Fedha
ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu, ukiondoa pumzi ambayo kila mtu
anaipata bure, kila kitu kinahitaji fedha. Na hata hiyo pumzi unapoumwa
inaacha kuwa bura na unaanza kuilipia. Fedha ni hitaji muhimu sana
kwenye maisha yetu, kwa sababu ndiyo inatuwezesha kupata kila
tunachotaka.
KIPATO;
ongeza kipato chako kwa kutoa thamani zaidi, kujituma zaidi na
kuwafikia wengi zaidi. Kama umeajiriwa tekeleza majukumu mengi zaidi na
magumu zaidi. Kama unafanya biashara wafikie wateja wapya na wengi
zaidi. Fanya zaidi ya ulivyozoea kufanya huko nyuma na kipato chako
kitaongezeka.
MATUMIZI;
Dhibiti sana matumizi yako, peleka fedha zako kwenye yale mambo ambayo
ni muhimu pekee kwenye maisha yako, kama kitu siyo muhimu, achana nacho.
Matumizi huwa yana tabia ya kukua kadiri kipato kinavyokua,
usipoyadhibiti yatakurudisha nyuma.
UWEKEZAJI;
Hutakuwa na nguvu za kufanya kazi kama unavyofanya sasa miaka yako
yote. Hivyo unahitaji kuifanya fedha yako ikufanyie kazi na kukiingizia
kipato. Na hapa ndipo uwekezaji unapokuwa muhimu. Weka akiba na wekeza
akiba hiyo kwenye maeneo ambayo yanazalisha zaidi kwa baadaye.
No comments:
Post a Comment