Hatua muhimu ya kupata kile unachotaka ni kujua kwa hakika nini hasa unachotaka. Huwezi
kupata kile usichokijua, hivyo lazima ujue kwa undani kile unachotaka
na kukifikiria kwa ukamilifu wake ndiyo uweze kukipata.
Unapaswa
kutengeneza picha kwenye fikra yako ya kile unachotaka, kwa namna
unavyokitaka kisha weka picha hii kwenye fikra zako mara nyingi. Kila unapokuwa na muda ambao huna kazi, tumia muda huo kufikiria picha hiyo na kujiona tayari umeshapata kile unachotaka.
Unapoifikiria picha ya kile unachotaka, unapaswa kuwa na imani kwamba tayari umeshakipata kwa namna unavyokitaka. Ona kama tayari unacho. Kwa njia hii, mfumo wa fikra unaoongoza dunia utakuwezesha kupata kile unachotaka.
No comments:
Post a Comment