Mwanzilishi
wa kampuni ya Microsoft Bill Gates, amezindua kampeni ya kusaidia watu maskini
zaidi barani Afrika, kusini mwa jangwa la sahara, kwa kufuga kuku
Bilionea
huyo Bill Gates anasema kuwa kufuga kuku kunaweza kuwa kifaa muhimu katika
kukabiliana na ufukara hohe hahe.
Ameahidi
kutoa kuku 100,000, na ukurasa katika mtandao wa mradi huo tayari umewavutia na
kusambazwa kwa maelfu ya watu.
Umoja
wa Mataifa unakisia kuwa asilimia 41 ya watu katika Bara la Afrika, Kusini mwa
jangwa la Sahara wanaishi katika ufukara mkubwa.
Bwana Gates alisema kuwa mkulima anayefuga
kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola 1,000 kwa mwaka.
Bwana
Gates alisema kuwa mkulima anayefuga kuku watano anaweza kupata zaidi ya Dola
1,000 kwa mwaka. Mtu hutajwa kuwa maskini iwapo anapata Dola 700 pekee kwa
mwaka.
Alisema
kuwa lengo la mradi huo ni kusaidia zaidi ya asilimia 30 ya watu wanaoshi
mashambani Kusini mwa Jangwa la Sahara ili wapate huduma ya kufuga kuku wa hali
ya juu mbao watachanjwa. Alisema hatua hiyo itaongeza watu wanaofuga kuku kwa
asilimia tano.
Ananukuliwa
akisema kuwa kuku huongezeka maradufu na kwa hivyo hakuna uekezaji ulio na
mapato mazuri kwa asilimia ya juu kuliko ufugaji kuku.
Alisema
hayo alipokuwa akianzisha mradi huo jijini New York. Anashirikiana na shirika
na kutoa misaada kwa maskini la Heifer International.
Watu
milioni 800 huishi katika hali ya umaskini hohehahe, kulingana na takwimu za
Umoja wa Mataifa.
CHANZO CHA
HABARI : BBC SWAHILI , 09 JUNI, 2016
No comments:
Post a Comment