Tuesday, June 15, 2021

JINSI YA KUPATA NA KUTUNZA WATEJA KWENYE BIASHARA YAKO.

Rafiki yangu mpendwa,
Kila ninapopata nafasi ya kushauri au kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, huwa nawauliza kama wanajua dhumuni na malengo ya biashara zao.

Majibu ambayo huwa napata yanaonesha wazi kwamba wengi hawajui tofauti ya dhumuni na lengo la biashara zao.
Wengi hujiona wapo kwenye biashara ili wapate faida.

Ni fikra na mtazamo huo ndiyo vimekuwa kikwazo kwa ukuaji wa biashara zao. Kama biashara inachoangalia ni kuingiza faida pekee, lazima itapoteza wateja kwa kiasi kikubwa sana.



Dhumuni la biashara linapaswa kuwa ni kutengeneza na kutunza wateja. Lakini lengo kubwa la biashara linapaswa kuwa kutengeneza faida. Ni kupitia wateja ndiyo biashara inaweza kuingiza faida.
Hivyo kwa kuanza na wateja, biashara itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutengeneza faida nzuri.

Biashara nyingi huwa zinashindwa kwa sababu hazina wateja wa kutosha kuziwezesha kujiendesha kwa faida. Kwenye makala ya leo ya ushauri wa changamoto tunakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza na kutunza wateja kwenye biashara na iweze kufanikiwa.

Wasomaji wenzetu waliotuandikia kuomba ushauri kwenye hili walikuwa na haya ya kusema;

“Biashara yangu inapoteza wateja kila siku haikui zaidi ya kumaliza pesa zangu za kubrandy nimefungua Min Juice bar huduma na bidhaa tunazozalisha ni nzuri na bora sana lakini tatizo ni nini?” – Victor V. G.

“Sehemu nilipo weka biashara sio chumba cha njee ni ngum kufikiwa na wateja nifanye nini ili niweze kufikiwa na wateja na kujulikana pande zote” – Laban H.

Changamoto hizo mbili linamlenga mteja, moja kupata mteja na ya pili kumtunza asipotee. Tutayajadili haya mawili kwa kina.

Kupata wateja wa biashara.

Ili kupata wateja kwenye biashara yako, lazima kwanza uchague ni wateja wa aina gani unaowalenga, lazima ujue sifa zao kabisa.
Kwa bidhaa au huduma unayouza, jua ni watu gani unaowalenga na jua sifa zao muhimu.
Jua matatizo au mahitaji waliyonayo ambayo biashara yako inatatua.
Jua uwezo wao wa kuweza kumudu gharama ya unachouza.
Jua wanakopatikana na njia gani ya kuweza kuwafikia.

Ukishazijua sifa za wateja wa biashara yako, usiwasubiri waje kwenye biashara, bali wafuate kule walipo.
Uzuri wa zama hizi siyo lazima biashara yako iwe eneo linaloonekana ndiyo ipate wateja.
Kwa kuwa na mkakati mzuri wa masoko unaweza kuwafikia wateja kule waliko, iwe ni ana kwa ana au kwa mawasiliano.
Usifanye biashara kizamani kusubiri waje, bali toka na watafute wateja.
Tayari umeshajua matatizo au mahitaji yao na tayari una suluhisho linalowafaa, ni wewe kuwafikia na kuhakikisha wanajua uwepo wa biashara yako na kushawishika kuja kwenye biashara yako.

Baada ya kuwashawishi wateja na wakaja kwenye biashara yako, unapaswa kuwashawishi wanunue.
Usiwakubalie kirahisi pale wateja wanapokuambua wameshaona na watakuja siku nyingine kununua, hapo wanakukimbia kirahisi.
Washawishi wanunue kwa kuwahakikishia kwamba hawatapoteza fedha zao wanapofanya maamuzi ya kununua.
Kumbuka wateja wako wametafuta fedha zao kwa maumivu na hawapo tayari kutengana nazo kirahisi. Lazima uwape uhakika kwamba wakitumia fedha zao kwenye biashara yako yatakuwa ni matumizi bora kuliko mengine wanayoweza kufanya kwa fedha hizo.

Mjue mteja, mfikie mteja na kumshawishi kuja kwenye biashara na anapofika mshawishi anunue, hizo ni hatua tatu kubwa za kupata wateja kwenye biashara yako.

Kutunza wateja wa biashara wasipotee.

Kama mteja hajanunua kwenye biashara yako, huyo siyo mteja wako. Hata kama amekuahudi atanunua, kama bado hajanunua, usimhesabie ni mteja.
Mteja akishanunua kwako mara moja, ni rahisi kununua tena kwa mara nyingibe kulimo kwa mteja ambaye hajanunua kabisa.
Mteja ambaye ameshanunua, kuna imani ambayo tayari ameshaijenga kwenye biashara.

Wanapokosea wafanyabiashara wengi ni kuhangaika kukimbizana na wateja wapya huku wakiwasahau kabisa wateja ambao tayari walishanunua.
Hii ni sawa na kuacha dhahabu ya uhakika uliyonayo ndani na kwenda kuhangaika kutafuta dhahabu sehemu ambayo huna uhakika nayo.

Sisemi uache kutafuta wateja wapya, ila ninachosema ni juhudi unazoweka kutafuta wateja wapya, weka juhudi za kiwango hicho hicho kuwatunza wateja ambao tayari wameshanunua.
Kuwatunza wateja ambao wameshanunua kwako, zingatia haya muhimu.

Moja ni kuwapatia huduma bora kabisa kwenye biashara yako. Wape wateja wako huduma bora ambazo hawawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote. Hilo litawasukuma kurudi tena kwako kwa sababu wanajua watapata ambacho hawawezi kupata pengine.
Kama hakuna tofauti ya wanachopata kwako na wanachopata kwa wengine, hawatajisumbua kurudi tena kwako.

Mbili ni kuendelea kuwasiliana nao mara kwa mara. Kila mteja ambaye ameshanunua kwako, hakikisha unakuwa na mawasiliano yake. Uzuri kila mtu ana njia mbalimbali za mawasiliano, kuanzia namba za simu, barua pepe na mitandao ya kijamii.
Mteja akishanunua kwako hawezi kuwa mgumu kutoa mawasiliano yake, hivyo muombe akupe mawasiliano hayo na yatumie kuwasiliana naye.
Siyo tu unatumia kumtangazia biashara yako, bali kumjulia hali, kumtumia salamu mbalimbali kulingana na sikukuu au matukio mbalimbali.
Kadiri unavyowasiliana na wateja wako, ndivyo wanavyokufikiria wewe na biashara yako na kuja kwako pale wanapokuwa na uhitaji.

Tatu ni waombe wakuletee wateja zaidi. Kama mteja ameridhika na huduma unazompa, na hilo utalijua kwa shuhuda atakazokupa yeye mwenyewe, muombe awaalike watu wake wa karibu nao waje kupata huduma hizo.
Mteja anapochukua hatua ya kuwaalika wengine, yeye mwenyewe ataendelea kuja maana hawezi kuwaleta watu halafu yeye asije.
Kwa kumshawishi na akakubali kuleta wateja zaidi, anakuwa amechagua kuendelea kuwa mteja wako kwa muda mrefu zaidi.
Na mteja anapokuletea wateja zaidi, hakikisha unawapa huduma bora kabisa ili asipoteze imani yake kwa wale aliowashawishi kuja kwenye biashara yako.

Utoaji wa huduma bora na za kipekee, mawasiliano ya mara kwa mara na wateja kukuletea wateja zaidi ni njia bora za kuwafanya wateja kuendelea kuwa kwenye biashara yako.

Kama mfanyabiashara jua dhumuni na lengo la biashara na weka juhudi kubwa kwenye kutafuta wateja wapya wa biashara yako, na juhudi za aina hiyo pia kwenye kuwatunza wateja ambao tayari wameshanunua.
Kwa namna hiyo biashara itakuwa na wateja wengi na kuweza kuingiza faida nzuri.

 

MIHEMKO : MOTO UNAOTUTEKETEZA.

Tunaishi katika wakati ambao vyombo vya habari vimepata nafasi kubwa ya kutoa taarifa, matangazo au habari ambazo zinasababisha watu wengi kuhemka au kujengewa hofu dhidi ya mambo yanavyoendelea katika jamii. Utaona au kusikia matangazo iwe katika vyombo vya habari au mtandaoni yote yameshajua namna yanavyoweza kufanya watu washindwe kujidhibiti kuamua mambo au kufuatilia vitu. Hili limechangia sana watu wengi waendeshe maisha yanayokosa utulivu kabisa.

Utaona naona ambavyo matukio mengi yakitokea iwe ni jambo linalovuma mtandaoni basi kila mtu hatataka kutulia limpite bali afuatilie. Kufuatilia huko hakujasaidia zaidi kumeleta usumbufu mkubwa kwa maisha ya watu wengi pale ambapo hata wameweza kuwa wamejiunga kupewa taarifa ya mambo ikitokea basi waarifiwe almaarufu “notifications”. Hili limesababisha watu muda wote wakae mitandaoni au kushika simu kuhakikisha hapitwi na matukio yoyote yale. Hili limesababisha watu wengi wakose muda binafsi wa kukaa wenyewe kutafakari maisha.

Si ajabu kuona leo hii watu wakishindwa kudhibiti hisia zao za furaha au huzuni kwa kushirikisha kila kitu katika mitandao ya kijamii. Mfano mtu kagombana na mpenzi wake basi hilo tukio atataka watu wote wajue kuwa mahusiano yao yapo katika migogoro. Wengine hata wameweza kuthubutu hata kuanika mambo yao ya siri mtandaoni na baadaye wanajutia juu ya maamuzi hayo waloyatenda sababu tu ya mihemko au hasira.

