Kila
mmoja wetu kuna hadithi ambayo anaiishi, hadithi ambayo umekuwa
unajiambia kila siku na imekuwa kikwazo kwako kupiga hatua. Kwa mfano
kama umetokea familia masikini na huna elimu, hadithi yako inaweza kuwa
kwamba wewe huwezi kufanikiwa kwa sababu umetoka familia masikini na
huna elimu kubwa.
Lakini
hadithi hiyo ni uongo, ni kweli unaweza kuwa umetoka familia masikini
na huna elimu kubwa, lakini hicho siyo kinachokuzuia kufanikiwa. Wapo
wengi waliotoka kwenye umasikini mkubwa kuliko wako na hata hawakupata
elimu kabisa lakini wamefanikiwa.
Hivyo
badili hadithi inayokuzuia kufanikiwa na tengeneza hadithi mpya ya
mafanikio yako ambayo itakusukuma kufanikiwa zaidi. Hadithi yako ya
mafanikio iguse yale maeneo ambayo una uimara na uyatumie kama sababu ya
wewe kufanikiwa.
Hadithi
yako mpya iwe ni kinyume kabisa na ile iliyouwa inakuzuia. Ukishaandika
hadithi hii jiambie na kujikumbusha kila siku mpaka iwe sehemu ya fikra
zako.
No comments:
Post a Comment