Afya
ndiyo mtaji wa kwanza na muhimu sana kwenye maisha yetu, bila ya afya
bora na imara huwezi kufanya chochote kikubwa kwenye maisha yako. Afya
unaweza kuichukulia kirahisi sana unapokuwa nayo, lakini ukishaipoteza
gharama zake ni kubwa sana.
KULA VYAKULA
vya kiafya kwa kuepuka sukari, kupunguza wanga na kuongeza zaidi
mbogamboga, matunda, mafuta na protini. Sumu namba moja kwenye afya zetu
ni wanga na sukari, ukiweza kudhibiti hili utakuwa na afya bora.
KUFANYA MAZOEZI,
kila siku fanya mazoezi ya kukimbia kwa angalau nusu saa. Mazoezi ya
kukimbia ni mazoezi bora kabisa na yasiyo na gharama kwako. Hakikisha
unafanya haya kila siku.
KUPUMZIKA,
pata muda wa kutosha wa kulala kulingana na uhitaji wa mwili wako. Kwa
wastani binadamu tunahitaji masaa 6 mpaka 8 ya kulala kwa siku. Jua
mwili wako unahitaji kiasi gani na kila siku upe muda huo. Hili
litakufanya uwe imara na kuweza kuweka juhudi kwenye shughuli zako.
No comments:
Post a Comment