Bado kuna kundi la watu wachache ambao wana uwezo wa kudhibiti mihemko yao licha wanaweza kuonesha kwa wengine namna walivyoguswa na matukio au hali wazipitiazo. Mtu anajenga udhibiti wa mihemko akijua katika mihemko kuna maamuzi ya ovyo hufanyika na mwisho wake ni fedheha. Mtu ambaye pia anashindwa kujidhibiti kifalsafa ni kudhihirisha uchanga wa kuielewa falsafa. Udhibiti wa mihemko au hisia ni ukomavu ambao katika shule ya falsafa unahimizwa sana maana kuna manufaa makubwa katika udhibiti wa mihemko kuliko hasara zake.

Njia ni ile ile katika udhibiti wa mihemko kwa kujiuliza je nitakalo kulifanya ni lazima kulifanya ?. Kadri unavyojiuliza na kujihoji juu ya ulazima wa kushirikisha kitu, kusema kitu, kufanya kitu ndivyo unavyoweza kuamua kitu kwa hekima na bila majuto siku za usoni. 

Karibu   Ujiunge   na " DARASA  ONLINE "  kujifunza  zaidi

Tuwasiliane

NA  KOCHA MWL.  JAPHET   MASATU , DAR  ES  SALAAM , TANZANIA
WhatsApp + 255 716 924136  /  + 255 755 400128 / + 255 629748937 /  + 255 688 361 539
EMAIL :   japhetmasatu@gmail.com

 

Sunday, June 13, 2021

WAEPUKE KAMA UKOMA WATU WENYE TABIA HIZI 15 , NI SUMU KWA MAFANIKIO YAKO.


 Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu wanaitwa ‘watu sumu’ watu ambao kwa kujihusisha nao unajikuta ukirudi nyuma badala ya kusonga mbele.

Kwa kuwa wale unaojihusisha nao huwa wana ushawishi mkubwa kwako, unapaswa kuwa makini sana na kila mtu unayemruhusu awe karibu yako.

Leo tunakwenda kuziangalia tabia 15 za watu hao sumu, kama unazo unapaswa kuziacha na ukiwaona watu wanazo kaa nao mbali.




Tabia 15 za watu sumu wa kuwaepuka kwenye maisha yako.

( 1), KUISHI  JUU  YA  KIPATO.
Mtu yeyote anayetumia zaidi ya kipato chake ni mtu sumu, hataweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yake.
Hawa ni watu ambao hukopa fedha kwa matumizi ya kawaida ambayo hata siyo muhimu.
Kama una tabia hii acha mara moja. Na ukishaona mtu ana tabia hii achana naye, maana atakushawishi na wewe uwe kama yeye.

( 2 ). WANAJUA  KILA  KITU  KWENYE   MICHEZO  NA  BURUDANI.
Watu sumu huwa wana muda mwingi wa kufuatilia mambo ya michezo na burudani kuliko wanavyotumia kufanya mambo ya kuwapa mafanikio.
Badala ya kuyageuza maisha yao kuwa burudani kwao kwa kuziishi ndoto zao, wanatafuta burudani kutoka nje, kitu ambacho huwa hakiwasaidii.
Chagua kupata burudani kwenye kuishi ndoto zako na siyo kuhangaika na ndoto za nje.

( 3 ). KUFUATILIA  WATU  MAARUFU.
Watu sumu huwa wanafuatilia na kujua maisha ya wengine kuliko wanavyoyajua maisha yao wenyewe.
Wanayajua mahusiano ya watu maarufu, wanajua kiasi cha fedha walichonacho na hata wanajua jinsi ya kuwashauri.
Cha kushangaza, hawajui kuhusu fedha zao wenyewe na hawawezi kujishauri licha ya maisha yao kuhitaji sana ushauri kuliko hata wanaoutoa kwa wengine.
Acha mara moja kufuatilia maisha ya wengine na pambana na maisha yako, na wale wanaopenda kufanya hivyo, achana nao.

( 4 ). HAWAPENDI  HATARI.
Kufanya vitu vipya kuna hatari ya kushindwa, watu sumu hawapendi kushindwa, hivyo hufanya yale tu waliyozoea.
Wakikuona wewe unajaribu vitu vipya na vikubwa hawatakuacha kirahisi, watakukosoa na kukukatisha tamaa ili usichukue hatua hizo.
Tambua bila kuchukua hatua hatari huwezi kufanikiwa, hivyo achana na yeyote anayekukatisha tamaa kwenye hatua kubwa unazopanga kuchukua.

( 5 ). HAWANA  MSUKUMO  MKUBWA.
Watu sumu wameridhika sana na maisha ya chini waliyonayo, hawana msukumo wa kufanya makubwa zaidi. Wakipata kazi wanaona wamemaliza kila kitu. Wakiwa na biashara ndogo wanaona wameshayawezea maisha. Ni mpaka wakutane na changamoto ndiyo wanajua mazoea siyo mazuri.
Wewe kuwa na msukumo wa kufanya makubwa, jiwekee malengo makubwa na pambana kuyafikia, ukishayafikia usiridhike, weka malengo mengine makubwa zaidi.
Achana kabisa na wale walioridhika na maisha yao ya chini.

