Bila
ya hekima, fedha na afya tunazopigania kuwa nazo, zitatupoteza kabisa.
Hekima ndiyo inayotuongoza vizuri kwenye maisha yetu, ndiyo
inayotuwezesha kufanya maamuzi sahihi kwetu ambayo yanafanya maisha yetu
yawe bora zaidi.
KUSOMA;
kila siku ya maisha yako, soma angalau kwa dakika 30, na soma vitabu
vinavyoongeza maarifa na uelewa wako kwenye kile unachofanya na hata
maisha kwa ujumla. Tenga na linda sana muda huu wa kujisomea, ndiyo
utakaokutoa hapo ulipo sasa na kukufikisha mbali zaidi.
UZOEFU WA WENGINE;
chagua watu ambao utajifunza kupitia wao, hawa tunawaita menta.
Unapaswa kuwa na mtu ambaye unataka kufikia hatua ambazo amefikia yeye,
kisha kujifunza kila kitu kuhusu yeye. Kama yupo hai na yupo karibu
unaweza kutafuta nafasi ya kuonana naye. Na kama yupo mbali huwezi
kumfikia au alishafariki basi jifunze kupitia maandiko yake na hata
maandiko yaliyoandikwa kuhusu wewe. Mazuri aliyofanya na pia jifunze
makosa aliyoyafanya ili uweze kuyaepuka.
KUTAFAKARI;
Unapaswa kuwa na muda wako mwenyewe, muda wa kutafakari, kuyatafakari
maisha yako na kutafakari kila unachofanya, kuanzia ulikotoka, ulipo
sasa na kule unakokwenda. Kila mwisho wa siku yako tafakari kila hatua
uliyochukua kwenye siku hiyo na angalia wapi umefanya vizuri, wapi
umekosea na wapi unahitaji kurekebisha na kuboresha zaidi. Majibu ya
maswali mengi uliyonayo kuhusu maisha tayari unayo, ni wewe kutafakari
na kujisikiliza na utapata majibu mengi sana.
No comments:
Post a Comment