Mitandao
ya kijamii imekuwa chanzo cha wengi kupoteza muda mwingi wa maisha yao.
Pia imekuwa chanzo cha wengi kupata msongo na sonona kutokana na
kufuatilia maisha ya wengine na kujilinganisha nao, kitu ambacho siyo
sahihi kwa sababu wengi huigiza kwenye mitandao hiyo.
Hivyo
ili kuepuka kupoteza MUDA na UTULIVU wako, na ili kupata AMANI ya moyo
na kuepukana na msongo na sonona, acha kabisa kutumia mitandao ya
kijamii. Jaribu hili , ile mitandao ambayo inachukua muda
wako mwingi na kila ukiingia unatoka ukiwa unawaonea wengine wivu kwa
mambo mazuri yanayoendelea kwenye maisha yao, acha kuitumia mara moja.
Ukiacha
kutumia mitandao hii utajikuta ukiwa na muda mwingi wa kufanya kazi
zako, kujifunza kupitia kusoma vitabu na hata muda wa kukaa na wale watu
wa karibu na muhimu kwako.
Tumia
mitandao hii ya kijamii kama tu inakuingizia KIPATO, kama unafanya
biashara na unatangaza kupitia mitandao hii na inakuletea wateja, basi
endelea kutumia kwa madhumuni ya biashara. Tofauti na hapo achana nayo.
Mitandao
ya kijamii inaingiza fedha kupitia wewe, wewe ndiyo bidhaa inayouzwa na
mitandao hii kwa wale wanaotangaza biashara zao. Hivyo kama na wewe
huingizi fedha kupitia mitandao hii, achana nayo, usikubali kuuzwa kwa
wengine.
Wapo
wanaosema kama siyo mitandao ya kijamii hawawezi kukutana na maarifa
mazuri kama haya. Hilo siyo kweli, maarifa mazuri yanapatikana pale
unapoyatafuta, na mitandao ya kijamii siyo sehemu nzuri kwako kujifunza.
Hivyo acha kutumia mitandao ya kijamii 2020, labda kwa lengo la kibiashara pekee.
No comments:
Post a Comment