Thursday, September 15, 2016

MATOKEO YA MICHEZO YA UEFA ILIYOCHEZWA USIKU WA LEO



Matokeo ya michezo ya UEFA iliyochezwa usiku wa leo
  • 15 Septemba 2016

Wachezaji wa Madrid wakishangilia ushindi 

Ligi ya klabu bingwa barani ulaya imeendelea kutimua vumbi usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na michezo tisa ikipigwa katika viwanja tofauti.

Manchester City wakiwa nyumbani wameibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach, hatrick ya Kun Aguero na goli moja la Kelechi Iheanacho yalitosha kuipatia Man City alama tatu na kuwa timu ya pili kwenye msimamo wa kundi C ambalo linaongozwa na Barcelona.

Tottenham Hotspurs ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha 2-1 dhidi ya Monaco ya Ufaransa ambayo inaongoza ligi kuu nchini humo.
Lakini usiku wa kuamkia leo ilikuwa ni kicheko kwa wachezaji na washabiki wa Leicester City, wakiwa ugenini waliipiga Club Brugge ya ubelgiji jumla ya magoli 3-0 huku Riyad Mahrez akifunga mara mbili.



Huu ni mchezo wa kwanza kwa Leicester City UEFA
Borussia Dortmund ikiwa ugenini iliidhalilisha Legia Warszawa ya Poland kwa dozi ya 6-0.
Na katika mchezo uliowastaajabisha wengi ulikuwa ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Sporting CP Lisbon ya ureno ambapo Madrid iliibuka na ushindi wa magoli 2-1.
Sporting Lisbon ilikuwa ya kwanza kuandika goli kwenye dakika ya 48 goli lililodumu hadi dk ya 89 ya mchezo ambapo C.Ronaldo aliisawazishia timu kwa mpira wa adhabu ndogo maridadi kabisa uliyoenda moja kwa moja kimiani, sekunde chache kabla mpira kumalizika Alvaro Morata aliiandikia Real Madrid goli la pili akiunganisha krosi ya James Rodriguez.
 Sergio Aguero kwa sasa ana magoli 9 katika michezo tisa ya msimu huu
Matokeo mengine 
Bayern 04 Leverkusen 2-2 CSKA Moscow
FC Porto 1-1 F.C. Copenhagen
Juventus 0- 0 Sevilla
Lyon 3-0 Dinamo Zagreb 

BBC  SWAHILI

No comments:

Post a Comment