Wewe Sio Mtabiri Mzuri, Hivyo Acha Kujiogopesha.
Mara baada ya sultani wa dubai kuamua kusafiri baharini na baadhi ya wapambe wake.
Siku iliyofuata walijumuika kwa pamoja kwa ajili ya kuanza safari.
Hata
hivyo , wakati meli ilipoondoka kutoka nchi kavu, mmoja wa wapambe
wake, ambaye hakuwahi kuona bahari hapo kabla alianza kupata hofu ya
kukaa ndani ya meli , alilia na kupiga kelele.
Sultani alijaribu kumtuliza lakini hakumsikiliza.
Watu wengi kwenye meli walijaribu kumtuliza lakini hawakufanikiwa.
Safari ya kila mtu ambayo ilipaswa kuwa ya kufurahia na utulivu , iligeuka kuwa moja ya mateso.
Sultan hakujua cha kufanya.
Siku mbili zilipita kama hivo.
Mpambe huyo alikataa kula hata kulala.
Kila mtu kwenye meli alichukizwa na tabia yake.
Sultan alifikiria inaweza kuwa bora zaidi kurudi bandarini.
Hapo ndipo mtu mmoja alipomjia na kusema, mkuu kwa idhini yako, nitaweza kumtuliza.
Ikiwa tu utaniruhusu kutumia njia zangu bila kuhoji.
Bila kusita, sultan alisema, “ dhahiri “. Una ruhusa yangu.
Si hivyo tu kama utafanikiwa nitakulipa kwa ajili ya kutatua tatizo hili.
Mtu mwenye hekima alitoka nje na kumwambia mmoja wa wafanyakazi “ Mtupie ndani ya bahari, mara moja”.
Mfanyakazi alisita kwanza lakini mtu huyo alikuwa na ruhusa ya sultani, kwa hivyo alimshika mtu huyo na kumtupa baharini.
Mpambe aliripuka na kuzama , akameza maji mengi ya bahari.
Kisha akarudi juu na akapiga kelele zaidi kuliko hapo awali na akazama tena.
Hii ilitokea mara 2-3 na kisha waziri akaamuru arudishwe tena ndani ya meli.
Mpambe alirudishwa ndani ya meli, mara hii hakulalamika wala kulia na safari ikawa na amani.
Kila mmoja alifurahia safari na wote walikuwa na amani.
Baada ya kumaliza safari, meli ilirudi bandarini.
Aliporudi,
kabla ya kuondoka kwenye meli , sultan akaenda kumwona, Yule
mwanahekima na kumuuliza, ulijuaje kwamba kwa kumtupa mtu huyo baharini,
atatulia?
Yule
mwanahekima alimjibu , “kwa sababu ya uzoefu wangu wa kwenye ndoa”,
baada ya ndoa yangu, siku zote nilikuwa na hofu ya kumpoteza mke wangu
na siku zote nilikuwa nikimlalamikia na kama vile mtu huyo alivyofanya
kwenye meli.
Siku moja mke wangu hakuweza kunivumilia tena aliniacha.
Kuishi bila yeye ilikuwa uzoefu wa kutisha kutoka kwangu.
Alirudi pale nilipomuahidi kwamba sitamlalamikia tena.
Kwa njia hiyo hiyo, mtu huyo alikuwa hajawahi kupima maji ya chumvi na hakuwahi kujua uchungu wa kuzama.
Lakini alipotupwa baharini na kurudishwa kwenye meli, hapo ndipo alipoelewa.
Umekuwa unatabiri mambo mengi sana kuhusu maisha yako, lakini je ni mambo mangapi uliyotabiri yametokea?
Ni mambo mangapi ambayo ulikuwa unayahofia, yanakunyima usingizi yametokea kweli?
Nafikiri ni machache sana, kama hata yapo.
Ukweli ni kwamba wewe sio mtabiri mzuri, na wala hutakuwa mtabiri mzuri kadiri siku zinavyokwenda.
Umekuwa
ukijitabiria kwamba maisha yatakuwa magumu zaidi, kwamba utapata hasara
kwenye biashara, kwamba utafukuzwa kazi, kwamba mambo hayataenda
vizuri!!
Lakini haya yote huwa yanatokea?
Hayatokei na hata kama yakitokea sio kwa sababu umetabiri ila kwa sababu umeamua kukubaliana na kile unachotabiri.
Unatabiri
kwamba utapata hasara kwenye biashara halafu unaendelea kuendesha
biashara yako kwa mazoea, unaishia kupata kweli hasara.
Ninachotaka kukuambia leo ni kwamba chochote unachotabiri leo hakina maana, chochote unachohofia leo ni kupoteza muda wako.
Hata ungetabiri kiasi gani na kujijaza hofu kiasi gani hakuna mmoja wetu anayejua nini kitatokea kesho.
Na
hii ni vizuri sana kwa sababu lengo lako kubwa ni kuishi vizuri leo,
kufanya kile ulichopanga kukifanya leo, kwa ubora wa hali ya juu sana
kama vile ndio unakifanya kwa mara ya mwisho na hutakuwa na haja ya
kuhofu kuhusu kesho tena.
Kwa
sababu ukiishi vizuri leo, unaandaa mazingira mazuri ya kuishi vizuri
kesho. Ukifanya kazi yako kwa ubora leo unaandaa mazingira mazuri ya
kufanya kazi yako vizuri kesho.
Ukimhudumia
mteja wako vizuri leo, kwa huduma nzuri ambayo hajawahi kuipata sehemu
nyingine yeyote, unafikiri kesho ataenda wapi?
Unaona mambo yalivyo mazuri sasa?
Huna
haja ya kutabiri, huna haja ya kuhofia, weka nguvu zako kwenye kufanya
kilicho bora leo, sasa hivi wakati bado una nafasi hiyo ya kufanya
hivyo.
NA KOCHA MWL JAPHET MASATU, DAR ES SALAAM
JIUNGE SASA NA DARASA ONLINE UJIFUNZE KWA VITENDO
TUWASILIANE KWA WhatsApp + 255 716 924 136