Wakati wa mlipuko kama huu, hakuna anayejua nini kitatokea kesho, na
kadiri mambo yanavyozidi kuwa mabaya, ndivyo watu wanaendelea kutabiri
kwamba mambo yatakuwa mabaya zaidi.
Watu wanatishana na kupeana wasiwasi mkubwa. Wapo wanaosema huu ndiyo
mwisho wa dunia. Kila mtu ana maoni yake. Lakini tunajua kitu kimoja
kuhusu maoni, siyo ukweli.
Hakuna aliyeweza kutabiri ujio au madhara ya mlipuko huu, na hakuna
anayeweza kutabiri kwa uhakika mambo yataendaje. Tunachojua ni kwamba
tutavuka hili, kama ambavyo jamii ya binadamu imevuka mengi siku za
nyuma.
Hivyo wewe kuwa chanzo cha matumaini sahihi kwa wateja wako. Katika
hali ya wasiwasi kama hii, watu wanapenda kuwasikiliza wale wanaoleta
habari njema, lakini siyo habari njema hewa. Bali habari njema sahihi.
Usiwe mtu wa kutoa habari mbaya kwa wateja wako, utawatisha na
kuwafanya waahirishe kununua. Badala yake kuwa mtu wa kutoa habari
njema, mtu wa kuwapa wateja wako moyo na hapo watajisikia vizuri na
kununua. Ukiweza kuwaonesha jinsi kile unachouza kinawasaidia kupunguza
makali ya mlipuko, wateja wanakujali zaidi.
Mfano; biashara za ushauri na mafunzo zinapaswa kuwa
chanzo cha matumaini kwa wateja wake. Kwa kuwaonesha kwamba hili
linaloendelea siyo mwisho wa dunia na mambo yatakwenda vizuri baada ya
hili.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment