1. Amka asubuhi na mapema sana, angalau masaa mawili kabla ya muda wako wa kuanza kazi.
2. Unapoamka cha kwanza kufanya shukuru, kwa sala au tahajudi.
3.
Andika malengo yako makubwa kila siku unapoamka, malengo ya mwaka,
miaka 5, miaka 10 na hata miaka 50. Lazima uwe na malengo ya aina hii.
4. Ipangilie siku yako kabla hujaianza, weka vipaumbele vyako kwa siku husika, viwe kati ya 3 mpaka sita. Andika kabisa nini utafanya na kwa muda gani wa siku hiyo.
5.
Soma kitabu au pata maarifa yoyote chanya na ya hamasa kabla hujaianza
siku yako. soma angalau kurasa kumi za kitabu kila siku.
6. Fanya mazoezi ya viungo kabla ya kuianza siku yako, mazoezi bora kabisa ni kukimbia.
7. Epuka habari au kitu chochote hasi muda wa asubuhi. Usisikilize redio, wala kuangalia tv au kusoma magazeti.
8. Unapoingia
kwenye kazi au biashara yako, fuata vipaumbele ulivyoweka vya kufanya
kazi, na unapokamilisha jukumu weka alama ya vema kisha nenda kwenye
jukumu jingine.
9. Fanya jambo moja kwa wakati, usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja, unapoteza nguvu na umakini.
10. Unapofanya kazi, akili na mawazo yako yote yawe kwenye kile unachofanya, usiwe unafanya kazi huku unafikiria vitu vingine.
11. Kula
kwa afya, punguza sana vyakula vya wanga na sukari, kula matunda na
mbogamboga kwa wingi na kunywa maji mengi zaidi, angalau lita tatu kwa
siku nzima.
12.
Ondoka kwenye mitandao yote ya kijamii unayotumia kama haikuingizii
fedha moja kwa moja. Sheria ya kutumia mitandao ya kijamii iwe hii, iwe
inakuingizia fedha moja kwa moja. Kama hakuna fedha inayoingia kupitia
mitandao hiyo, achana nayo mara moja.
13. Acha kabisa kutumia kilevi cha aina yoyote ile, kuanzia pombe, sigara, madawa ya kulevya na hata viburudisho kama kahawa.
14. Kwenye
kila kipato unachoingiza, sehemu ya kumi ya kipato hicho usitumie kwa
namna yoyote ile, hicho ni kipato ulichojilipa na utakitumia kwa
kuwekeza kwa ajili ya baadaye.
15. Imarisha
sana mahusiano yako na watu wote wa karibu kwako, kuanzia familia yako,
ndugu, jamaa na marafiki na pia wale unaohusiana nao kwenye kazi au
biashara.
16. Imalize
siku yako kwa kutafakari yale uliyofanya, matokeo uliyopata, makosa au
changamoto ulizokutana nazo na namna unavyoweza kufanya kwa ubora zaidi
siku inayofuata.
17. Lala mapema ili uweze kuamka mapema, kama hufanyi kazi za usiku, saa nne inapaswa kukukuta kitandani ukiwa umeshalala.
18.
Tumia neno HAPANA mara nyingi uwezavyo, neno hapana ndiyo litakupa
uhuru wako. Kama kitu hakikuwezeshi kufika kule unakotaka kufika, sema
hapana bila ya kuona aibu.
Ndimi MWL JAPHET MASATU, DAR ES SALAAM , TANZANIA.
MOBILE PHONE: WhatsApp +255 716924136 / +255 755400128 / +255 688 361 539
EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
No comments:
Post a Comment