Wewe mfanyabiashara ukiumwa au wasaidizi wako wakiumwa, biashara
itaathirika zaidi. Hivyo wewe na timu yako mnapaswa kuwa mstari wa mbele
katika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu.
Hakikisha njia zote za kujikinga zinajulikana na kutumika na kila
anayehusika kwenye biashara yako. Njia kuu zinafahamika, kunawa mikono
kwa maji safi na sabuni, kuepuka kushikana, kuepuka kushika uso. Hivi
vyote vinapaswa kufanyiwa kazi.
Pia eneo la biashara liboreshwe kwa namna ambayo linapunguza
maambukizi. Ukaribu baina yako au watoa huduma na wateja unapaswa
kupunguzwa. Maeneo ya kunawa mikono yanapaswa kuwepo au dawa za
kusafisha mikono kupatikana kwa urahisi.
Usiache kujilinda wewe na timu yako kwa kuepuka gharama, ukiugua wewe au timu yako, ni tiketi ya kifo kwa biashara yako.
Mfano; kwenye kila eneo la biashara kunapaswa kuwa
na sehemu ya watu kunawa mikono kwa maji na sabuni au kwa dawa maalumu.
Pia kama biashara inahusisha watu wengi, kuwekwe utaratibu wa kupunguza
msongamano wakati huu. Kwenye huduma za afya, watoa huduma wanapaswa
kuwa na vifaa vya ziada vya kujilinda wao wenyewe.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment