Saturday, June 20, 2015

SIRI YA UTAJIRI ----BUNI MRADI UNAOTATUA MATATIZO YA WATU ! UTAPATA PESA !!






 




Kwa  wafanyabiashara  na   wajasiriamali  maana  kuu  ya  biashara  zote  ziwe  ni   za  mjasiriamali    mdogo  au muwekezaji  mkubwa  ni    KUTATUA   MATATIZO  YA  WENGINE “.   Tunasema  mtu  fulani  kafanikiwa  kimaisha. NI   TAJIRI !   .Ana  pesa  nyingi. Naam ! Ni  kweli  kafanikiwa , lakini  amefanya  nini  kupata  pesa hizo ? 
SIRI  NI  HII : Katatua  matatizo  ya  watu  ! Naam , ndiyo  ukweli. Hakuna  njia  ya  mkato !!  BUNI  shughuli  inayotatua  matatizo  ya  watu, utapata  PESA !!

        Kabla  ya  kuanza  biashara  yoyote  hata  kama  ni  ndogo  kiasi  gani   , FANYA  UTAFITI  wa  kutosha  kama  biashara  unayotaka  kufanya  kama  inaweza   kuwatatulia   watu  matatizo  yao ?   Kama  jibu  ni  NDIYO    basi   ANZA  MARA  MOJA , hakika  UTAFANIKIWA .  Kama  jibu  ni   HAPANA   , LIACHE   MARA  MOJA !  Huwezi   kufanikiwa  kwa  kuuza  sweta  na  Mwamvuli   wakati  wa  joto . Ukipata  HASARA  utalalamika,    Mie  nina   mkosi ! “  

        Siyo  mkosi ! Bali  umeshindwa  kuwatatulia watu  shida  zao. Watu  hawana  shida  ya   sweta  au  mwamvuli. Biashara  yako   imekosa  maana.Ulifikiri  maana  ya  biashara  ni  kupata  pesa ?  La  hasha ! Maana  na  sababu  ya  biashara  yako  ni  kutatua  MATATIZO  YA  WATU.   Ndugu  yangu    kupata  Pesa  ni  malengo   yako  tu.  ANGALIA   MAZINGIRA , NYAKATI, WATU,

Kwa  mfano  kuna  kijiji  au   mji  wana  ukosefu  wa  mafuta  ya  taa. Karibu   watu  200  katika  kijiji  hicho  au  mji  huo   wanalazimika  kusafiri  mamia  ya    kilometa  kufuata  mafuta  ya  taa  katika  kijiji  kingine  au  mji  mwingine. Kama  utaleta  duka lenye   kuuza   mafuta  ya  taa  hapo . NINI  KITATOKEA  HAPO ?  JIBU  UNALO :  NI  KUPATA  PESA .

ANGALIZO : Usiseme  unataka  kufanya  biashara  YOYOTE  ile    kwani  kusema  kwamba  unataka  kufanya   biashara  yoyote  ile  BILA   YA  KUFANYA UTAFITI  NI  KUPOTEZA  MWELEKEO  ndugu  yangu  kwa  kuwa  utakuwa  HUJUI  UNATAKA  KUFANYA  NINI , Watu   wana   shida  gani  hapa ?au  eneo  unaloishi ?   Wanahitaji   nini ?  Nini  hawana  ?. Kama  hujui  cha  kufanya  hakuna   kitu  utakochofanya. HILI  NI  TATIZO  LA  WATANZANIA  WENGI !!


                    WAZO + UTAFITI +  MTAJI==  BIASHARA


KWANINI  UTAFITI   NI   MUHIMU  KABLA  YA  BIASHARA ? Kutofanya  utafiti  ni  chanzo   cha  biashara  nyingi  kuanguka  au  kuharibika.
Utafiti  ni   moja  ya  sababu   zilizowafanya  Wazungu  wafike  hapo  walipo leo. Wao  wamewekeza  zaidi  kwenye  UTAFITI   kuliko  kitu  chochote.Je, unaifahamu  JAPAN ? K una  wakati  maendeleo  yake  yalikuwa  kama  Tanzania. Lakini  baada   ya   kuwekeza  kwenye  UTAFITI , leo  ni  ya  tatu   duniani  kwa  uchumi. Leo  hii  nchi  ya  CHINA  ina   nguvu  kubwa  kiuchumi. Ni  tishio  duniani .Ni  matokeo  ya  kuwekeza  katika  UTAFITI.Hizo  ni  nchi ,  lakini    UTAFITI   unahitajika  sana   pia   kwa   mtu   binafsi  kwa  ajili  ya  maendeleo  yake.
      Unapofanya  UTAFITI   utajua  watu   wanahitaji  nini ?  Nini  hawana ?Baada  ya   kuwaza  fanya  UTAFITI . Hata  kama  utatumia   miezi , miaka  katika  utafiti wako. Hakika   utakachofanya  hapo  baada   ya    UTAFITI , watu   watakubali , watakuheshimu. Usikurupuke  tu  kwa  kuiga  fulani  alifanya  hivi  akapata   pesa ,  nawe  unaingia.  Mh !  Hatari  ndugu  yangu !  Vitu   vya  kuigilizia   havimfikishi  mtu  mbali . USIIGILIZIE, JIFUNZE  KISHA  LIPA   GHARAMA  NA   UTOE  VYA  KWAKO. Watanzania  wengi  wanapenda  vitu  bwelele , vya  rahisi  rahisi  hawapendi  kulipa  gharama ! 


JITAMBUE  :  Nataka  utambue  kitu  muhimu  kwamba   wewe  ni  wa  pekee  katika  kila kitu  hapa  duniani. Uliumbwa  kwa  jinsi  ya  ajabu   na  ya  kutisha     { ZABURI  139 : 14 }, hakuna  aliye  kama  wewe  ulimwenguni  kote , kwa  hiyo  usijaribu  kuwa  fulani. Unaweza  kutamani    jinsi  watu  fulani  wanavyofanya  mambo    yao    lakini usisahau  kwamba  wapo    wanaotamani   jinsi  unavyofanya  wewe  pia. Kama  bado  hujawaona  subiri  kidogo  wanakutafuta. Mtu   mmoja   mwenye  hekima   akasema ,  “ washa  moto  kwenye  kichwa  chako ,  watu   lazima  watakuja  tu   kuona  jinsi  unavyowaka “ Watu  hawana  haja  ya  kuona  marudio, wanataka   kuona  vitu  vipya.  Nitaandika   makala   yenye  kichwa   USIIGE    BALI  JIFUNZE   NA  TOA    CHA   KWAKO “ ndani  ya  blog   hii   MAISHA   NA  MAFANIKIO  BLOG. Endelea  kutembelea    blog  hii  ujifunze   siri  za   kufanikiwa   katika  maisha ! UNAWEZA  KUFANIKIWA ! HUJACHELEWA  !!


 JE,  NITAFANYA  BIASHARA  GANI ?
 Lazima   ujiulize  kwamba  unataka  kufanya    biashara  gani ? Fanya  UTAFITI  wa  kutosha  kama   biashara   unayotaka  kufanya  itakuwa  na   manufaa ,  au   laa !   Njia  ya  kukusaidia  ndugu  yangu   mtanzania   kuamua  ufanye  biashara  gani  ni  katika  utafiti  wako  ujiulize   maswali   yafuatayo :--
  {1}. Umewahi  kufanya   kazi  au  biashara  gani ?
   {2}. Umesomea   nini ?
   { 3}. Vipaji  vyako  ni  vipi ?
   {4 }. Ni  biashara  ipi  au  kazi  ipi  unapenda  zaidi  kuliko  nyingine   na  kwa  sababu  gani ?
  {5}. Je,  jambo  ninalotaka  kufanya   litaleta  faida ?
  {6}. Je, litawaondolea  watu  matatizo ?
   {7}. Je, litabadilisha  maisha  yangu  kwa  kiwango  gani  ?
   {8}.Je, watu  waliowahi   kufanya  kama  ninalotaka  kufanya   wakoje ?
{9}.J e,  watu  wanasemaje ?
{10 }.Je,  eneo  linafaa     kufanyia  shughuli   hii ? 

      Orodha  ni  ndefu . Ukisha   jiuliza  maswali   haya  chukua   kalamu  na  karatasi   uandike   maswali    yako  na  kuyajibu.Ukikagua    maswali   na  majibu  yako  utagundua   shughuli    unayoipenda , unayoiweza   na  una   kipaji   na   hiyo  ndiyo  inayokufaa. Ukishachagua  biashara   unayoipenda  ni  rahisi  sana   KUFANIKIWA  kwani   shughuli   utazifanya  kwa   hiyari   bila    kujilazimisha.
USHAURI    WANGU :  Kama  utakuwa   bado   hujafikia  uamuzi   baada  ya  hapo  basi  tafuta   na  wasiliana   na   washauri   ili   mbadilishane  mawazo   na   ufundishwe   jinsi    ya   kuamua   ufanye   biashara   gani .


 

MAMBO  MUHIMU  YA   KUFANYIA   UTAFITI    KABLA  YA  BIASHARA
{1}. Kujua  siri  ya  biashara   unayotaka   kufanya  ili  upate  mbinu  za  kupata  mafanikio.Unaweza  kupata  siri   au  kujifunza  mbinu   kutoka   kwa  watu  wanaofanya  biashara  kama  unayotaka  kufanya.Suala  hili  ni  gumu  sana  kwani   wafanyabiashara  wengi   huwa   wanaficha   siri  za  biashara  zao  ili  kulinda   wasizidiwe  maarifa  na  washindani  wao.Unaweza   kuipata  siri  hiyo  kama  utakwenda   kupata  ushauri  toka   kwa  mfanyabiashara  ambaye  yuko  mbali  na  mahali  unapofanyia  biashara , au  tafuta  ushauri  kwa  wataalamu  wa  mambo  ya  biashara.

{2}.Fanya  utafiti  wa   soko  la   bidhaa  unazouza  au   unazotarajia  kuuza. Jiulize , je,  bidhaa  unazotaka  kuziuza  zina  soko ? Utawauzia    watu  gani  na  utauzaje ? Kama  wewe   ni   ni  mzalishaji , una   mazao /  bidhaa  unapaswa   kuuza  kwa   jumla , mchanganyikio   ama   rejareja ? Je, utatangaza   vipi   bidhaa  zako ? Nitafundisha   kwa  kirefu  katika  makala   yenye  kichwa   “ TANGAZA  KILE  ULICHONACHO /TANGAZA  HUDUMA  AU   BIDHAA  ZAKO “  

{3}. Tengeneza  bajeti  yako  kwa   kuorodhesha  vitu  vinavyohitajika  na  gharama  zake  ili  kuweza   kuanzisha   biashara  yako.  Vitu  hivyo   ni :--
 {a}.Gharama  za   Kujenga  au  kupanga  ofisi.
 {b}.Gharama  za   Leseni  ya   biashara.
 {c}.Makadirio  ya   KODI  toka  TRA.
 {d}.Gharama  ya  vifaa  vya  ofisi  yaani ,  Samai, makaratasi, mitambo, mashine, n.k.
 {e}.Manunuzi  ya  malighafi  au  bidhaa  za  kuanzia   biashara.
 {f}.Idadi  ya    wafanyakazi     na  gharama  za  mishahara  yao.
 {g}.Gharama  nyinginezo  kama   vile   umeme , maji, n.k.
{4}.Unatakiwa  kujua  ni   MTAJI  kiasi  gani  unahitajika  kuanzisha  biashara  yako. MTAJI   HUO   utaujua  baada  ya  kujumlisha   gharama   zilizoorodheshwa  katika  kipengele   namba { 3}  hapo  juu. Gharama   hizi  ni  za  mwaka  ule   wa  kwanza  wa  kuanzia  biashara.

{5}. TAFUTA   MTAJI
Mtaji  unaweza   kupatikana  kutoka  kwenye  vyanzo  vifuatavyo :
 {a}. Akiba au   mshahara.
 {b}.Msaada  au   mkopo  kutoka  kwa  ndugu  na  jamaa.
 {c}. Kuingia  ubia  na mtu   mwenye  mtaji
 {d}. Mkopo  toka  baadhi  ya  asasi  kama  vyama  vya  akiba   na   mikopo {SACCOS },NGO  za  kifedha   isipokuwa  Benki  kwani   hizi   huwa   hazitoi  mikopo  kwa  mtu  anayeanzisha  biashara.
Nitafundisha    kwa  kirefu  katika  makala   yenye  kichwa   “ NI   VIPI   UPATE  MTAJI ?  Pia  nitafundisha   “ UNASHINDWA  KUPATA  MKOPO  BENKI ? NJIA  HIZI   HAPA.
 “ Kuna  njia   moja  tu  ya  kujitengenezea  pesa  nyingi , nayo  ni  biashara   yako  mwenyewe “ {  J.PAULO  GETTY }.

Asante   msomaji  wangu  kwa  kusoma  makala   hii   nzuri  yenye  kuelimisha !  Tembelea    MAISHA  NA  MAFANIKO  BLOG”  kwa  kujifunza  mambo   mapya   kila  siku !!  USIKATE  TAMAA , UNAWEZA  KUFANIKIWA !!  Mungu  Akubariki !!


Makala  hii  imeandikwa  na  MWL   JAPHET  MASATU . Ni   Mwl  wa  Saikolojia, Elimu  ya  Maisha na  Mafanikio ,  Biashara / Ujasiriamali.Anapatikana  kwa namba  + 255 716  924 136 /  +  255  755  400  128 /  +  255 785  957   077. 

 Kama  una  lolote  unataka  kuchangia   mawazo , ushauri   kuhusiana  na   mada  yetu  hii  .  Karibu  sana.
Kama   una  swali   lolote   kuhusiana   na   mada  yetu  hii   msomaji  wangu   uliza !!!


 

No comments:

Post a Comment