Mara
nyingi tumekuwa tunakwepa magumu kwenye maisha yetu, tumekuwa tunaomba
tusikutane na magumu, kwa sababu tunaona magumu ndiyo kikwazo cha sisi
kuwa na maisha tunayoyataka. Lakini hilo siyo sahihi, kama tusingekutana
na magumu kabisa kwenye maisha yetu, maisha yangekosa maana na
tusingeweza kuwa watu ambao tumekuwa sasa.
Magumu
ambayo tumekutana nayo kwenye maisha ndiyo yametufanya tuwe watu ambao
tumekuwa sasa. Hivyo badala ya kukataa na kukimbia magumu, tunapaswa
kuyakaribisha kwa mikono miwili. Kwa sababu kupitia magumu ndiyo
tunakua, na ndiyo tunafikia uwezo mkubwa uliopo ndani yetu.
Kufukuzwa
au kukosa kwako kazi huenda kumekufanya ukaweza kuanza biashara yako.
Kusumbuliwa kwenye mahusiano yako ya mwanzo na yakavunjika ndiyo
kumekupelekea kutengeneza mahusiano mengine bora. Na hata kupata hasara
na kufa kwa biashara yako ya mwanzo kumekuwa funzo la wewe kufanikiwa
kwenye biashara nyingine.
Tusiogope
wala kukimbia magumu, na wala tusiombe kutokukutana na magumu. Badala
yake tuombe kuwa imara zaidi ili kuweza kukabiliana na kila gumu
tunalokwenda kukutana nalo.
No comments:
Post a Comment