Wanamajlis,
Mara nyingi nimekuwa kila nikieleza historia ya TANU na harakati za kudai uhuru nimekuwa nikimtaja Abdulwahid Sykes na Kariakoo Market ambako alikuwa akifanya kazi kama Market Master.
Soko
lenyewe ndilo hilo hapo juu kama lilivyokuwa katika miaka 1950 hadi
miaka ya 1970 lilipovunjwa na kujengwa soko hili tulionalo sasa.
Bahati mbaya huwezi kuona ofisi ya Abdul Sykes lakini mkono wa kulia wa picha hiyo ni Mtaa wa Swahili ukikatizwa na Mtaa wa Tandamti (Mtaa wa Mshume Kiyate).
Bahati mbaya huwezi kuona ofisi ya Abdul Sykes lakini mkono wa kulia wa picha hiyo ni Mtaa wa Swahili ukikatizwa na Mtaa wa Tandamti (Mtaa wa Mshume Kiyate).
Kushoto ni Mtaa wa Nyamwezi.
Ofisi ya Abdul Sykes ilikuwa katikakati ya Mtaa wa Swahili na Tandamti na Swahili na Mkunguni.
Hapo ndipo Mwalimu Nyerere alipopelekwa na Abdul na akawa Nyerere akija pale ofisini kwa Abdul kila alipokuja mjini kutoka Pugu.
Hapo sokoni ndipo Mwalimu Nyerere alipojuana na Shariff Abdallah Attas mmoja wa watu maarufu wa Dar es Salaam enzi zile na mtu aliyekuwa anajua mengi katika historia ya TANU.
Abdul aliuza
kadi za kwanza za TANU ndani ya ofisi ile kiasi kwamba iko siku
alizozana na Town Clerk Mzungu aliyetaka kujua kwa nini kadi za TANU
zinauzwa pale.
Katika
miaka ile ya 1950 mwanzoni hapo palikuwa moja ya vituo vya harakati na
kituo kingine kilikuwa Ilala Welfare Centre ofisini kwa Hamza Mwapachu.
Baada ya kazi walikuwa wakikutana Tanga Club New Street na Mkunguni kujiburudisha na kuzungumza siasa.
CHANZO CHA TAARIFA : MOHAMED SAID WEBSITE.
No comments:
Post a Comment