( 6 ). WANAWALAUMU  WANASIASA.
Watu sumu huwa wanatupa lawama zao kwa wanasiasa na wengine wenye mamlaka. Kama hawajapata wanachotaka, wanaona sababu ni wanasiasa.
Wanawasikilia na kuwaamini wanasiasa wanapowaahidi mambo mbalimbali.
Wasichojua ni kwamba wanasiasa wanaishi kwa kuwategemea wao, hivyo hawawezi kuwasaidia kwa namna yoyote ile.
Jua haya maisha ni vita yako mwenyewe, kama utashinda au kushindwa ni kwa sababu zako mwenyewe hivyo usimlaumu yeyote.
Usimwamini mwanasiasa yeyote anapokuahidi chochote, pambana kwa juhudi zako kupata kile unachotaka.

( 7 ). WANACHUKIA  MATAJIRI.
Watu sumu huwa wanawachukia sana matajiri, wanawaona ndiyo chanzo cha wao kubaki kwenye umasikini. Au wanapotaka kitu kutoka kwa matajiri na wasiwape, wanawaona wana roho mbaya. Wasijue kwamba matajiri hao wana nidhamu kubwa kwenye yale waliyopanga.
Wapende matajiri, waone ni watu wazuri, jifunze kutoka kwao ili na wewe uweze kufikia utajiri pia.
Na ukimuona mtu yeyote anawasema vibaya matajiri, kaa naye mbali.

( 8 ). WANAKANDIA  ELIMU   YA  MAENDELEO  BINAFSI.
Watu sumu huwa wanajiona tayari wanajua kila kitu kwenye maisha yao. Waambie wasome vitabu vya maendeleo binafsi na watakuambia hawana muda. Waoneshe muda wanaopoteza na watakuambia hakuna kipya kwenye vitabu hivyo, ni yale yale tu.
Wewe usiwe kwenye kundi hilo, penda kujiendeleza binafsi, soma vitabu, jifunze na chukua hatua.
Na unapokutana na mtu akakuambia hakuna kipya kwenye vitabu au tayari anajua yote hayo, kaa naye mbali, ni mtu sumu huyo.

 ( 9 ). WANAKUPA  USHAURI  MBAYA.
Watu sumu hukimbilia kukupa ushauri kabla hata hujawaomba na ushauri wanaokupa huwa ni mbaya. Kwa sababu hawataki upige hatua kuliko wao, watahakikisha wanakushauri mambo yatakayokukwamisha.
Usipende kutoa ushauri kwa wale ambao hawajakuomba na epuka sana kupokea ushauri kwa watu ambao hujawaomba.
Gharama ya ushauri wa bure ni pale unapoanza kuufanyia kazi, kwa kuwa utakugharimu sana.
Jua watu ambao ushauri wao huwa una walakini na waepuke sana, maana pia huwa wanalazimisha upokee ushauri wao.

(10 ). KUULIZA  MASWALI  YA  KIJINGA.
Watu sumu huwa wanapenda sana kuuliza maswali ya kijinga. Waambie kitu kizuri na wao watatafuta njia ya kuonesha hakiwafai wao.
Waambie wasome vitabu watakuambia hawajui wapate wapi vitabu.
Waambie wapambane kutoka kwenye umasikini na watakuambia wote hatuwezi kuwa matajiri.
Waambie wajiajiri watakuambia wote tukijiajiri nani atamfanyia kazi mwenzake.
Yote hayo ni maswali ya kijinga na usijisumbue kuyajibu, waache wajiridhishe nayo.
Waepuke sana watu wenye maswali ya kijinga, maswali yanayotengeneza vikwazo kwenye kila jambo zuri.

( 11 ). HAWANA  NIDHAMU.
Wanapanga kufanya kitu, ila inapofika wakati wa kukifanya wanaahirisha na kuona hawajawa tayari.
Tatizo siyo kutokuwa tayari, tatizo ni kukosa nidhamu ya kujisimamia na hilo linakuwa kikwazo kwa mafanikio yako.
Jijengee nidhamu ya hali ya juu sana, panga mambo na fanya kama ulivyopanga bila kuruhusu chochote kukuzuia.
Na ukiwaona watu ambao hawana nidhamu, kaa nao mbali.

( 12 ). WANA CHUKI  NA  WIVU.
Watu sumu hawapendi kuona wengine wakipiga hatua kuliko wao, hivyo huwa na chuki na wivu kwa wale wanaopata matokeo mazuri kuliko wao.
Usiwe mtu wa chuki au wivu, kuwa mtu wa kupenda na kujifunza kutoka kwa wengine.
Na unapojikuta umezungukwa na watu wenye chuki na wivu, kimbia haraka.

( 13 ). HAWAWEZI  KUDHIBITI  HISIA  ZAO.
Watu sumu ni watu ambao hisia zao hulipuka haraka hata kwa vitu vidogo tu. Huwa ni rahisi sana kukasirishwa na mambo madogo madogo na yasiyo na tija. Kwa watu kujua udhaifu wao, wanautumia kujinufaisha.
Jifunze kudhibiti hisia zako na usimpe yeyote ruhusa ya kukukasirisha kwa jambo lolote lile.
Pia waepuke sana wale ambao hisia zao zinaweza kuibuliwa na mambo madogo madogo.

( 14 ). WANACHAFUA  MIILI  NA  AKILI  ZAO.
Watu sumu huchafua miili yao kwa kuilisha vyakula visivyo vya afya na vilevi mbalimbali, hilo hupelekea miili yao kuwa dhaifu na kushindwa kupambana na mafanikio.
Pia huchafua akili zao kwa kujaza habari hasi na umbea.
Epuka kuchafua mwili na akili yako, lisha vitu ambavyo ni safi na bora. Epuka vyakula vya haraka, vilevi na habari hasi.
Pia waepuke wote ambao hawathamini miili na akili zao.

( 15 ). WANA  SABABU  NYINGI.
Watu sumu huwa wana sababu za kujitetea kwenye kila jambo. Huwa siyo watu wa kuchukua uwajibikaji kwenye jambo lolote lile.
Wewe achana na sababu, kama kuna kitu kimetokea, kubali kuwajibika. Kwa njia hiyo wengi watakuamini na kukupa majukumu zaidi.
Waepuke sana wale wenye sababu na visingizio kwenye kila jambo.

Kwa kuangalia tabia hizi 15, kuna watu wengi itabidi uachane nao kwenye maisha yako, lakini hakuna namna, lazima ufanye hivyo kama unayataka mafanikio makubwa katika  sayari  hii  DUNIA.

Saturday, June 12, 2021

KIJANA WA KITANZANIA AU WEWE MTANZANIA , USIPOJIANDAA HAKUNA MJOMBA. FANYIA KAZI MAENEO 10 HAYA UTAFANIKIWA.

Kwa kufanyia kazi maeneo haya 10 ninayoshirikisha hapa, kuna nafasi nzuri ya kujenga vijana imara na wenye mchango mkubwa kwenye taifa letu.

( 1 ): BIASHARA  NA  UJASIRIAMALI.
Serikali haina uwezo wa kuwaajiri vijana wote waliohitimu elimu katika ngazi mbalimbali. Hata sekta binafsi pia haiwezi kuwaajiri wote wanaotaka kazi.
Lakini jamii zetu zina mahitaji na changamoto mbalimbali ambazo zikipata utatuzi wapo tayari kulipia.
Hii inatoa fursa kubwa ya vijana kuweza kufanya biashara na ujasiriamali wa aina mbalimbali kulingana na mahitaji yaliyo kwenye jamii.
Vijana wanaziona sana fursa hizo na wapo tayari kuzifanyia kazi, lakini mazingira yamekuwa siyo rafiki kwao kuchukua hatua.
Kuanzisha na kurasimisha biashara kwenye nchi yetu kimekuwa kikwazo kwa wenye nia ya kufanya hivyo.

Tunashukuru usajili wa biashara umerahisishwa sana kupitia BRELA, ila eneo la kodi bado lina changamoto kubwa.
Kijana anayeanzisha biashara mpya anatakiwa kuanza kulipa kodi kabla hata biashara haijaweza kuzalisha faida.
Biashara yoyote ile ina hatari ya kufa hasa kipindi cha mwanzo.
Kama ukiwekwa utaratibu wa vijana kupata neema ya kodi katika miaka miwili ya mwanzo ya biashara, huku wakiwa wanazifanya biashara zao kwa mfumo rasmi, itasaidia sana.
Taifa litapata mapato zaidi kupitia mzunguko unaotengenezwa na biashara mpya zinazoanzishwa na vijana kuliko linavyopoteza kwenye kodi.

( 2 ): FEDHA  NA  UCHUMI.
Hali ya uchumi wa kijana wa Tanzania bado iko chini sana kutokana na ushiriki wake mdogo kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Na kikwazo cha kwanza ni fedha, vijana wengi hawana vipato kabisa na wale walio navyo haviwatoshelezi kwenye mahitaji yao.
Hilo linakuwa kikwazo kwao kushiriki shughuli za uchumi kama kuanzisha biashara na hata kuwekeza pia.
Huduma za kifedha zimekuwa zinawatenga vijana kwa sababu hawakidhi vigezo muhimu vilivyowekwa, kama kuwa na dhamana ili kupata mikopo.

Kwa kuwa serikali imeweza kuwakopesha vijana wengi wakapata elimu ya juu, inaweza pia kuwakopesha fedha za kuwawezesha kushiriki shughuli za uchumi.
Vijana wajengewe uwezo wa kuwa kwenye vikundi ambavyo vitapewa mikopo ya kutumia kwa shughuli za uchumi na kuilipa kwa njia nafuu kuliko mikopo ya taasisi za kifedha.
Pia elimu ya kijana iweze kutumika kama dhamana ya kupata fedha kwa shughuli mbalimbali anazofanya.

( 3 ). KILIMO  NA  UFUGAJI.
Uhitaji wa chakula ni mkubwa kwenye nchi yetu na nji za jirani.
Nchi yetu imejaliwa kuwa na eneo kubwa la ardhi ambayo bado haijatumika kabisa.
Hayo yanatoa fursa kubwa ya vijana kuweza kujishughulisha na kilimo na ufugaji.
Lakini changamoto kwenye eneo hilo ni kubwa mno. Kuanzia kwenye uzalishaji mpaka kufika sokoni, kijana anakumbana na mengi yanayomuangusha kabisa.

Vijana wengi wamejaribu kilimo na ufugaji na hawajaweza kurudia tena kutokana na anguko ambalo wamepitia.
Kukosa miundombinu bora, kama kutegemea mvua badala ya kuwa na nyezo za umwagiliaji imekuwa inaathiri sana uzalishaji.
Na hata pale kwa bahati nzuri kijana anapoweza kuzalisha vizuri, akifika sokoni bei inakuwa siyo rafiki kwake, anapata hasara na kushindwa kurudi tena shambani.

Kutengwa kwa maeneo ya kilimo na ufugaji ambayo yamewekewa miundombinu muhimu hasa ya upatikanaji wa maji ya uhakika itasaidia sana kwenye hili.
Pia kufungua masoko hasa ya nje itampa kijana wigo mpana wa kuuza kile anachozalisha.

( 4 ). SAYANSI  NA  TEKNOLOJIA.
Sayansi na teknolojia vinakua kwa kasi kubwa mno na hakuna anayeweza kuvizuia.
Ukuaji huu wa kasi wa teknolojia umefungua fursa za vijana kuweza kujiajiri kwa urahisi kabisa kwa kutumia mtandao wa intaneti.
Lakini kijana wa Tanzania bado anakutana na vikwazo vingi anapojaribu kutumia fursa ya teknolojia kujiajiri.

Changamoto ya kwanza ipo kwenye urasimishaji wa biashara ambazo kijana anaweza kufanya mtandaoni akiwa hata nyumbani. Hilo linawafanya washindwe kukua kwenye  biashara hizo na hata kupata huduma nyingine muhimu.

Changamoto nyingine kubwa ni kulipwa kutoka nje ya nchi. Teknolojia imerahisisha mtu kuweza kuuza huduma mbalimbali za kidijitali kwa mtu yeyote aliye popote duniani.
Lakini kupokea malipo kutoka nchi za nje, jasa nje ya Afrika Mashariki ni kitu kigumu sana.
Kuna mifumo ya kupokea malipo mtandaoni kama Paypal na Stripe, lakini haifanyi kazi kwa hapa Tanzania.

Ni wakati sasa wa kufungua mifumo hii ya malipo ili vijana waweze kutumia teknolojia kuuza huduma zao na kupokea malipo popote duniani.

( 5 ). ELIMU  NA  UBUNIFU.
Mfumo wetu wa elimu pamoja na mapungufu yake mengi umeweza kuzalisha wahitimu wengi kwenye ngazi mbalimbali.
Kuna changamoto kubwa mbili zinazomkabili kijana kwenye eneo hili.

Changamoto ya kwanza ni kuhitimu huku akiwa hana uwezo wa kufanya chochote. Elimu yetu kwa sehemu kubwa imekuwa ni ya kukariri na kujibu mitihani. Vijana wanahitimu wakiwa na ufaulu mkubwa lakini hakuna wanachoweza kufanya.
Ni wakati sasa wa kufanya mapinduzi kwenye mfumo wetu wa elimu, ili uzalishe vijana wenye uwezo wa kufanya vitu vyenye tija kwa jamii.
Elimu ikuze ubunifu wa vijana katika kuyatumia mazingira yao kuzalisha thamani zaidi kwao na kwa wengine pia. Iwajengaa kujitambua na kujiamini kwenye yale wanayofanya.

Changamoto ya pili ni mzigo mkubwa wa deni la elimu ya juu kwa wale waliopata nafasi ya kusoma elimu hiyo kwa mkopo.
Mikopo ya elimu ya juu imekuwa na msaada mkubwa, kwani wengi tusingeweza kugharamia elimu hiyo bila mkopo.
Lakini mkopo huo umekuja kuwa kikwazo kikubwa kwa kijana kujinasua kiuchumi.
Anayepata ajira anakatwa kiasi kikubwa kulipa deni hivyo hawezi kubaki na fedha ya kutosha kumwezesha kufanya shughuli za kiuchumi.
Ambaye hajapata ajira deni lake linaendelea kukua zaidi na zaidi.

Mabadiliko yafanyike kwenye sera ya urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu ili impe kijana ahueni ya kuweza kushiriki shughuli nyingine za uchumi.

( 6 ). AJIRA  NA  KUJIAJIRI.
Pamoja na kwamba serikali haiwezi kuwaajiri vijana wote, bado ina uwezo wa kutengeneza fursa za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa vijana.
Bado taifa lina uhitaji wa wafanyakazi na watoa huduma zaidi kwenye jamii zetu. Jamii bado haijapata wahudumu wa kutosha hasa kwenye sekta za afya na elimu.
Hivyo serikali inapaswa kuwekeza kwenye kuajiri vijana zaidi na kupitia kufanya hivyo inajenga nguvu kazi kubwa zaidi.
Lakini pia serikali inapaswa kuweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuweza kuwaajiri vijana wengi. Kadiri mazingira ya kibiashara yanavyokuwa mazuri, ndivyo sekta binafsi zinavyostawi na kutoa nafasi zaidi za ajira.
Na kwa wale ambao wanakosa nafasi za kuajiriwa serikalini au kwenye sekta binafsi, wawe na mazingira mazuri ya kuweza kujiajiri wenyewe kama tulivyoona kwenye sekta mbalimbali hapo juu.

( 7 ). UONGOZI  NA  USIMAMIZI.
Vijana wanahitajika sana kwenye nafasi mbalimbali za uongozi. Hili linaleta damu mpya kwenye uongozi lakini pia linatengeneza viongozi wazuri kwa ajili ya siku zijazo.
Hakuna njia bora ya kujifunza kitu chochote kile kama kufanya. Hivyo vijana watajifunza uongozi kwa kupewa nafasi za uongozi.
Kwa bahati mbaya sana kizazi cha sasa cha vijana kimepita kwenye vyuo vikuu ambavyo havijaweza tena kutengeneza viongozi kama zamani.
Serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu hazipo tena huru kama zamani, hivyo vijana hawajifunzi kuwa viongozi huru wanaofanya maamuzi yao wenyewe. Tunakokwenda tunatengeneza taifa la viongozi wasiokuwa na msimamo wao wenyewe hasa kwa maslahi ya taifa.

Kumekuwa na mabaraza ya vijana ndani ya vyana vya siasa, lengo lake yamekuwa ni kutengeneza viongozi. Lakini hayawezi kufanya vizuri kwa sababu ndani ya vyama vijana wanaegemea zaidi kwenye itikadi. Na hata kupata nafasi hauangaliwi uwezo, bali kuonekana na kujipendekeza.
Ni muhimu nafasi za uongozi na usimamizi zitolewe kwa vijana kwa kuangalia uwezo wao. Na siyo tu uwezo kwenye ufaulu wa kielimu, bali kuangalia mambo ambayo kijana ameweza kufanya mwenyewe bila ya kusimamiwa na yeyote.
Uwezo ukitumika katika kuwapa vijana uongozi, itawezesha kupata viongozi wazuri, na pia kuwajenga kuwa viongozi bora zaidi.

( 8 ). VIWANDA  NA  UZALISHAJI.
Hakuna nchi inayoweza kupiga hatua kiuchumi bila ya uzalishaji. Serikali imekuwa inaimba wimbo wa viwanda lakini mtazamo umekuwa zaidi kwenye viwanda vikubwa vinavyolenga wawekezaji kutoka nje.
Nchi yetu inazalisha kila aina ya malighafi, lakini bidhaa nyingi tunaingiza kutoka nje.
Kuna fursa kubwa ya vijana kuweza kujiingiza kwenye shughuli za viwanda na uzalishaji ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi.

Mambo yanayohitajika katika kuwezesha hili ni elimu ya uzalishaji na viwanda itolewe kwenye vyuo vyetu vya ufundi.
Mchakato wa kuanzisha kiwanda ufanywe kuwa rahisi hasa kwa wazawa ili kupunguza urasimu unaokuwa kikwazo kwa wengi.
Upatikanaji wa mitaji na miundombinu mengine muhimu kwa ajili ya viwanda.
Sehemu kubwa ya bidhaa tunazoagiza nje zinaweza kuzalishwa hapa nchini na vijana kama wakiwekewa mazingira mazuri.

( 9 ). AFYA  NA  USTAWI.
Bila afya ya vijana taifa haliwezi kustawi. Afya ndiyo mtaji wa kwanza na muhimu kabisa kwa maendeleo ya taifa.
Vijana wana changamoto nyingi za kiafya, kuanzia afya ya uzazi, ulevi na uraibu, kushindwa kumudu gharama za afya na kukosekana kwa huduma bora za afya hasa maeneo ya vijijini.

Elimu ya afya ya uzazi na afya kwa ujumla inapaswa kutolewa kwa vijana ili wajue thamani ya afya zao na kujikinga na maradhi.
Elimu ya afya ya akili inapaswa kupewa kipaumbele kikubwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa ya akili na ambayo hayashughulikiwi vizuri kutokana na watu kukosa uelewa wa magonjwa hayo.
Vilevi na madawa ya kulevya vinapaswa kudhibitiwa sana ili visiharibu nguvukazi ya taifa.
Bima za afya kwa kila kijana ni muhimu ili kuweza kupata huduma za afya bila kuwepo kwa kikwazo cha gharama.
Na huduma za afya zinapaswa kuwa bora kwenye kila eneo ili kijana aweze kuzipata pale anapozihitaji.

