Unahitaji kujizoesha kifikra na kisaikolojia kuwa na fedha nyingi, hata
kama bado hujazishika kwenye mikono yako au kuwa nazo kwenye akaunti
yako ya benki. Na unaweza kuanza kwa kufikiria mara kumi ya kipato
unachopata sasa, kisha kufikiria kipato hicho mara kwa mara, kukiwekea
mipango na kuweka lengo lako la kipato liwe ni kukua kufikia mara kumi
ya kipato chako cha sasa. Kwa njia hii utaongeza kiwango chako cha fedha
kisaikolojia.
Watu wengi wanajua aina moja ya akaunti ya kifedha, ambayo ni akaunti ya
benki, au akiba na uwekezaji ambao wamekuwa wamefanya. Hivyo ukitaka
kuangalia utajiri wa mtu, unaangalia ni kiasi gani cha fedha anacho
kwenye akaunti zake za benki na uwekezaji kiasi gani amefanya.
Aina ya pili ya akaunti ya kifedha, ukiacha akaunti ya benki, ni akaunti
ya fedha ya kisaikolojia. Kila mmoja wetu, ana kiwango chake cha
kifedha kwenye fikra zake, ambacho ndiyo ameshajiambia anapaswa kupata
kiwango hicho. Yaani kila mmoja wetu, kuna kiwango chake cha fedha,
ambacho ameshakiweka kwenye fikra na mawazo yake, na akishapata kiwango
hicho basi akili yake inatulia na hakazani tena kupata fedha zaidi.
Waangalie watu wote ambao wamepata fedha nyingi kwa mkupuo, kiasi
kikubwa cha fedha ambacho hawajawahi kukishika kwenye maisha yao.
Waangalie watu ambao wameshinda bahati nasibu, waangalie watu ambao
wamerithi mali, waangalie watu ambao wamepokea mafao. Wengi haiwachukui
muda wanakuwa wameshapoteza fedha nyingi walizopata na kurudi kwenye
maisha yao ya kawaida.
Wanakuwa wamepata fedha nyingi kwenye akaunti ya benki, lakini
akaunti yao ya kisaikolojia inasoma kiwango cha chini. Hivyo wanaacha
kufikiria kabisa kuhusu fedha, wanaanza kupoteza fedha, mpaka zinapofika
kwenye kile kiwango chao cha kisaikolojia ndiyo wanastuka na kuanza
kufikiria kuhusu fedha.
Pia unaweza kufikiria mara 100, mara 1000 na hata zaidi ya kipato
unachopata sasa. Fikra zote hizo zitaiandaa akili yako kupokea fedha
zaidi na kuweza kutulia na fedha zaidi unazopata. Unapofikiria mara elfu
moja ya kipato unachopata sasa, ongezeko kidogo halitakusumbua kama
linavyokusumbua sasa.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment