Kama unafanya biashara ya kununua kwa jumla na kuuza kwa reja reja,
unapaswa kujihakikishia upatikanaji wa mali katika kipindi hiki cha
mlipuko. Kutokana na mipaka ya nchi nyingi kufungwa na shughuli
kusimamishwa, hili linaathiri sana uzalishaji. Hivyo jipange mapema kwa
kuhakikisha una mzigo wa kutosha katika kipindi cha mlipuko.
Kama unafanya biashara ya kuzalisha bidhaa, basi jihakikishie
upatikanaji wa malighafi katika wakati huu wa mlipuko. Mabadiliko
yanayoendelea yataathiri sana upatikanaji wa malighafi, jipange kwa
kuhakikisha hilo haliathiri uzalishaji wako.
Mfano; wafanyabiashara wa bidhaa zinazotoka nje,
kama nguo kutoka china, wamejikuta katika wakati mgumu kupata mzigo mpya
tangu mlipuko huu uanze. Hivyo ni muhimu kuangalia njia nyingine ya
kupata mzigo na kuhakikisha unapata mzigo wa kutosha kwa sababu hujui
mlipuko huu utaisha lini.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment