Friday, July 1, 2016

BAKHRESA AONESHA JEURI YA FEDHA ZIMBABWE



Bakhresa aonesha jeuri ya fedha Zimbabwe

Said Salim Bakhresa

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BILIONEA Mtanzania, Said Salim Bakhresa, amepanga kutumia dola za Marekani milioni 30 sawa na Sh bilioni 65.5 kuchukua umiliki wa kiwanda cha usagishaji Zimbabwe, Blue Ribbon Industries (BRI).

Kwa mujibu wa gazeti la Zimbabwe Mail, Bakhresa Group, moja ya himaya kubwa ya kampuni nchini Tanzania, imeifahamisha rasmi Tume ya Ushindani na Forodha ya Zimbabwe kuwa inapanga kununua umiliki wa asilimia 100 wa kampuni hiyo iliyotaabani.
Mwaka 2014, Bakhresa Group ilishinda zabuni ya kumiliki hisa katika BRI baada ya wanahisa wake wakuu kukaribisha zabuni kwa wawekezaji wainunue au kuingiza mtaji katika BRI ili kufufua operesheni za kampuni hiyo.

BRI, ambao ni watengenezaji wa mkate na vyakula vya mifugo imekumbwa na matatizo ya kifedha na ilikuwa ikihangaika kulipa mikopo iliyokopa kutoka ubia wa mabenki ya Zimbabwe na washirika wa kibiashara.

GAZETI   LA  MTANZANIA, IJUMAA, 01/07/ 2016

No comments:

Post a Comment