Friday, April 16, 2021

KAMA UNATAKA KUVUNJA TABIA FULANI AU URAIBU , USIJIRUHUSU KUWA KWENYE HALI HII YA KUFANYA KWA MAZOEA.

Siku moja mwandishi wa vitabu Tom Corley alifanya utafiti wa tabia za kila siku za matajiri 233 na pia akachunguza tabia za kila siku za watu maskini wapatao 128.

Alichogundua ni kuwa kulikuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya tabia za maskini na matajiri.  

Katika kipindi cha utafiti wake aligundua kuna karibu mambo 300 ambayo hutofautisha wanaofanikiwa na wale ambao hawafanikiwi maishani.

Mara nyingi ni rahisi sana kufikiri kuwa tofauti ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa hutokana na mambo makubwa sana yanayotutofautisha.

Ukweli ni kwamba tabia ina nguvu kubwa ya kuamua hatima yako ufanikiwe au ufeli.

Tabia za kitajiri ni ngumu kuzijenga na ni rahisi kuzivunja, upande wa pili ni kinyume chake tabia za kimaskini  ni rahisi kuzijenga na ni ngumu kuziacha.  

Na hii ni kwa sababu Ujengaji wa tabia huwa unaanzia kwenye akili zetu, hivyo hata kuzivunja lazima kuanzie kwenye akili zetu pia.

Huwa tunaijenga tabia kwa kutumia nguvu ya kufikiri lakini tabia ikishajijenga huwa tunaitekeleza bila hata ya kufikiri(mindless).

Chukua mfano mdogo wakati unajifunza kuendesha baiskeli au gari.

Mwanzoni ulikuwa unafikiria kila unachofanya , hukuweza hata kuongea na mtu wakati unaendesha, maana kila wakati ulikuwa unafikiri kuchochea au kukanyaga mafuta, breki na kubadili gia.

Lakini baada ya kuwa dereva mzoefu, unajikuta unaendesha bila hata ya kufikiria , tena unaweza kuendesha huku ukiwa unaongea na wengine.

Mfano huo unatuonesha jinsi akili zetu zinavyojenga tabia , mwanzo tunatumia nguvu na umakini mkubwa kwenye kufikiri lakini baadaye tunaifanya bila hata ya kufikiri.

Ni hiyo hali ya kufanya bila ya kufikiri ndiyo inayojenga na kufanya uraibu uwe mgumu kuvunja.

Wengi wenye uraibu huwa wanajikuta wameshafanya kile walichozoea bila hata ya kufikiri.

Kwenye teknolojia na mitandao ya kijamii ndivyo pia uraibu unajengeka.

Awali wakati unaanza kujifunza kutumia simu janja au mitandao ya kijamii ulikuwa unatumia nguvu na kufikiri.

 Ila baadae inakuwa rahisi kwako , unajikuta umeshika simu na uko kwenye mitandao ya kijamii bila hata ya kufikiria.

Ili tuweze kuvunja uraibu huu na wa aina nyingine , tunapaswa kutumia akili zetu vizuri, kama zilivyotuwezesha kujenga tabia, hivyo pia zitatuwezesha kuvunja tabia na uraibu.

Kama unataka kuvunja tabia za kimaskini ambazo zinakupotezea muda na zina kurudisha nyuma na huzipendi, huna budi kutumia uwepo wa akili (mindful) , mbinu hii itakusaidia sana kuvunja tabia nyingi mbaya.

Hii ni mbinu ambayo imenisaidia mimi na maelfu ya watu

KARIBU  UJIUNGE   DARASA  ONLINE   UJIFUNZE ZAIDI

 WASILIANA  NAMI--KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

WhatsApp + 255 716924136  /   + 255 755  400  128

2 comments:

  1. Kupitia " DARASA ONLINE "" utajifunza mambo saba(7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

    Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

    Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.

    Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

    Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu. Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

    Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

    Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

    Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

    Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

    Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

    Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

    Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

    Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

    Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

    Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

    Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

    Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

    Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

    Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

    Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

    ReplyDelete