Wakati wa majanga kama haya, wengi huacha kufanyia kazi mikakati yao
ya ukuzaji wa biashara. Kwa kuwa hali ya uchumi inakuwa siyo nzuri,
wateja siyo wengi na waliopo hawanunui sana, wafanyabiashara huona
hakuna haja ya kujisumbua, badala yake wanasubiri mpaka mambo yawe
vizuri.
Kama tulivyoona mpaka sasa, hakuna mwenye uhakika mambo yatarudi sawa
lini, inaweza kuwa kesho, wiki ijayo, mwezi ujao au mwaka ujao, hakuna
ajuaye.
Hivyo wewe endelea na mikakati yako ya ukuzaji wa biashara kama vile hakuna mlipuko unaoendelea.
Endelea na mkakati wako wa masoko kwenye matangazo na hata
kuwatembelea wateja kule walipo, mtaa kwa mtaa, ofisi kwa ofisi na
nyumba kwa nyumba. Ila hakikisha unajikinga na kuikinga timu yako.
Endelea na mkakati wa mauzo kwa kuwashawishi wateja kununua na kununua zaidi ya walivyopanga kununua.
Endelea na mkakati wa utoaji wa huduma bora sana kwa wateja wako ili wanunue tena kwako na wawaambie watu wao wa karibu kununua
Mikakati hii inapaswa kufanyiwa kazi kila siku, iwe kuna majanga au
hakuna. Hata kama huoni matokeo yake kwa haraka, usiache kufanya.
Mfano; mikakati ya masoko, mauzo na huduma kwa
wateja kwenye kila biashara inapaswa kuendelea kama vile hakuna
kilichobadilika, ila iendane na hali halisi ilivyo sasa.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment