasa iwe upo kwenye ajira na unataka kwenda kujiajiri au tayari umeshajiajiri, masomo haya kumi tunayokwenda kujifunza hapa yatakusaidia sana kuanzisha na kukuza biashara yako.
- FREELANCE TO FREEDOM: The Roadmap for Creating a Side Business to Achieve Financial, Time and Life Freedom kilichoandikwa na mpiga picha aliyeweza kutoka kwenye ajira mpaka kujiajiri mwenyewe na kufikia mafanikio makubwa. Mpiga picha huyo ni Vincent Pugliese akishirikiana na mke wake Elizabeth katika safari ya kutoka kwenye utumwa wa ajira pamoja na madeni mpaka kufikia uhuru wa kifedha, muda na hata maisha kwa ujumla. Kwenye hiki, Vicent anatushirikisha safari nzima ya maisha yake ya kutoka kwenye utumwa mpaka kwenye uhuru.
- RANGE: Why Generalists Triumph In A Specialized World kilichoandikwa na David Epstein. Kwenye kitabu hiki, David ametuonesha jinsi ambavyo hadithi ya kubobea haraka ambayo imekuwa inatumiwa na wengi kama mfano wa mafanikio isivyo sahihi. Ametushirikisha kwa kina jinsi ambavyo kutokubobea kwenye jambo moja kuna manufaa makubwa kwa mtu, hasa kwa maisha na mafanikio ya baadaye.
- STREET SMARTS: An All-Purpose Tool Kit for Entrepreneurs kilichoandikwa na waandishi na wafanyabiashara wawili ambao ni Norm Brodsky na Bo Burlingham. Norm na Bo wana uzoefu wa muda mrefu katika kuanzisha na kukuza biashara, na kupitia kitabu hiki wametushirikisha uzoefu wao katika biashara, wametupa mafunzo muhimu ambayo tukiweza kuyatumia tutapiga hatua sana kwenye biashara zetu. Kitabu hiki kina sura 17 na mwisho wa kila sura kuna mambo manne muhimu ya kuondoka nayo na kwenda kuyafanyia kazi.
- PROFIT FIRST: A Simple System To Transform Any Business From A Cash-Eating Monster To A Money-Making Machine kilichoandikwa na Mike Michalowicz. Mike anatuambia biashara nyingi zimekuwa zinaendeshwa bila ya kutengeneza faida, kitu kinachopelekea biashara hizo zife. Hivyo anatuambia njia pekee ya kuendesha biashara yenye mafanikio, ni kwa kuanza kupata faida kwanza kabla ya mengine yote. Mike anasema, faida kwenye biashara inapaswa kuanza kupatikana siku ya kwanza unapoanza biashara, na siyo kusubiri mpaka siku zijazo.
- SMALL GIANTS: Companies That Choose to Be Great Instead of Big ambacho kimeandikwa na Bo Burlingham. Kitabu hiki kimeandikwa kupitia utafiti uliofanyika kwa biashara ambazo zimechagua kuwa bora badala ya kuwa kubwa. Hizi ni biashara ambazo zilikuwa na nafasi ya kukua zaidi lakini wamiliki wa biashara hizo kuchagua kuzifanya zibaki kuwa biashara ndogo ambazo ni bora zaidi. Kwenye kitabu hiki utajifunza jinsi ambavyo tunaweza kuendesha biashara yako kwa ubora hata kama ni ndogo.
- FINANCIAL INTELLIGENCE; A Manager’s Guide to Knowing What the Numbers Really Mean kilichoandikwa na waandishi na washauri wa biashara Karen Berman, Joe Knight na John Case. Kupitia kitabu hiki tunajifunza kwa kina kuhusu namba za biashara na taarifa za kifedha unazopaswa kuzijua na kuzielewa. Haijalishi kama umeajiriwa, unafanya biashara au umejiajiri mwenyewe, bila ya kuzijua namba za biashara kwenye kile unachofanya, huna tofauti na mtu anayetembea gizani huku amefungwa kitambaa machoni.
- THIS IS MARKETING: You Can’t Be Seen Until You Learn To See kilichoandokwa na Seth Godin. Seth Godin anasifika kama mmoja wa wabobezi wa masoko katika zama tunazoishi sasa. Seth amekuwa akihubiri aina ya tofauti ya masoko, ambayo haimlengi kila mtu, bali inachagua kulenga watu wachache. Kwenye kitabu hiki, tunajifunza namna bora ya kufanya masoko yenye tija kwenye biashara zetu na maisha kwa ujumla, kwa sababu kila kitu kwenye maisha yetu kinahusu masoko.
- TRILLION DOLLAR COACH: The Leadership Playbook of Silicon Valley's Bill Campbell, kitabu hiki kimeandikwa na Alan Eagle, Eric Schmidt, na Jonathan Rosenberg. Hawa ni wakurugenzi wa makampuni ya teknolojia ambao waliwahi kufanya kazi na Kocha Bill Campbell ambaye ana mchango mkubwa sana kwenye ukuaji wa makampuni makubwa ya teknolojia duniani ambayo ni Google, Apple, Amazon, Facebook, Intuit na mengine mengi. Kitabu hiki kimeeleza maisha ya Bill pamoja na misingi yake ya ukocha wa mafanikio.
- THE INTELLIGENT ENTREPRENEUR: How Three Harvard Business School Graduates Learned the 10 Rules of Successful Entrepreneurship kilichoandikwa na Bill Murphy Jr. Kitabu hiki ni tofauti kabisa na vitabu vingine vya ujasiriamali, kwani kimetushirikisha sheria kumi za kufanikiwa kwenye ujasiriamali, kupitia hadithi za wajasiriamali watatu waliofuatiliwa kwa kipindi cha miaka kumi. Wajasiriamali hao walikuwa wahitimu wa shahada ya uzamili ya biashara (MBA) kutoka shule ya biashara ya chuo kikuu cha Havard (Havard Business School).
- START SMALL FINISH BIG: 15 Key Lessons to Start and Run Your Own Successful Business. Kitabu hiki kinaelezea hadithi ya aliyekuwa mwanzilishi wa migahawa inayoitwa SubWay ambayo ni migahawa maarufu duniani kwa vyakula vya haraka. Mwanzilishi huyo ambaye alikuwa ni Fred DeLuca aliweza kuanzisha biashara hiyo akiwa na umri wa miaka 17 pekee, kwa mtaji mdogo wa dola elfu moja (mwaka 1965) ambao alikopeshwa na rafiki yake.
- IT STARTS WITH PASSION: Do What You Love and Love What You Do ambacho kimeandikwa na Keith Abraham. Kupitia kitabu hiki Keith anatufundisha kwamba, hatuwezi kufanikiwa kwenye maisha kama hatupendi kile ambacho tunakifanya. Kama ndani yetu hakuna msukumo mkubwa unaoanza na upendo, hatuwezi kuhimili mikiki mikiki na changamoto tutakazokutana nazo kwenye safari ya mafanikio. Hivyo tunapaswa kujua kile ambacho tunakipenda na kukifanya na kama hatujui tunachopenda, basi chochote ambacho tunakifanya, tukipende sana.
- INDISTRACTABLE: How To Control Your Attention And Choose Your Life, ambacho kimeandikwa na Nir wa Eyal. Nir ni mtaalamu teknolojia na mwanasaikolojia pia, mtu ambaye amesoma tafiti nyingi zinazohusisha jinsi saikolojia wa mwanadamu inavyoweza kutekwa na kuwa tegemezi wa teknolojia. Kwenye kitabu chake cha INDISTRACTABLE, Nir anatuonesha jinsi ambavyo tunaweza kuondokana na mitego ya kisaikolojia iliyowekwa na makampuni ya teknolojia na kuweza kunasa umakini wetu na kuleta usumbufu kwetu.
- STILLNESS IS THE KEY ambacho kimeandikwa na Ryan Holiday. Ryan amekuwa akiandika vitabu vyake kutoka kwenye msingi wa falsafa ya ustoa na kuiweka kwa namna ambayo tunaweza kuiishi na kunufaika nayo kwenye zama tunazoishi sasa. Kwenye kitabu cha STILLNESS IS THE KEY, Ryan ametuonesha nguvu kubwa iliyopo kwenye utulivu, ambayo tukiijua na kuweza kuitumia basi itakuwa ufunguo wa mambo mengi kwenye maisha yetu. Tangu enzi na enzi, ukiangalia kila aina ya falsafa au dini, utulivu umekuwa unasisitizwa sana. Ni kupitia utulivu ndiyo tunaweza kufikiri sawasawa, kuiona picha kubwa na kujua hatua sahihi za kuchukua.
- THE SUBTLE ART OF NOT GIVING A F*CK: A Counterintuitive Approach to Living a Good Life ambacho kimeandikwa na Mark Manson. Kama jina lilivyo, mwandishi anatufundisha jinsi ya kuacha kujali yale yasiyotuhusu. Anachotuambia ni kwamba, maisha yetu yanakuwa magumu kwa sababu tunahangaika na mambo yasiyotuhusu au yaliyo nje ya uwezo wetu. Pia ameeleza jinsi ambavyo ushauri wa wahamasishaji wengi unavyowafanya watu wengi kuwa watumwa na kushindwa kuwa na maisha bora.
- SAPIENS: A Brief History of Humankind kilichoandikwa na mwanahistoria Yuval Noah Harari. Yuval amefanya kazi kubwa ya kuchimba historia kamili ya binadamu tangu miaka 70,000 iliyopita ambapo ndipo historia ya binadamu imeanza kuhesabiwa wakati mapinduzi ya kifikra yalipotokea. Miaka 12,000 iliyopita ndipo mapinduzi ya kilimo yalipotokea na miaka 500 iliyopita, mapinduzi ya sayansi yalianza, ambayo ndiyo tunayaishi mpaka sasa. Kwenye kila mapinduzi ambayo tumepitia, Yuval ameonesha mafanikio na changamoto mbalimbali.
- FOOLED BY RANDOMNESS: The Hidden Role of Chance in Life and in the Markets kilichoandikwa na mwanahisabati, mwanafalsafa na mwekezaji Nassim Nicholas Taleb. Taleb ameandika kitabu hiki kwa kushirikisha uzoefu wake kwenye uwekezaji kwenye soko la hisa, ambapo wachache wanaochukuliwa wamefanikiwa sana siyo kwa sababu ya ujanja wao au juhudi zao, bali ni kwa bahati tu. Taleb anakwenda mbali zaidi na kuonesha kwamba katika kila eneo la maisha, kuna bahati ambazo watu wanakutana nazo na zinawasaidia kupiga hatua. Lakini wakishapiga hatua wanasahau bahati hizo na kuona ni juhudi zao wenyewe. Kwa sisi kujua mchango wa bahati kwenye maisha yetu, tunaweza kujiweka kwenye upande mzuri wa bahati kuwa na manufaa kwetu.
- ATOMIC HABITS: An Easy & Proven Way to Build Good Habits & Break Bad Ones kilichoandikwa na James Clear. Mwandishi James Clear baada ya kupitia tafiti mbalimbali za kisayansi, kisaikolojia na kijamii, ameweza kuja na mfumo bora sana wa kujenga au kuvunja tabia yoyote ile. Mfumo huo una hatua nne ambazo mtu ukiweza kuzifuata, hakuna tabia itakayokushinda. Mfumo huo unapatikana kwenye kitabu hiki cha ATOMIC HABITS.
- HOOKED: How to Build Habit-Forming Products, kilichoandikwa na Nir Eyal ambaye anatuonesha jinsi ambavyo makampuni makubwa yanatumia saikolojia yetu sisi binadamu kutengeneza bidhaa na huduma ambazo tunasukumwa kuzitumia muda wote.Kupitia kitabu hiki unajifunza vitu viwili kwa wakati mmoja; kutengeneza bidhaa au huduma ambayo watu watasukumwa kuitumia muda wote na kuepuka kuwa mtumwa wa bidhaa na huduma ambazo zimetengenezwa kwa lengo la kukusukuma wewe kuzitumia, hasa pale zinapokuwa hazina manufaa kwako.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Monday, December 30, 2019
VITABU VIZURI VYA KUSOMA----HITS THE BOOKS
USIJISUMBUE KUWABADILISHA WATU , WATU HUWA HAWABADILISHWI
Watu
huwa hawapendi kubadilishwa, na wakigundua mtu anataka kuwabadilisha
basi wanaleta upinzani mkubwa kuhakikisha hilo halitokei.
Watu
huwa wanaweza kubadilika kama watachagua kubadilika wao wenyewe, lakini
siyo kulazimishwa kubadilika, hivyo ndivyo saikolojia ya binadamu
ilivyo.
Hivyo usijisumbue kumbadili mtu yeyote yule, hutaweza, utaishia kuibua tu migogoro isiyo na manufaa.
Kama
unataka mtu mwenye sifa fulani, mtafute mtu mwenye sifa hizo na siyo
kumchukua yeyote na kujiambia utambadilisha, unajidanganya.
Kwenye
mahusiano, iwe ni ya mapenzi au ndoa, chagua mtu ambaye sifa alizonazo
sasa unaweza kwenda nazo na siyo kujiambia utambadilisha.
Kwenye ushirikiano wa biashara au kazi, chagua kushirikiana na mtu ambaye sifa unazoziona sasa kwake unaweza kwenda nazo.
Na hata unapoajiri, angalia sifa ambazo mtu anazo na kama unaweza kwenda nazo.
Usijidanganye kwamba sifa fulani ambayo mtu anayo unaweza kuibadili, unatafuta matatizo wewe mwenyewe.
Mtu
mmoja amewahi kuulizwa anawezaje kuwafanya wafanyakazi wake kuwa na
tabia nzuri, alijibu kwa kusema; “siwaambii wafanyakazi wawe na tabia
nzuri, bali naajiri watu ambao tayari wana tabia nzuri”.
USITOE USHAURI KWA MTU AMBAYE HAJAKUOMBA , USICHUKUE USHAURI KWA AMBAYE HUJAMWOMBA.
Ushauri ni kitu ambacho unapaswa kuwa nacho makini sana wakati wa kutoa na hata kutokea.
Tuanze
na kutoa, kamwe usitoe ushauri kwa mtu ambaye hajakuomba umshauri,
unaweza kuona unamsaidia mtu huyo, lakini utakuwa unapoteza muda wako
bure. Watu huwa hawafanyii kazi ushauri ambao hawajautafuta wenyewe.
Unaweza kumwona mtu yupo kwenye hali fulani na kufikiri ushauri wako
utamsaidia, ukamshauri vizuri na ukashangaa hafanyii kazi yale
uliyomshauri. Hii ni kwa sababu mtu huyo hajawa na maumivu ya kutosha
kumsukuma kutaka kutoka pale alipo sasa na ushauri wako ni kelele tu
kwake. Mtu anayekuja kwako na kukuomba ushauri, ni mtu ambaye ameshaumia
vya kutosha na anataka njia ya kuondoka kwenye maumivu, huyu ukimshauri
anazingatia. Hivyo kama mtu hajakuomba ushauri, usijisumbue kutoa
ushauri wako.
Tukienda
kwenye kupokea ushauri, usichukue ushauri wa mtu ambaye hujamwomba
akushauri. Hii ni kwa sababu mtu anaweza kuona jambo fulani kwa nje na
akajumuisha kwamba tatizo lako ni hili na hatua za kuchukua ni hizi.
Lakini mtu huyo anakuwa hajajua kwa undani unapitia nini hivyo ushauri
huo unakuwa siyo sahihi. Kama unataka ushauri, mtafute mtu ambaye
unamwamini, mweleze kile unachopitia bila ya kuficha chochote, kisha
yeye awe na taarifa sahihi na kukushauri kwa usahihi. Lakini siyo ule
ushauri wa juu juu ambao watu wanatoa kwa kuona mambo ya nje bila kujua
yale ya ndani.
Huwa
nasema ushauri wa bure utaona gharama yake pale unapoanza kuufanyia
kazi. Huwa siyo ushauri sahihi. Hivyo chukua ushauri kwa watu ambao ni
sahihi, watu wenye uzoefu au ujuzi na ambao wanaielewa hali yako. Na
siyo kuchukua ushauri kwa kila anayekuambia ungefanya hivi au ungefanya
vile. Kadhalika usikimbilie kutoa ushauri kwa mtu ambaye hajakuomba, kwa
sababu unakuwa hujaelewa kwa undani anapitia nini na utakachomshauri
hatofanyia kazi.
Wapo
wanaosema mbona mimi natoa ushauri kupitia makala hizi wakati
sijaombwa. Ukweli ni kwamba mimi sijakuletea maarifa haya nyumbani
kwako, au kukulazimisha usome, bali wewe umeyatafuta au kukutana nayo na
kuona yanakufaa, hivyo ukasoma. Kuna wengi wanakutana na maarifa haya,
lakini wanayapita, kwa sababu hayana maana au umuhimu kwao. Lakini wewe
umeyapokea, kwa sababu kuna kitu unatafuta na hivyo unayathamini. Hivyo
wajibu wangu ni kushirikisha maarifa sahihi ambayo mtu akiyatumia
anaweza kupiga hatua kwenye maisha yake, lakini siwezi kumlazimisha mtu
asome au kuchukua hatua.
USIANZE SIKU YAKO KWA KUFUATILIA HABARI.
Habari
nyingi ni hasi au zenye kuibua hisia kwa wafuatiliaji wake. Fungulia
chombo chochote cha habari au tembelea mtandao wowote unaotoa habari na
utaona habari gani zinapewa kipaumbele. Ni habari za kutisha au
kusisimua. Habari za mauaji, ajali, mapigano, wizi, utekaji, ukatili na
nyingine kama hizo.
Unapoianza
siku yako kwa habari za aina hii, unavuruga kabisa akili yako.
Unajikuta umepata hasira au kukata tamaa na kuona dunia haina maana.
Hata mambo ambayo ulipanga kuyafanya hutaweza kuyafanya kwa hamasa kubwa
pale ambapo umeshakutana na habari za kutisha au kukatisha tamaa.
Ndiyo
maana nakushauri usianze siku yako kwa habari, sijakuambia usifuatilie
kabisa habari (japo hilo ni jema ukiliweza), ila usianze nazo kwenye
siku yako. Anza siku yako kwa kusali/kutahajudi, kusoma vitabu,
kupangilia siku yako na kisha kuanza majukumu muhimu kwako kikazi au
kibiashara. Mwisho wa siku wakati umeshakamilisha yale muhimu, hapo sasa
unaweza kupitia habari ili ujue nini kinaendelea.
Ukifanya
hivi utajikuta unakuwa na siku tulivu, siku ambayo umeweka umakini wako
kwenye yale muhimu kwako kufanya na siyo kuvurugwa na habari za mambo
yanayoendelea, ambayo hayakuhusu moja kwa moja.
Wapo
wanaosema ni muhimu kuanza na habari kwa sababu kunaweza kuwa na kitu
muhimu unapaswa kujua kabla siku haijaanza, labda kuna daraja
limeharibika hivyo usipoanzana habari hutajua. Nasema hiyo siyo sababu
yenye mashiko ya kuruhusu siku yako ichafuliwe na habari nyingi hasi. Na
nikuambie kitu kimoja rafiki yangu, kama kuna habari muhimu kweli,
itakufikia hata kama hufuatilii habari. Tukienda na mfano huo wa daraja
kuharibika, hivi unafikiri unahitaji chombo cha habari kujua hilo? Kila
mtu atakuwa anazungumzia hilo na hivyo utajua tu.
Kadhalika
kwa habari nyingine ambazo ni muhimu, wale wanaokuzunguka watakuwa
wanazizungumzia, hivyo kama ni kitu chenye umuhimu utakijua tu.
Usikubali kuharibu siku yako kwa kuanza na habari, anza siku yako kwa mipango yako na kisha imalize kwa habari.
PUNGUZA SANA AU ACHA KABISA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KAMA HAIKUINGIZII KIPATO
Mitandao
ya kijamii imekuwa chanzo cha wengi kupoteza muda mwingi wa maisha yao.
Pia imekuwa chanzo cha wengi kupata msongo na sonona kutokana na
kufuatilia maisha ya wengine na kujilinganisha nao, kitu ambacho siyo
sahihi kwa sababu wengi huigiza kwenye mitandao hiyo.
Hivyo
ili kuepuka kupoteza MUDA na UTULIVU wako, na ili kupata AMANI ya moyo
na kuepukana na msongo na sonona, acha kabisa kutumia mitandao ya
kijamii. Jaribu hili , ile mitandao ambayo inachukua muda
wako mwingi na kila ukiingia unatoka ukiwa unawaonea wengine wivu kwa
mambo mazuri yanayoendelea kwenye maisha yao, acha kuitumia mara moja.
Ukiacha
kutumia mitandao hii utajikuta ukiwa na muda mwingi wa kufanya kazi
zako, kujifunza kupitia kusoma vitabu na hata muda wa kukaa na wale watu
wa karibu na muhimu kwako.
Tumia
mitandao hii ya kijamii kama tu inakuingizia KIPATO, kama unafanya
biashara na unatangaza kupitia mitandao hii na inakuletea wateja, basi
endelea kutumia kwa madhumuni ya biashara. Tofauti na hapo achana nayo.
Mitandao
ya kijamii inaingiza fedha kupitia wewe, wewe ndiyo bidhaa inayouzwa na
mitandao hii kwa wale wanaotangaza biashara zao. Hivyo kama na wewe
huingizi fedha kupitia mitandao hii, achana nayo, usikubali kuuzwa kwa
wengine.
Wapo
wanaosema kama siyo mitandao ya kijamii hawawezi kukutana na maarifa
mazuri kama haya. Hilo siyo kweli, maarifa mazuri yanapatikana pale
unapoyatafuta, na mitandao ya kijamii siyo sehemu nzuri kwako kujifunza.
Hivyo acha kutumia mitandao ya kijamii 2020, labda kwa lengo la kibiashara pekee.
TOFAUTI KATI YA TAJIRI NA MASIKINI KATIKA KUJIFUNZA NA KUKUA...
MATAJIRI huwa wanajifunza kila siku na kuendelea kukua zaidi. Wanajisomea vitabu na kutafuta maarifa mbalimbali yanayowawezesha kupiga hatua. Wanaamini kuna mengi hawajui hivyo kujifunza zaidi, na hilo linawafanya wafanikiwe.
MASIKINI wao hawana muda wa kujifunza, wanaamini tayari wanajua kila kitu. Hawasomi vitabu ila habari za udaku na mitandao ya kijamii ndivyo wanapenda kufuatilia. Kwa njia hii wamekuwa hawajifunzi na hivyo kubaki kwenye umasikini wao.
Saturday, December 28, 2019
Wednesday, December 25, 2019
TOFAUTI YA TAJIRI NA MASKINI KATIKA KUDHIBITI FEDHA.
MATAJIRI wana uwezo wa kudhibiti fedha zao na hivyo kuweza kupiga hatua zaidi. Hawana ulimbukeni kwenye fedha, hawabadili maisha yao kwa sababu wamepata fedha zaidi. Na pale wanapopata fedha zaidi, wanaiwekeza.
MASKINI hawawezi kudhibiti fedha zao, wana ulimbukeni mkubwa kwenye fedha. Wakipata fedha zaidi wanabadilika, wanaanza kununua vitu visivyo muhimu mpaka fedha hiyo iishe. Kwa namna hii, wanashindwa kupiga hatua na kila wanapopata fedha zaidi, ndiyo wanapotea zaidi.Acha ulimbukeni kwenye fedha, jifunze jinsi ya kudhibiti fedha zinazokuja kwako ili uweze kuzitumia kupiga hatua zaidi.
Tuesday, December 24, 2019
Sunday, December 22, 2019
Friday, December 20, 2019
KUWA MKWELI KWAKO ------- ???
Dunia
inatupa kila fursa ya kukata kona, kuchukua njia za mkato kwenye kila
ambacho tunafanya. Ni rahisi kufanya hivyo kwa sababu kila mtu anafanya
hivyo. Lakini pale unapofanya kitu kisichokuwa sahihi, ni wewe ambaye
utabeba matokeo yake na hilo litakusumbua kwa muda mrefu. Kuepuka
usumbufu unaotokana na yale uliyofanya, ni muhimu kuwa mkweli kwako
binafsi.
Thursday, December 19, 2019
TOFAUTI KATI YA TAJIRI NA MASKINI KATIKA KIPIMO CHA MALIPO
MATAJIRI huwa wanachagua kulipwa kwa matokeo ambayo wanazalisha na hilo linawapelekea kulipwa zaidi kadiri wanavyozalisha zaidi.
MASKINI huwa wanachagua kulipwa kwa muda wanaofanya kazi, na hilo linawapa ukomo kwenye kulipwa kwao kwa sababu muda una ukomo.
Acha sasa kutaka kulipwa kwa muda na anza kuchagua kulipwa kwa matokeo unayozalisha. Muda una ukomo, lakini matokeo hayana ukomo.
Ajira ni moja ya maeneo ambao unalipwa kwa muda, ndiyo maana unapaswa kuwa na biashara ya pembeni.
MASKINI huwa wanachagua kulipwa kwa muda wanaofanya kazi, na hilo linawapa ukomo kwenye kulipwa kwao kwa sababu muda una ukomo.
Acha sasa kutaka kulipwa kwa muda na anza kuchagua kulipwa kwa matokeo unayozalisha. Muda una ukomo, lakini matokeo hayana ukomo.
Ajira ni moja ya maeneo ambao unalipwa kwa muda, ndiyo maana unapaswa kuwa na biashara ya pembeni.
WENGI TUNAISHI KIMAZOEA---------- ?????
Moja ya vitu vinavyowazuia watu wengi kupiga hatua kwenye maisha ni
kukosa kipimo sahihi cha kujipima na kujifanyia tathmini kwenye maisha
yao. Wengi wanaishi kwa mazoea, leo wakifanya kile walichofanya jana, na
kesho kwenda kufanya kile walichofanya leo. Halafu wanaweza kulalamika
kwa nini wanajituma sana lakini hawafanikiwi
Wednesday, December 18, 2019
Saturday, December 14, 2019
Thursday, December 12, 2019
Monday, December 9, 2019
Sunday, December 8, 2019
Wednesday, December 4, 2019
Monday, December 2, 2019
Sunday, December 1, 2019
ACHA KUKIMBIZANA NA KILA AINA YA FURSA
Kuna fursa mpya imekuja, umeshawishiwa kwamba ni nzuri na ukafanya maamuzi ya kuingia kwenye fursa hiyo. (fuga kware)
Umeamua
kuingia, wakati unaanza kufanya unakutana na ugumu fulani, kabla
hujaanza kutatua ugumu uliokutana nao, unasikia kuna fursa nyingine bora
zaidi ya hiyo ya kwanza. Hii ya sasa ni ya uhakika zaidi inalipa zaidi na haisumbui. (fuga sungura, ndiyo habari ya mjini).
Unaingia
kwenye fursa ya pili nayo unaianza, ukiwa na matumaini makubwa, lakini
pia unakutana na baadhi ya changamoto kwenye fursa hiyo, ambazo awali
hukuambiwa. Wakati
unaanza kufanyia kazi changamoto hizo, unasikia kuna fursa nyingine
kabambe, hiyo siyo ya kukosa, ni nzuri, na haikuhitaji wewe ufanye kazi
kabisa, ni kukaa kwenye mtandao tu kwa dakika chache na kuingiza fedha. Oh,
tena huhitaji kufanya, wewe unaweka tu hela na wataalamu wanakusaidia
kufanya unasubiri kupokea tu faida (fanya forex au cryptocurrency).
Kama mpaka sasa hujaelewa kinachoendelea hapo, una tatizo, na nipo hapa kutatua tatizo hilo.
Iko
hivi rafiki, kila fursa ni nzuri na ina changamoto zake, kila fursa ina
ugumu ambao lazima ukutane nao, uuvuke na ndiyo uweze kufanikiwa.
Sasa
unapokutana na ugumu kwenye fursa moja, usikimbilie kwenye fursa
nyingine, badala yake tatua ugumu huo na kuendelea na fursa hiyo mpaka
ufanikiwe.
Ninachokuambia leo ni hiki; ACHA kukimbizana na kila aina ya fursa mpya inayokuja. Hutafanikiwa
kwa kujaribu kila fikra, bali utafanikiwa kwa kuchagua fursa moja na
kuifanyia kazi kweli mpaka kufanikiwa, na hapo utakutana na magumu na
changamoto nyingi, katika kuyavuka magumu hayo ndiyo utafanikiwa.
Bilionea Richard Branson amewahi kusema fursa ni kama daladala, ukikosa moja jua kuna nyingine inakuja. Hivyo
ACHA kabisa kukimbizana na kila aina ya fursa, chagua kitu kimoja na
kifanye, weka kazi, weka muda na kuwa na subira na ung’ang’anizi mpaka
upate kile unachotaka.
Na
kwa kumalizia, ukiona unakaribishwa kwenye fursa ambayo unaahidiwa
kupata fedha bila ya kufanya kazi yoyote ile, yaani wewe unaweka tu
fedha halafu kwa namna fulani zinazaliana na unavuna faida kubwa na kwa
haraka, basi jua hili; WEWE NDIYO FURSA YENYEWE.
ACHA kukimbizana na kila aina ya fursa, chagua kitu kimoja au vichache utakavyofanya mpaka ufanikiwe.
Friday, November 29, 2019
Saturday, November 23, 2019
VITUKO VYA TAREHE ZA MSHAHARA------- ??????
Tarehe za mshahara huwa zina vituko sana. Mtu anaondoka nyumbani hakuwa na mpango wa kununua chochote, lakini anarudi na furushi ka vitu kemkem alivyonunua, ambavyo anajishawishi ni muhimu. Ila umuhimu huo unakuwa umeonekana kwa sababu mtu anakuwa na fedha.
Lakini pesa zinapoisha, mtu anarudi kwenye maisha ya unyonge, maisha ya
uombaomba, maisha ya kukopa. Je umechoshwa na hali hiyo?
Kama jibu ni ndiyo basi KARIBU UJIUNGE NASI KATIKA DARASA LA SEMINA---ONLINE ( Google Classroom ) KILA SIKU KWA ADA YA Tshs 10000 kwa mwezi , ndani ya DARASA LA SEMINA utajifunza jinsi unavyoweza kutengeneza kipato cha pembeni ya mshahara wako na ukawa na maisha mazuri wakati wote na siyo tu tarehe za mishahara.
Kwa maelekezo Zaidi Wasiliana na Mwl. Japhet Masatu kwa namba zifuatazo : WhatsApp / Call / Meseji +255 716 924136 / + 255 755 400 128 .
Tengeneza maisha yenye msimamo sasa na acha kuishi mwisho wa mwezi kwa
mwisho wa mwezi.
UJINGA NI MZIGO.
MADOGO MADOGO YA KILA SIKU HUBOMOA AU KUJENGA NDOA.
Hakuna kitu kimoja peke yake kinaweza kuifanya ndoa yako kuwa bora.
Bali mkusanyiko wa mambo madogo madogo ya kila siku ndiyo yanaweza
kujenga au kubomoa ndoa.
Hakuna mtu ambaye ameamka akajikuta na tabia ambayo anayo sasa katika ndoa yake. Tabia zote tulizonazo katika mahusiano yetu tumezitengeneza sisi wenyewe iwe ni tabia nzuri au mbaya bali sisi ndiyo wazazi wa tabia ambazo tunazo sasa.
Katika shabaha ya makala yetu ya leo tunakwenda kujifunza utii wa mgongo wa ndoa.
Uti wa mgongo wa ndoa yako ni heshima. Unapoheshimika heshimika.
Mwenzako anapowahi kurudi nyumbani hapo amekuheshimu. Heshima ni kitu cha bure wala hakihitaji mtaji.
Unapomheshimu mwenzako kwa yale mambo madogo naye anakuheshimu pia.
Leo ni vigelele kesho isiwe kelele.
Thamini kile anachofanya mwenzako, kwa kufanya hivyo unakuwa unamweshimu mwenzako.
Unapompenda mwenzako unakuwa unamweshimu. Hivyo kumpatia mwenzako upendo ni kumpa dozi ya heshima.
Ukiheshimiwa jiheshimu. Hapa unatakiwa kujiheshimu hata uvaaji wako, tembea yako ioneshe kama vile vile wewe ni mke au mume wa mtu.
Huwa tunajidharirisha sisi wenyewe kwa namna nyingi, unapokuwa mlevi kwa mfano, ukalewa mpaka kujikojolea hapo unapokuwa umemdharirisha mwenzako na kumvunjia heshima.
Unapomshirikisha mwenzako wa ndoa katika mipango yako hapo unakuwa una mweshimu na yeye atakuheshimu pia na kwa kukushirikisha mipango yake.
Unapomuaga mwenzako au kumjulisha kuwa leo utachelewa kufika nyumbani kwa kitendo Kama hiko hapo utakuwa unamweshimu mwenzako wa ndoa.
Nyumba zinaungua usiku mchana zinakuwa vizuri ni methali ya kihaya, hapo ina maana kwamba hata kama mnatofauti zenu mzimalize ndani na mkiwa nje muwe vizuri.
Hatua ya kuchukua leo; mweshimu sana mwenzako wa ndoa. Mpe dozi ya upendo na msikilizane kwa upendo na kuheshimiana kila siku.
Kwahiyo, hakuna kitu kidogo katika ndoa. Thamani yoyote unayoitoa kwa mwenzako inakuwa ni heshima na heshima inakuwa ni uti wa mgongo wa ndoa yako.
Hakuna mtu ambaye ameamka akajikuta na tabia ambayo anayo sasa katika ndoa yake. Tabia zote tulizonazo katika mahusiano yetu tumezitengeneza sisi wenyewe iwe ni tabia nzuri au mbaya bali sisi ndiyo wazazi wa tabia ambazo tunazo sasa.
Katika shabaha ya makala yetu ya leo tunakwenda kujifunza utii wa mgongo wa ndoa.
Uti wa mgongo wa ndoa yako ni heshima. Unapoheshimika heshimika.
Mwenzako anapowahi kurudi nyumbani hapo amekuheshimu. Heshima ni kitu cha bure wala hakihitaji mtaji.
Unapomheshimu mwenzako kwa yale mambo madogo naye anakuheshimu pia.
Leo ni vigelele kesho isiwe kelele.
Thamini kile anachofanya mwenzako, kwa kufanya hivyo unakuwa unamweshimu mwenzako.
Unapompenda mwenzako unakuwa unamweshimu. Hivyo kumpatia mwenzako upendo ni kumpa dozi ya heshima.
Ukiheshimiwa jiheshimu. Hapa unatakiwa kujiheshimu hata uvaaji wako, tembea yako ioneshe kama vile vile wewe ni mke au mume wa mtu.
Huwa tunajidharirisha sisi wenyewe kwa namna nyingi, unapokuwa mlevi kwa mfano, ukalewa mpaka kujikojolea hapo unapokuwa umemdharirisha mwenzako na kumvunjia heshima.
Unapomshirikisha mwenzako wa ndoa katika mipango yako hapo unakuwa una mweshimu na yeye atakuheshimu pia na kwa kukushirikisha mipango yake.
Unapomuaga mwenzako au kumjulisha kuwa leo utachelewa kufika nyumbani kwa kitendo Kama hiko hapo utakuwa unamweshimu mwenzako wa ndoa.
Nyumba zinaungua usiku mchana zinakuwa vizuri ni methali ya kihaya, hapo ina maana kwamba hata kama mnatofauti zenu mzimalize ndani na mkiwa nje muwe vizuri.
Hatua ya kuchukua leo; mweshimu sana mwenzako wa ndoa. Mpe dozi ya upendo na msikilizane kwa upendo na kuheshimiana kila siku.
Kwahiyo, hakuna kitu kidogo katika ndoa. Thamani yoyote unayoitoa kwa mwenzako inakuwa ni heshima na heshima inakuwa ni uti wa mgongo wa ndoa yako.
Friday, November 15, 2019
Saturday, November 9, 2019
Friday, November 8, 2019
Wednesday, October 30, 2019
Monday, October 28, 2019
Sunday, October 27, 2019
Saturday, October 26, 2019
TABIA 10 ZA MSHAHARA ZINAZOKUFANYA UENDELEE KUWA MASKINI
1. Mshahara haujawahi kutosha.
2. Ongezeko la mshahara huwa haliendani na ukuaji wa gharama za maisha.
3. Mshahara huwa unaleta uteja, unapozoea kupokea kila mwezi unakuwa kama mlevi.
4. Mishahara huwa haikutani.
5. Mshahara hutengeneza tabia ya ukopaji sugu ambayo inakuwa mzigo zaidi.
6. Mshahara ni rushwa unayopewa ili usiishi ndoto zako.
7. Mwajiri anakulipa kiasi kidogo kiasi kwamba hutaacha kazi.
8. Mshahara unatengeneza wategemezi wengi, unapokuwa na mshahara kila mtu anajua lini umeupata.
9. Huwezi kutajirika kwa mshahara, bali utatajirika kwa kile unachofanya na mshahara huo.
10. Watu wengine ndiyo wanaoamua kiasi gani cha mshahara ulipwe.
Thursday, October 24, 2019
Friday, October 18, 2019
UTAJIRI NI ZAO LA FIKRA , SIYO ZAO LA FEDHA
Wengi hufikiri utajiri unaanzia kwenye fedha, lakini hilo siyo sahihi.
Na ukitaka kudhibitisha hilo, angalia wale wanaopata fedha nyingi kwa wakati mmoja, mfano wanaoshinda bahati nasibu, wanaorithi mali na wanaopata mafao, ndani ya muda mfupi hujikuta wamepoteza fedha zao zote.
Utajiri ni zao la fikra, wanaotajirika wana namna ya tofauti ya kufikiri ambayo masikini hawana. Ndiyo maana kama leo fedha zote duniani zitagawanywa sawa ka kila mtu, baada ya muda mfupi zitarudi kwa wachache matajiri.
Kama ungependa kujifunza namna sahihi ya kufikiri itakayokupeleka kwenye utajiri, JIUNGE NA DARASA LA SEMINA---GOOGLE CLASSROOM ujifunze Kila Siku kwa kulipia ADA ya shs 10000 tu kwa mwezi.
Tuwasiliane kwa WhatsApp / Call / Message +255 716 924 136 / + 255 755 400 128 / + 255 688 361 539
Kocha Mwl Japhet Masatu, Dar es Salaam, Afrika Mshariki , Tanzania
Na ukitaka kudhibitisha hilo, angalia wale wanaopata fedha nyingi kwa wakati mmoja, mfano wanaoshinda bahati nasibu, wanaorithi mali na wanaopata mafao, ndani ya muda mfupi hujikuta wamepoteza fedha zao zote.
Utajiri ni zao la fikra, wanaotajirika wana namna ya tofauti ya kufikiri ambayo masikini hawana. Ndiyo maana kama leo fedha zote duniani zitagawanywa sawa ka kila mtu, baada ya muda mfupi zitarudi kwa wachache matajiri.
Kama ungependa kujifunza namna sahihi ya kufikiri itakayokupeleka kwenye utajiri, JIUNGE NA DARASA LA SEMINA---GOOGLE CLASSROOM ujifunze Kila Siku kwa kulipia ADA ya shs 10000 tu kwa mwezi.
Tuwasiliane kwa WhatsApp / Call / Message +255 716 924 136 / + 255 755 400 128 / + 255 688 361 539
Kocha Mwl Japhet Masatu, Dar es Salaam, Afrika Mshariki , Tanzania
Tuesday, October 15, 2019
Monday, October 14, 2019
Friday, October 11, 2019
Tuesday, October 8, 2019
Monday, October 7, 2019
Sunday, October 6, 2019
Thursday, October 3, 2019
Sunday, September 29, 2019
Saturday, September 28, 2019
KOSA KUBWA UNALOFANYA KWENYE MSHAHARA WAKO UNAOPOKEA KILA MWEZI
Kwa mshahara au kipato chochote unachopokea, iwe ni malipo ya kazi zako binafsi au faida unayotengeneza kwenye biashara, kuna kosa moja kubwa umekuwa unalifanya. Kosa hilo ni KUMLIPA KILA MTU NA KUJISAHAU WEWE MWENYEWE.
Hebu fikiria unapopata fedha unaanza na nini? Kulipa madeni, kulipa bili, kununua vyakula, kununua nguo, kulipia starehe na mapumziko mbalimbali. Baada ya siku chache za kupata fedha unakuwa umeimaliza yote, huku wewe ukibaki mtupu kabisa.Sasa rafiki, jua kwamba huwezi kuwa huru kifedha kama utaendekeza utaratibu huo wa kuwalipa wengine na kujisahau wewe mwenyewe. Kwenye kila kipato unachoingiza, mtu wa kwanza kumlipa unapaswa kuwa wewe.
Monday, September 23, 2019
MSHAHARA NI MADAWA YA KULEVYA , JIFUNZE JINSI YA KUEPUKANA NA MADHARA YAKE
Nassim Taleb anatuambia kuna vitu vitatu vyenye uraibu mbaya, madawa ya
kulevya(unga), vyakula vya wanga (sukari) na mshahara wa kila mwezi.
Ukishauzoea mshahara, ni vigumu sana kuweza kufanya kitu kikubwa kwenye maisha yako. Kwa sababu maisha yako yanakuwa ya mipango ya mwisho wa mwezi tu. Kwamba mwisho wa mwezi huu nitafanya hiki au kile.
Mshahara ukitoka unakuwa na mipangilio mingi kuliko kiwango chake, hivyo ndani ya siku mbili unakuwa umeisha. Na hapo unafanya nini? Unajua vyema, unaanza kukopa kwa sababu unajua mshahara ujao utalipa. Na hapo ndipo uraibu unapojenga mizizi.
Kuondokana na uraibu huu wa mshahara, lazima uanze kujijengea msingi wa kipato nje ya mshahara.
TEMBELEA BLOGS ZA MWL. JAPHET MASATU , JIFUNZE , JIUNGE NA DARASA LA MAFUNZO KILA SIKU NA UCHUKUE HATUA , MAISHA NA WEWE !
Tuwasiliane kwa Call / Message / ( WhatsApp + 255716924136 )/ + 255 755 400128 / +255 688 361 539
Saturday, September 21, 2019
Thursday, September 19, 2019
Monday, September 16, 2019
Sunday, September 15, 2019
Saturday, September 14, 2019
Friday, September 13, 2019
MIPANGO YA MAISHA INAPASWA KUJA KABLA YA MIPANGO YA BIASHARA.
Ni
rahisi sana kuweka malengo na mipango mikubwa ya kibiashara, lakini
unapokaa na kujiuliza kwa nini unataka kufikia malengo hayo makubwa
unakosa jibu la uhakika.
Watu
wengi wamekuwa wanapotea kwenye biashara kwa sababu wanaweka malengo ya
biashara kabla hawajaweka malengo ya maisha. Wanataka kuwa mabilionea
kupitia biashara zao, na hilo linawataka kuweka maisha yao yote kwenye
biashara na kusahau vitu vingine vyote. Wanaweza kufikia lengo hilo,
lakini maeneo mengine ya maisha yao kama afya na mahusiano yanakuwa
yameathirika sana.
Kabla
hujaweka lengo kubwa la biashara, anza kwanza na lengo kuu la maisha
yako. Jua unataka kuwa na maisha ya aina gani, jua maisha ya mafanikio
kwa upande wako yana maana gani.
Ukishajua
kwamba unataka nini kwenye maisha yako, hapo sasa unaweza kuitumia
biashara yako kuwa na maisha unayoyataka wewe. Lakini ukianza kufikiria
unachotaka kwenye biashara pekee, utaishia kuwa na maisha mabovu sana.
Tuesday, September 10, 2019
Saturday, September 7, 2019
Friday, September 6, 2019
Wednesday, September 4, 2019
Tuesday, September 3, 2019
Monday, September 2, 2019
UNAPOJIAJRI , UNAPASWA KUFIKIRI TOFAUTI NA WALE WALIOAJIRIWA.
Unapojiajiri, unapaswa kufikiri tofauti
kabisa na wale walioajiriwa. Kwa sababu kuna vitu ambavyo watu
walioajiriwa hawajisumbui navyo sana, kwa sababu wameahidiwa vinafanyiwa
kazi, mfano bima ya afya, mafao ya uzeeni na mengineyo. Unapoachana na
ajira na kuamua kujiajiri moja kwa moja, mambo hayo utapaswa
kuyahangaikia mwenyewe, lazima utafute bima yako na familia yako na pia
lazima uwekeze ili kujiandaa kwa siku zijazo. Kwa sababu hakuna
anayekuandalia mafao, unapaswa kutengeneza uwekezaji wako mwenyewe,
ambao miaka mingi ijayo utaweza kukuingizia wewe kipato hata kama
hufanyi kazi moja kwa moja.
Saturday, August 31, 2019
BECOMING ENTERPRENUER : KWA NINI KUJIFUNZA NI KITU MUHIMU KWA MJASIRIAMALI ??
Kujifunza zaidi au kila siku ni kitu muhimu kwa mjasiriamali, sababu ujasirimali ni TAALUMA.
Ujasirimali hauishii tu ktk;
---kuanzisha Biashara
----kujiajiri mwenyewe
-----kuwa na uthubutu
-----kuwa na malengo
-------kuwa na wazo zuri la Biashara nk
--------Unahitaji kujifunza na kuwa na ujuzi ili uweze kuendesha na kusimamia miradi au Biashara zako ili ufanikiwe. Pia kuwa na skills utakazo tumia kukabiliana na changamoto zozote zitakazo jitokeza, kutafuta masoko ya bidhaa zako, jinsi ya kuwekeza, kutengeneza mpango Biashara, kusimamia wafanyakazi wako nk.
.
Huwezi kuwa mjasiriamali kama huja jifunza ujasiriamali, Kama ilivyo taaluma nyingine huwezi kuwa mjasiriamli kama huja jifunza au kupata mafunzo ya ujasiriamali.
Ujasirimali hauishii tu ktk;
---kuanzisha Biashara
----kujiajiri mwenyewe
-----kuwa na uthubutu
-----kuwa na malengo
-------kuwa na wazo zuri la Biashara nk
--------Unahitaji kujifunza na kuwa na ujuzi ili uweze kuendesha na kusimamia miradi au Biashara zako ili ufanikiwe. Pia kuwa na skills utakazo tumia kukabiliana na changamoto zozote zitakazo jitokeza, kutafuta masoko ya bidhaa zako, jinsi ya kuwekeza, kutengeneza mpango Biashara, kusimamia wafanyakazi wako nk.
.
Huwezi kuwa mjasiriamali kama huja jifunza ujasiriamali, Kama ilivyo taaluma nyingine huwezi kuwa mjasiriamli kama huja jifunza au kupata mafunzo ya ujasiriamali.
Friday, August 30, 2019
Saturday, August 24, 2019
Sunday, August 18, 2019
HAKUNA ANAYEKOSEA KWA MAKUSUDI.
Upo
msingi wa ustoa ambao utakuwezesha kuishi maisha yako kwa utulivu bila
ya kujali wengine wanasema au kufanya nini. Moja ya vitu ambavyo
vinatusumbua sana zama hizi ni mambo ambayo wengine wanasema au
wanafanya. Huwa tunayaruhusu yatuumize, tukiamini kwamba watu hao
wanafanya mambo hayo kwa makusudi ili kutuumiza.
Lakini
wastoa wanatuambia kwamba, watu wanaofanya mambo ambayo yanatuumiza,
hawafanyi hivyo kwa makusudi, bali wanafanya hivyo kwa sababu hawajui
kulicho sahihi kufanya. Hivyo hupaswi kuumia kwa sababu yao, badala yake
unapaswa kuwaonea huruma na kuona kama kuna namna unaweza kumsaidia ili
asiendelee kukosea.
Mfano
mzuri ni pale mtoto mdogo anapokupiga kofi, je utarejesha kwa kumpiga
kofi pia? Je utakasirika? Je utamnunia? Je utasema amekudharau? Majibu
hapo ni hapana. Lakini vipi mtu mzima mwenzako akikupiga kofi? Hapo
mambo yanabadilika, unaona amekudharau, utataka kulipiza, utakasirika na
hata kumnunia. Lakini kama utachukulia mtu huyo amekupiga kofi kwa
kutokujua au kwa bahati mbaya, hutapata hisia hizo.
Hivyo
cha kujifunza hapa, tusikimbilie kuhukumu pale watu wanapofanya vitu
kwamba ni vibaya au wamedhamiria kutuumiza. Badala yake tuchukulie
kwamba watu hao hawajui wanachofanya au wamefanya kwa bahati mbaya, na
hilo litatuzuia sisi kuumia.
Mfano
mzuri ni kwenye wizi au utapeli, mtu akikuibia, badala ya kuumia,
unapaswa kumwonea huruma, kwa sababu kwanza hajui njia sahihi ya
kutengeneza kipato ambayo itampa maisha ya utulivu na pili, kwa tabia
yake hiyo, ataishia jela au kaburini, maana ataiba akamatwe na wananchi
wenye hasira kali hadi kufa, au apelekwe polisi na baadaye kufungwa.
Unaona jinsi ambavyo unaondoka kwenye upande wa lawama na kuwa upande wa
utulivu!
CHAGUA SHUJAA WA MAISHA YAKO.
Wastoa
wamekuwa wanaelewa umuhimu wa kuwa na mashujaa, watu ambao tunayapima
maisha yetu kupitia wao. Lakini hili ni eneo ambalo limekuwa na
changamoto kubwa sana zama hizi, kwa sababu kumekuwa na mashujaa wengi
feki. Siku hizi watu wanaoweza kutengeneza umaarufu rahisi kupitia
mitandao ya kijamii, sanaa, michezo au siasa ndiyo wanaonekana mashujaa
kwa wengi. Na wengi wanawafuata watu hao, lakini hakuna wanachojifunza
kwa sababu mwisho wa siku umaarufu wa watu hao huanguka, kwa sababu
haujajengwa kwenye misingi sahihi.
Ni
muhimu uchague mashujaa sahihi wa maisha yako, kutokana na misingi
wanayoiishi au waliyoiishi ambayo unaweza kujijengea kwenye maisha yako
na ukaweza kupiga hatua pia. Kadiri unavyojifunza falsafa hii na
kujifunza wengine walioiishi falsafa hii, utavutiwa na maisha ya baadhi
ya wanafalsafa na kuwachagua kuwa mashujaa wako.
JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO MAKUBWA YA MAISHA KIAFYA.
Kuna
wakati tunakutana na mabadiliko makubwa kimaisha kwenye afya zetu.
mabadiliko haya yanaweza kutuyumbisha sana kama hatuna msingi sahihi
tunaouishi. Mfano ni pale mtu anapopata ulemavu wa mwili ambao unaathiri
maisha na hata kazi za mtu. Wengi huvurugwa sana na mabadiliko ya aina
hii, kitu ambacho hupelekea maisha yao kudorora na hata kufa mapema.
Wastoa
wanatupa njia sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya aina hii, kwa
kutuambia tunapaswa kufikiria na kutumia kile tulichonacho na siyo
kuangalia tumekosa nini. Kama umepata ulemavu wa miguu, kumbuka bado una
mikono, macho, masikio, na viungo vingine, ambavyo kama utaweza
kuvitumia vizuri maisha yako yatakuwa bora.
Mmoja
wa wanafalsafa wa Ustoa, Epictetus, ambaye alikuwa mwalimu bora sana wa
falsafa hii, alikuwa mtumwa. Katika maisha yake ya utumwa, aliumizwa na
kupata ulemavu wa miguu. Hili lilimpa ulemavu wa maisha, lakini
hakuruhusu ulemavu huo uathiri maisha yake, aliangalia mambo gani
mengine anayoweza kufanya, kama kujifunza na kufundisha falsafa na siyo
kuangalia alichokosa.
Somo
muhimu la kuondoka nalo hapa ni usiweke nguvu zako kwenye yale
uliyokosa au kupoteza, badala yake weka nguvu zako kwenye yale uliyonayo
na jinsi unavyoweza kuyatumia kwa ubora zaidi.
FALSAFA YA USTOA NA UTAJIRI.
Kwenye Falsafa ya Ustoa, vitu vimegawanyika katika makundi matatu;
Kundi la kwanza ni vitu vizuri kufanya au kuwa navyo (virtues), ambavyo ni vinne; hekima, ujasiri, haki na kiasi.
Kundi
la pili ni vitu vibaya kufanya au kuwa navyo (vices), ambavyo ni
kinyume na hivyo vizuri, yaani, upumbavu, woga, udhalimu na tamaa.
Kundi
la tatu ni vitu ambavyo siyo vizuri na wala siyo vibaya (indifferent),
ambavyo hakuna ubaya kuwa navyo, lakini pia hupaswi kujitesa ili kuwa
navyo. Hapa vitu vingine vyote kwenye maisha vinaingia hapo, kuanzia
afya, kazi, biashara, fedha na kadhalika.
Sasa
kwa misingi ya ustoa, wengi hufikiri inawataka wawe masikini, watu
wasiojali fedha wala utajiri. Lakini katika historia, moja ya
wanafalsafa waliokuwa na maisha mazuri basi ni wastoa. Seneca alikuwa
tajiri mkubwa enzi zake na mwanasiasa, Marcus Aurelius alikuwa mtawala
wa Roma. Kwa kifupi wastoa walijihusisha na maisha ya kila siku na ya
kawaida, wakifanya yale ambayo kila mtu anafanya.
Na
hii ni sababu nyingine nzuri kwa nini tunapaswa kuwa wastoa, kwa sababu
ni falsafa ambayo haipingi mtu kuwa na fedha, au kujihusisha na mambo
mengine, kama tu hayavunji msingi wa wema.
Zipo
baadhi ya dini na falsafa ambazo zinawafundisha wafuasi wake kuachana
kabisa na mambo ya dunia, kutoa maisha yao kwa ajili ya falsafa au Mungu
pekee. Lakini wote tunajua maisha yana mahitaji yake, hutaenda kulipa
ada za watoto kwa falsafa, na wala hutaenda dukani kupata chakula kwa
kusema wewe ni mwanafalsafa.
Hivyo
kwa kuishi kwa falsafa ya ustoa, unakuwa huru kufanya upendacho, ila tu
kiwe sahihi kwako na kwa wengine, na pia unakuwa huru kujikusanyia
fedha utakavyo, ila tu ufanye hivyo kwa usahihi na kwa manufaa ya
wengine pia.
Na
kikubwa nilichojifunza ni kwamba ukiishi misingi ya falsafa ya ustoa,
una nafasi kubwa ya kuwa tajiri, lakini pia utakuwa huru na utajiri huo.
Kwa sababu kwanza utakuwa unafanya kilicho sahihi na kuachana na yasiyo
sahihi, pia utaepuka kufanya mambo ambayo yatakupotezea fedha, kwa
kudhibiti vizuri hisia zako. Lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba
hutafungwa na utajiri wako, hata kama utapoteza kila kitu, bado utabaki
imara na maisha yako yataendelea.
Naweza
kuhitimisha kwa kusema, Ustoa ni falsafa ya watu wakuu na matajiri,
najua unapenda kuwa mkuu, unapenda kuwa tajiri na kuwa huru na maisha
yako, hivyo basi, ijue na kuiishi misingi ya ustoa.
KUHUSU KIFO NA KUJIUA.
Moja
ya vitu ambavyo vimekuwa vinawasumbua watu wengi n kifo. Wote tunajua
kuna siku tutakufa, lakini hatutaki kufikiria wala kupata picha ya kifo
chetu. Kadhalika tunajua wale watu wa karibu kwetu, ambao tunawapenda
sana kuna siku watakufa. Lakini huwa hatufikirii wala kupata picha ya
vifo vyao. Kinachotokea ni tunakutana na vifo ghafla na vinatuumiza
sana.
Wastoa wana maeneo matatu ya kuzingatia kuhusu kifo.
Kwanza
ni kifo chako mwenyewe, ambapo wastoa wanasema hakuna sababu ya
kukiogopa kifo, kwa sababu ni sehemu ya maisha yako na kinaweza kutokea
muda wowote. Hivyo wakati wowote unapaswa kuwa tayari kukikabili kifo.
Inapofanya jambo lolote, lifanye kama ndiyo mara ya mwisho kwako
kulifanya, kama vile kifo kinakusubiri. Kwa njia hii hutaahirisha jambo
lolote muhimu na utafanya mambo kwa usahihi. Wastoa wanasema kama
unaogopa kifo, maana yake bado hujaanza kuishi. Lakini kama utachagua
kuishi maisha yako, kifo hakitakusumbua, kwa sababu wakati wowote
utakuwa tayari.
Mbili
ni vifo vya watu wa karibu kwetu. Wazazi wetu, watoto wengu, wenzi wetu
na ndugu wengine ni watu tunaowapenda na kuwajali sana. Inapotokea
wamefariki dunia, huwa tunaumia, tunalia na kuhuzunika sana. Kwa wengine
vifo vya watu wao wa karibu huwa vinawavuruga sana, vinaishia kuwapa
magonjwa ya akili. Wastoa wanatuambia vifo vya watu wa karibu kwetu
vinatuumiza kwa sababu vinatukuta hatujajiandaa. Wanatuambia kila
unapoongea au kukutana na mtu wako wa karibu, jiambie kimoyomoyo kwamba
hiyo ni mara ya mwisho kukutana naye. Epictetus anatuambia kila
unapombusu mtoto wako, jiambie unambusu mtu ambaye anaweza kufa muda
wowote. Kwa kuchukulia hivi, utajali sana, kwa sababu unajua mtu anaweza
kupotea muda wowote, na hilo linapotokea utaumia, lakini
halitakuvuruga, kwa sababu ni kitu ambacho ulijua kitatokea, a pia
ulishatumia fursa ulizokuwa nazo kabla mtu huyo hajafariki.
Tatu
ni kujiua. Wastoa wa zamani, wengi waliishia kujiua wenyewe au kupewa
adhabu ya kifo. Hii ilitokana na tawala za kidhalimu zilizokuwepo enzi
hizo na wastoa hawakuogopa kuzisema na kuzipinga. Hilo liliwafanya
wawekwe vizuizini, kufukuzwa au kuhukumiwa kufa. Wastoa walikuwa
wakipokea adhabu hizo bila ya kuruhusu ziharibu utulivu wao wa ndani.
Mfano mstoa alipohukumiwa kifo, alikipokea kama sehemu ya maisha na
kusimamia misingi yake. Lakini pia wapo wastoa ambao walipofika mwisho
wa maisha yao, yaani uzee na kuona wameshakamilisha jukumu lao la
maisha, basi walijiua. Hii ni dhana ambayo ilikuja kupotea, lakini zama
hizi imeanza kurudi. Wapo watu ambao wanachagua kuyakatisha maisha yao
kwa sababu mbalimbali. Hapa hatuzungumzii wale wanaojiua kukimbia
majukumu au matatizo waliyosababisha, bali wale ambao wanaona imetosha
sasa na wanataka kupumzika. Hilo pia ni zoezi la kistoa.
MATAWI MATATU YA FALSAFA YA USTOA.
Falsafa
ya ustoa inafananishwa na mti ambao una vitu vitatu ili uweze kuwa mti.
Mti una mizizi ambayo inaupa uimara na virutubisho, shina ambalo
linahifadhi chakula na kutoa umbo na matawi ambayo yanatengeneza chakula
na kuvuta hewa.
Falsafa ya ustoa ina matawi matatu;
Moja
ni fizikia (physics), hili ni tawi linalojihusisha na sayansi ya asili,
jinsi dunia ilivyo na inavyojiendesha. Hii ndiyo mizizi ya falsafa hii.
Mbili
ni maadili (ethics), hili ni tawi ambalo linaipa falsafa hii msimamo,
jinsi ya kuishi na kujihusisha na wengine. Hili ndiyo shina la falsafa
hii.
Tatu
ni mantiki (logic), hili ni tawi ambalo linahusika na kufikiri pamoja
na kufanya maamuzi sahihi. Haya ndiyo matawi ya falsafa hii.
Ili
maisha yetu yakamilike, lazima tuwe vizuri kwenye maeneo hayo matatu,
kuijua dunia na hapa tunapaswa kuwa na ujasiri na kiasi, kuwa na maadili
tunayoyaishi ambapo tunapaswa kuwa watu wa haki na mwisho kutumia akili
zetu kufikiri, ambapo tutaweza kuwa na hekima.
Ukiona
hapo, matawi matatu ya ustoa ambayo ni FIZIKIA, MAADILI NA MANTIKI,
ndiyo yanazalisha misingi mikuu minne ya ustoa ambayo ni HEKIMA,
UJASIRI, HAKI NA KIASI. Kwa kifupi, falsafa nzima ya Ustoa imejumuishwa
kwenye sentensi hiyo.
FALSAFA YA USTOA
Falsafa
ya Ustoa ilianza miaka 300 kabla ya Kristo ambapo Zeno, mwanzilishi wa
falsafa ambaye kwa wakati huo alikuwa mfanya biashara alikuwa safarini
na chombo chake kikaharibika akiwa Athens Ugiriki. Akiwa hapo Athens,
alitembelea maktaba na kuperuzi maandiko yaliyokuwepo, alikutana na
mafunzo ya Socrates na yakamvutia sana. Akamuuliza mhusika wa maktaba
ile, ni wapi anaweza kuwapata watu ambapo atajifunza zaidi kuhusu
falsafa, na hapo akaoneshwa mwanafalsafa Crates na akamfuata, hapo ndipo
safari yake ya kujifunza na kuwa mwanafalsafa ilipoanzia.
Zeno
alijifunza kupitia Crates ambaye alikuwa kwenye shule ya falsafa
inayoitwa Cynics, ambao ni watu ambao hawakujali kuhusu chochote,
waliishi maisha kwa wakati waliokuwa nao na walihoji na kutilia mashaka
kila kitu.
Baada
ya kujifunza kwenye falsafa hii kwa muda, Zeno aliona falsafa ya Cynics
ilikuwa na mapungufu, kwa sababu huwezi kupuuza kila kitu kuhusu maisha
na ukawa na maisha bora. Hivyo alianzisha shule yake ya falsafa, ambapo
alikuwa akifundisha chini ya mti ulioitwa stoa. Na hapo ndipo jina la
Ustoa (Stoicism) lilipoanzia.
Tangu
kipindi cha Zeno, pamekuwepo wanafalsafa ambao wameiendeleza na kuikuza
zaidi falsafa hii ya zeno. Wanafalsafa kama Cato, Musonius Rufus,
Seneca, Epictetus na Marcus Aurelius kwa nyakati tofauti waliishi na
kufundisha falsafa hii.
Subscribe to:
Posts (Atom)