Kazi kubwa ya kila biashara ni kununua wateja wa biashara hiyo. Sasa
ili biashara iweze kufanikiwa, lazima iweze kununua wateja bora kwa
gharama ambazo siyo kubwa. Kitu ambacho wafanyabiashara wengi siyo tu
hawakifanyii kazi, ila hata hawakijui.
Inawezekana upo kwenye biashara, lakini hujui kama biashara yako
inanunua wateja. Sasa nikuambie tu, kila biashara huwa inatumia fedha
kununua wateja, na biashara yako pia inatumia fedha kununua wateja.
Labda nikuulize swali, biashara yako inatumia gharama kiasi gani
kununua wateja? Na je gharama ambazo biashara yako inatumia kununua
wateja zinarudi? Najua maswali haya yanaweza kukuacha ukiwa umeduwaa kwa
sababu hujawahi kufikiria kuhusu kununua wateja.
Sasa kwenye kitabu nilichosoma ; BUYING CUSTOMERS,
kilichoandikwa na kocha wa biashara Bradley Sugars, mwandishi
ametushirikisha njia sahihi za kununua wateja bora wa biashara zetu na
kwa gharama nafuu ambazo biashara inaweza kumudu.
Kwa kuanza, kila biashara huwa inanunua wateja. Kila hatua unayotumia
kuwafanya wateja wajue kuhusu uwepo wa biashara yako, ni kununua
wateja. Kama umewahi kutangaza biashara yako, umewahi kuandaa
vipeperushi, kama umetengeneza bango, au kuuza vitu kwa pamoja kwa bei
ya punguzo, kama umewahi kupunguza bei ili mteja anunue, au kutoa zawadi
kwa mteja anayenunua. Kama umewahi kutoa usafiri kwa mteja, au
kumpelekea alichonunua, au kumwomba mteja wako akuletee wateja zaidi.
Zote hizo ni harakati za kununua wateja unazotumia kwenye biashara yako.
Sasa kuna ambazo zinakuletea wateja bora, nyingine hazikuletei wateja
wazuri. Nyingine ni za gharama kubwa kwako, nyingine ni za gharama
ndogo.
Kupitia kitabu cha BUYING CUSTOMERS, tunakwenda kujifunza jinsi ya kununua wateja bora kwa gharama nafuu kwenye biashara zetu.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment