Huwezi kutengeneza na kutunza maono ya utajiri kama unahamisha mawazo yako kwenda kwenye picha inayokinzana mara kwa mara.
Hupaswi kufikiria kitu kinachopingana na utajiri unaotaka kwenye maisha
yako. Muda wako wote fikiria ile picha ya utajiri uliyojitengenezea.
Usizungumzie
kuhusu umasikini uliokuwa nao au wazazi wako waliokuwa nao,
usizungumzie kuhusu hali mbaya ya uchumi au mabaya yoyote yanayoendelea.
Hata kama mambo ni magumu kiasi gani, hayo yanapita, hayadumu milele.
Hivyo usiharibu fikra zako kwa kuyafikiria au kuyazungumzia.
Peleka mawazo na akili zako zote kwenye utajiri na ipe picha unayotaka kufikia na waache wengine wahangaike na hayo mengine.
No comments:
Post a Comment