Friday, May 29, 2020

JE , WEWE NI MWANDISHI NA MCHAMBUZI WA VITABU , SOMA KILA SIKU NA SHIRIKISHA WENGINE ULICHOJIFUNZA.

1. Andika kile ambacho kinatoka ndani ya moyo wako, kile ambacho unasukumwa kukiandika, na siyo kuandika kuwafurahisha watu.
2. Tengeneza sauti yako ya uandishi, unaweza kuwa na waandishi au mwandishi unayemkubali au kujifunza kwake, ukajikuta unaandika kama yeye, huwezi kufika mbali kiuandishi, tafuta mtindo wako mwenyewe wa uandishi, ambao utakutofautisha.
3. Kazi ya uandishi kuna wakati ina upweke mkubwa, inakuhitaji uwe na muda mwingi peke yako kuliko kazi wanazofanya wengine, lazima uwe tayari kwenye hilo.
4. Unastahili na unapaswa kulipwa kupitia uandishi wako, usiache kuwataka watu walipie pale wanapotaka zaidi kutoka kwako.
5. Chagua hadhira utakayoiandikia na cha kutaka kila mtu awe msomaji wako, kama unalenga kila mtu huna unayemlenga. Jua kabisa unamwandikia mtu wa aina gani, na hapo uandishi wako utagusa maisha ya mtu.
6. Unaweza kuandika makala 100 nzuri kabisa, na watu wachache mno wakakushukuru au kukupa moyo kwa unachofanya. Lakini ukaandika makala au kutuma ujumbe mmoja ambapo umekosea na utashangaa kila mtu anakukosoa na kukupinga. Hata watu ambao hawajawahi kukupa moyo kwa makala nzuri 100 ulizoandika, watakuwa wa kwanza kukuhukumu kwa makala moja mbaya uliyoandika. Elewa hilo na usikubali likuumize.
7. Sehemu kubwa ya wale wanaokukosoa kwenye uandishi ni wivu tu. Wanatamani wangeandika, ila hawawezi kukaa chini na kuandika, wakiona wewe unaandika wanatafuta makosa ya kuonesha kwamba wewe siyo bora kuliko wao.
8. Epuka sana kujisifia kila wakati kupitia uandishi wako, watu wana wivu, kadiri unavyojisifia ndivyo wanavyotafuta makosa ya kukurudisha nyuma.
9. Usisubiri ukamilifu, andika na toa, iwe ni makala au kitabu au chochote, una nafasi ya kuboresha zaidi baadaye, kwa kutoa toleo la pili na mengine mengi.
10. Fanya uandishi kuwa kitu cha kwanza kwenye siku yako, andika kabla hujaendelea na ratiba nyingine za siku yako. Ukishindwa kutenga muda wa asubuhi na kuandika, ni vigumu sana kupata muda siku yako ikishaanza, na pia siku inavyoenda unachoka, na akili ikishachoka, utajipa kila sababu kwa nini usiandike.
Makala  hii  imeandikwa   na  KOCHA   MWL    JAPHET   MASATU  ambaye  ni  mwalimu  kitaaluma ( B.Ed ( AE ) , Kocha  wa  MAISHA   NA  MAFANIKIO , MWANDISHI  na  MJASIRIAMALI  , BLOGGER
WhatsApp + 255 716  924 136 /  + 255 755 400128  /   + 255 688 361 539

No comments:

Post a Comment