Na
hili ndiyo linawasukuma watu kuchukua hatua mbalimbali, kuanzia
kuboresha afya zetu, kuboresha mwonekano wetu, kupata fedha na hata
madaraka ni kwa lengo la kutengeneza furaha kwenye maisha.
Lakini sasa tunapofanya furaha kuwa lengo la mwisho, hapo ndipo tunapojiangusha. Kwa sababu wengi wanafika mwisho wa kile walichofikiri kitawapa furaha, lakini hawapati furaha ambayo walifikiria wangeipata.
Hivyo njia bora ya kuipata furaha, siyo kusubiri mpaka mwisho wa kile tunachofanya, bali kutengeneza furaha wakati unakifanya.
Kama
unataka furaha ya kweli kwenye maisha, basi usisubiri mpaka mwisho wa
kile kitu unachofanya ndiyo uwe na furaha, badala yake tengeneza furaha
kwenye kila hatua unayopiga. Furaha inapaswa kuwa matokeo ya kile unachofanya kila siku, na siyo kusubiri mpaka ufike mwisho.
Na hili ndiyo tunakwenda kujifunza kwa kina kwenye kitabu cha juma hili.
Tafiti
zinaonesha kwamba furaha siyo kitu kinachotokea kwa bahati na wala siyo
kitu ambacho fedha inaweza kununua au madaraka kulazimisha. Furaha haitegemei matokeo ya nje badala yake inategemea jini tunavyotafsiri yale yanayotokea.
Furaha
ni hali ambayo inapaswa kuandaliwa, kutengenezwa na kulindwa na kila
mtu, kwa kuwa na tafsiri sahihi ya kila kinachoendelea kwenye maisha
yako.
Ni kwa kujihusisha moja kwa moja na kila kinachoendelea kwenye maisha yako, kiwe kizuri au kibaya ndiyo tunapata furaha. Siyo
kwa kukimbia au kutoroka yale yanayotokea au kujaribu kuikimbiza
furaha, bali kuyaishi maisha yako kwa namna yalivyo, ndiko kunakokuletea
furaha.
Hivyo
jibu fupi la kuwa na furaha kwenye maisha yako ni kujihusisha moja kwa
moja na maisha yako na kupokea kila kinachokuja kwako, iwe kizuri au
kibaya.
No comments:
Post a Comment