Ili biashara yako ikue vizuri na uweze kupata faida, lazima ufukuze baadhi ya wateja.
Kwanza kabisa unahitaji kuwapanga wateja wako kwenye makundi A, B, C, na D.
Kundi A ni wale wateja ambao wanalipa fedha nyingi na siyo wasumbufu.
Kundi B ni wale wateja ambao wapo tayari kulipia, lakini siyo
walipaji wa fedha nyingi, ila ni wateja wenye msimamo, ambao unaweza
kwenda nao muda mrefu, na hawana usumbufu mkishakubaliana.
Kundi C ni wale wateja ambao wanataka punguzo kwenye kila kitu, na
watakusumbua sana, wanaweza kununua kwa bei ya punguzo na bado wakarudi
tena kulalamika kwamba haikuwa sawa kwao.
Kundi D ni wale wateja ambao ni matatizo kwa biashara yako, kwanza
hawalipi kwa wakati, na kwenye kila kitu wanatafuta njia ya kubishana au
kugombana. Hawa ni wateja ambao wanakuja wakiwa wamejipanga kukusumbua,
ili wanufaike zaidi wao.
Ukishawagawa wateja wako kwenye makundi hayo manne, wahudumie vizuri
wateja wa kundi A na B, na fukuza wateja wa kundi C na D, kwa sababu
hawa ni wateja mabao hawana faida, na pia wanakuzuia usiwahudumie vizuri
wateja wa kundi A na B.
Swali ni unawafukuzaje wateja hao?
Zipo njia mbili;
Ya kwanza ni kuwapa utaratibu mpya wa kufanya biashara na wewe,
kwamba yale waliyozoea hayapo tena. Bei ni moja na haipungui na malipo
ni kwanza na siyo baadaye. Kama hawawezi hilo wanaweza kwenda kwenye
biashara nyingine.
Njia ya pili ni kuongeza bei ya bidhaa au huduma unayouza, na moja kwa moja watakimbia wenyewe.
Ukishaachana na wateja hao wasumbufu, nguvu zako peleka kwa wale wateja wazuri wa biashara yako.
Pia unapotangaza biashara yako, hakikisha unatumia lugha inayowavutia
wateja wa kundi A na B, badala ya kundi C na D. Kwa mfano kama tangazo
lako linasema kuna punguzo la bei au zawadi ya bure, utajikuta unavutia C
na D wengi, maana ndiyo wanaopenda rahisi na bure.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment