KANUNI MUHIMU YA MAFANIKIO KWENYE BIASHARA.
Nakushirikisha kanuni muhimu sana ya mafanikio kwenye biashara, ambayo ukiifuata kwenye biashara yako, utapiga hatua sana.
Kanuni hiyo inasema; eneo sahihi, muda sahihi, suluhisho sahihi, mawasiliano sahihi, hatua sahihi, malipo sahihi, rudia.
- )ENEO SAHIHI.
Kuna biashara nyingi ambazo zinaanzishwa
maeneo ambayo siyo sahihi, unakuta biashara ni nzuri, lakini kwa ilipo
haina wateja. Unapawa kuanzisha biashara kwenye eneo sahihi, eneo ambalo
wateja wapo ili uweze kuendesha biashara.
- )MUDA SAHIHI.
Kuna biashara ambazo zinaanzishwa kwenye
eneo sahihi, lakini kipindi ambacho zinakuwa zimeanzishwa siyo sahihi.
Labda watu wanakuwa hawajaielewa biashara hiyo, au siyo msimu wa watu
hao kutumia kitu kinachouzwa. Unapaswa kuanzisha biashara kwa wakati
sahihi.
- )SULUHISHO SAHIHI.
Unaweza kuanza biashara eneo sahihi na
lenye wateja wenye uhitaji, lakini usiuze kama kile unachouza
hakiwasaidii wateja kutatua tatizo walilonalo. Biashara yako inapaswa
kutatua tatizo sahihi la mteja.
- MAWASILIANO SAHIHI.
Unaweza kuwa na biashara uliyoanzisha
eneo sahihi, ukawa na suluhisho sahihi kwa wateja wako na bado usiuze,
kama hautakuwa na njia sahihi ya kuwasiliana na wateja wako. Ili watu
wajue na kununua unachouza, lazima uwasiliane nao, lazima uwe na mpango
wa masoko ambao unawafikia wateja wa biashara yako na wanajua kuhusu
uwepo wako na wananufaikaje na kile unachouza.
- )HATUA SAHIHI.
Hatua unazochukua kwenye biashara yako
ni muhimu sana. Ili biashara ikue na kuleta faida, lazima uchukue hatua
kubwa, kuwafikia wengi na kuwapa huduma bora kabisa. Kama unafanya
biashara kwa ukawaida, huendi hatua ya ziada, usitegemee matokeo makubwa
kutoka kwenye biashara hiyo. Kwenye biashara na kwenye maisha kwa
ujumla, unapata kile unachotoa.
- ).MALIPO SAHIHI.
Unaweza kuwa na biashara sahihi, eneo
sahihi, suluhisho sahihi na wateja wananunua sana. Lakini malipo
yasipokuwa sahihi, hutaweza kupiga hatua. Kama unauza bei rahisi ili
wengi wanunue, na unapata faida ndogo, hutaweza kutoa huduma bora na
hata kupiga hatua kutakuwa kugumu. Lazima uipangilie biashara yako kwa
namna ambayo malipo unayopata yanakuwezesha kuendesha maisha yako na
hata kutoa huduma bora zaidi kupitia biashara hiyo.
- ).RUDIA.
Ukishaanzisha biashara inayokidhi vigezo
vyote hivyo sita, hapo sasa unayo biashara, unayo mashine ya kuchapa
fedha. Sasa ukishakuwa na mashine ya kuchapa fedha unahitaji nini tena?
Ni kurudia huo mchakato kila wakati. Kila siku boresha biashara yako
kwenye maeneo hayo, na pia angalia fursa nyingine ambapo unaweza kutumia
kanuni hiyo kuanzisha na kukuza biashara mpya.
No comments:
Post a Comment