Saturday, September 26, 2015

UPO KATIKA KUNDI LIPI ?



INGAWA   sisi   ndio   tunaoishi  , kama  tunavyoweza   kukumbuka, ni   bayana  kwamba   tuna   UFAHAMU  mdogo   sana   kuhusu   MAISHA  yetu   kuliko   wanavyofahamu    marafiki  au  maadui   zetu wakubwa.
    Hawa    wanaweza    kujua   vizuri   kasoro   ya   ufahamu  wetu; wanaweza     kutathmini  udhaifu  wetu    kuliko   sisi  wenyewe ;  wanafahamu    kwa   usahihi  zaidi   uwezo   wetu   ulivyo ,  wakati   sisi   wenyewe  tunaweza    kujisifia   kwa   viwango   vsivyo   vya   kweli.
   Hatua   ya   mwisho    katika   kuishi  vizuri    ni    kuhakikisha  tunajifanyia    tathmini    sahihi. SAIKOLOJIA   inasaidia     kufahamu    hayo—hutupatia  DARUBINI   ya  ufahamu   ambayo     si    tu     inatuwezesha  KUJIFAHAMU    wenyewe   kama    wengine   wanavyotufahamu ,  lakini     pia    KUFAHAMU    WAZI   NGUVU   NA   UDHAIFU  WETU, KISHA    kutuonesha   uwezo   na  mapungufu  yetu.
       JUNG  ameainisha  ubinadamu   katika   makundi  mawili , LA  WATU  WASIRI  na  wale   WALIO   WAZI.Misamiati   hii   miwili   ina   maana   gani ?  Misamiati   hii  miwili   ina  maana  gani ?  Kwa  ufafanuzi   wa   haraka  haraka ,  WATU  WASIRI    wanaangalia   ndani ;  WATU  WA  WAZI   huangalia   nje . Picha    nzuri   zaidi   inapatikana   kwa   kuwa   na   aina   zinazotambulika.
      WATU   WASIRI   hupenda    kujisomea , wana   uwezo   mkubwa  wa    KUFIKIRI , HUEPUKA    MAKUNDI   YA  WATU, HUPENDA  UPWEKE ,  HUPENDA   KUFIKIRI  FIKIRI , KULIKO    VITU. Ni   wepesi    sana    kufikiri   na   kuchukia , lakini  mara  nyingi    huepuka    kuchanganyika   na  wengine. KUNDI   HILI   HUPENDA  VITABU   KULIKO   WATU , NI   WAFIKIRIAJI  SANA , WANA   AIBU    NA    HUPENDA    KUJIFICHA.
        Kundi  la   WALIO  WAZI   ni   kinyume   na   WASIRI ; HUPENDA  KUJIAMINI  na  KUTUMIA  NGUVU ,  HUPENDA   KUFURAHI ,  HUPENDA  KUWAPONGEZA  WENGINE , HUPENDA   KUCHANGANYIKA   NA  WENGINE , HUEPUKA   UPWEKE, HUPENDA    MAKUNDI  YA   WATU ,HUPENDA  ZAIDI  VITENDO   KULIKO   KUFIKIRIA  NA   VITABU. Hawapendi   kuficha   hasira   zao    wakichukia   na   hupenda   zaidi  KIJIKWEZA   kuliko   KUJISHUSHA.
      Je, unayatambua   makundi   haya ?  Wewe  upo   katika   kundi   lipi ? Bila   kusema   kuwa   unaweza    ukawa   pande   zote    mbili , isiwe   vigumu   kuamua  upande   ulio   na  uzito   zaidi.
       Hapa , sasa, kuna   somo   la   kujitathmini  mwenyewe. Tulia   na   uamue   iwapo  wewe   ni   MSIRI   au   MUWAZI ,  ndipo   ufahamu   utakaoupata      utakupatia   faida  mbili.
      KWANZA , utakuwa   na  uwezo  wa   kusahihisha   uwiano ,  yaani ,  kama  wewe   ni   MSIRI , unaweza  kuanza kupenda  kuwa   karibu  zaidi  na  vitu  pamoja   na  watu  kuliko  kujipenda   mwenyewe ; kama wewe  ni  MUWAZI,  unaweza  kuanza  kuchambua   rasilimali   ulizo  nazo. Kwani   tabia   yenye   uwiano   ndiyo   inayoweza    kukubalika   kwa    makundi   yote   mawili.Faida   ya  ziada  ni kwamba, huweza    kukupatia   ufahamu   wa  upinzani  mdogo    dhidi   ya  baadhi  ya  majukumu.
        Kwa   mfano, mtu   MSIRI  ana  FURAHA  katika  uwezo  wa   kazi.Hiyo  haimaanishi  kuwa   kundi  moja   haliwezi   kufanya  kazi   nzuri  ambayo  tabia  ya  kundi   linguine    hufaa  zaidi. Kwa   namna    yoyote  ile,  lakini  kwa   UFAHAMU, kwa   mfano ,  kama   wewe  ni  MSIRI ,  KWAMBA    unatakiwa    kuonesha   viwango  vya    mchanganyaji  mzuri, itakuwezesha   kufahamu  umuhimu  wa    kuongeza  jihudi   ili   kupata    MAFANIKIO.
       Hivyo,  ni   vyema   ufahamu   kundi   ulilomo   ndugu   yangu. UFAHAMU   utakaoupata   una   manufaa   sana   kwako.    
    
        Asante   kwa   kusoma    makala  hii ndugu  yangu   usisahau   kumshirikisha   mwenzako    AJITAMBUE.


Makala   hii  imeandikwa   na   MWL    JAPHET   MASATU. Anapatikana  kwa  E-MAIL ,   japhetmasatu@yahoo.com  + 255 716   924   136.

No comments:

Post a Comment