Rafiki, kila siku unasema, *sina muda* , kumbe ni wewe tu hujui namna ya kuutumia.
Haupo peke yako.
Kila siku unajiambia “sina muda”,
...lakini unatumia masaa mengi (masaa manne kwa siku) kwenye mitandao ya kijamii (WhatsApp, Facebook, Instagram, TikTok).
Unasema unataka kufanikiwa, lakini ratiba yako inasoma: kulala, kula, kuskrolu kwenye mitandao, kulalamika.
Unajua ni nini kinauma zaidi?
Ni kuona mtu ambaye alikuwa hana chochote, alikuwa anakunywa chai kavu na maandazi ya mia tano, leo hii anaingiza laki kwa siku,
... na bado wewe uko pale pale.
Tofauti si akili, si bahati, ni jinsi mtu alivyoamua kutumia muda wake.
Wengi wameaminishwa kuwa mafanikio ni kwa watu waliobahatika, au waliotoka familia nzuri.
Lakini ukweli ni huu: kila mtu ana masaa 24.
Elon Musk ana masaa 24.
Wewe pia una masaa 24.
Ukitumia saa 1 kwa siku kuboresha maisha yako, hayo ni masaa 365 kwa mwaka.
Nani anakuzuia?
Zifuatazo Ni Mbinu 3 Za Kuchukua Hatua Leo:
1. Saa Moja Tu Kila Siku:
Jifunze kitu kimoja kinachoweza kukuingizia kipato (kama Copywriting, content creation).
Simu yako iwe zana, sio toy.
2. Panga Muda Kama Mzigo Wa Gari:
Jua dakika zako zinaenda wapi.
Tengeneza ‘to-do list’ ya kweli, sio ndoto.
Fanya vitu 3 vya maana kila siku kabla ya saa tano asubuhi.
3. Tafuta Mtandao Wa Watu Wenye Malengo:
Unakuwa kama watu 5 unaotumia nao muda mwingi.
Kama wote ni wasumbufu, utakua msumbufu pia.
Hii hapa ndiyo ile hadithi ya kweli ya Kelvin wa Tandika:
Jamaa alikuwa mtaani, hana kazi rasmi.
Aliamua kujifunza jinsi ya kuuza bidhaa za watu wengine kupitia WhatsApp na Instagram.
Kila siku aliweka saa moja kujifunza na kupost.
Mwaka mmoja baadaye, ana duka la perfume na ameshaandika eBook inayoingiza hela kila mwezi.
Alianza na muda, si mtaji.
Usilale na “kesho nitaanza.”
Anza leo.
Kumbuka; Muda haukupi second chance, ila wewe unaweza kuamua kuanza upya leo.