( 10 ). TAFAITI  NA  MAANDIKO.
Kila kijana ambaye amefika elimu ya juu na kupata shahada, kuna utafiti amefanya. Lakini tafiti zote hizo huwa hazina manufaa yoyote kwa taifa. Zinachukuliwa kama sehemu tu ya mtu kupata shahada yake.
Hili siyo sawa, taifa linahitaji tafiti nyingi mno ili kujua nini kinaendelea kwenye kila eneo na nini kinaweza kufanyika.
Tafiti zinasaidia sana kuweza kufanya maamuzi sahihi kwenye mambo mbalimbali.
Vijana wanaweza kufanya tafiti na kuandika mambo yenye manufaa kwa taifa letu. Badala ya kuiga kila kitu kutoka kwa wengine, tunaweza kufanya tafiti kwa mazingira yetu na kujua kipi tunaweza kufanya na kikawa na tija.

Uwepo wa takwimu sahihi zinazohusu vijana pia ni hitaji muhimu katika kupima maendeleo ya vijana na ufanisi wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa.
Mfano kujua vijana wangapi wenye elimu za ngazi mbalimbali na taaluma mbalimbali, kujua wangapi wameajiriwa serikalini, sekta binafsi au kujiajiri wenyewe. Kujua wangapi wapo kwenye kilimo, teknolojia na sekta nyingine.
Kwa kuwa na taarifa sahihi itasaidia kufanya maamuzi yenye tija kwa vijana.

Maeneo haya kumi yamegusa karibu kila eneo la maisha ya kijana na hata Mtanzania kwa ujumla. Tafiti zaidi zinahitajika kwenye kila eneo ili kuweza kufanya maamuzi bora na yenye tija kwa vijana na taifa.

Imani yangu kubwa ni vijana wakiwezeshwa kwa kujengewa uwezo wa kuweza kuzitumia fursa nyingi zilizo kwenye jamii zetu, taifa letu litanufaika kwa kiasi kikubwa mno.
Taifa liwekeze kwa vijana, matokeo ya baadaye yatakuwa makubwa sana.

Je , unawaza   ufanye   nini ?  Ungana  na  " DARASA   ONLINE "  ujifunze mengi ya  kukuwezesha  kutoka  katika  hali  ya  utegemezi   na  kuweza  kusimama   peke  yako na  kufanikiwa.

NA  KOCHA  MWL.  JAPHET  MASATU , DAR  ES  SALAAM

Tuwasiliane  kwa  WhatsApp + 255 716924136  /   0755 400 128

 

WEKA NGUVU ZAKO KWENYE KUFANYA KILICHO BORA LEO , WAKATI BADO UNA NAFASI YA KUFANYA HIVYO.

Wewe Sio Mtabiri Mzuri, Hivyo Acha Kujiogopesha.

Mara baada ya sultani wa dubai kuamua kusafiri baharini na baadhi ya wapambe wake.

Siku iliyofuata walijumuika kwa pamoja kwa ajili ya kuanza safari.

Hata hivyo , wakati meli ilipoondoka kutoka nchi kavu, mmoja wa wapambe wake, ambaye hakuwahi kuona bahari hapo kabla alianza kupata hofu ya kukaa ndani ya meli , alilia na kupiga kelele.

Sultani alijaribu kumtuliza lakini hakumsikiliza.

 Watu wengi kwenye meli walijaribu kumtuliza lakini hawakufanikiwa.

Safari ya kila mtu ambayo ilipaswa kuwa ya kufurahia na utulivu , iligeuka kuwa moja ya mateso.

 Sultan hakujua cha kufanya.

Siku mbili zilipita kama hivo.

Mpambe huyo alikataa kula hata kulala.

Kila mtu kwenye meli alichukizwa na tabia yake.

Sultan alifikiria inaweza  kuwa bora zaidi kurudi bandarini.

Hapo ndipo mtu mmoja alipomjia na kusema, mkuu kwa idhini yako, nitaweza kumtuliza.

Ikiwa tu utaniruhusu kutumia njia zangu bila kuhoji.

Bila kusita, sultan alisema, “ dhahiri “. Una ruhusa yangu.

Si hivyo tu kama utafanikiwa nitakulipa kwa ajili ya kutatua tatizo hili.

Mtu mwenye hekima alitoka nje na kumwambia mmoja wa wafanyakazi “ Mtupie ndani ya bahari, mara moja”.

Mfanyakazi alisita kwanza lakini mtu huyo alikuwa na ruhusa ya sultani, kwa hivyo alimshika mtu huyo na kumtupa baharini.

Mpambe aliripuka na kuzama , akameza maji mengi ya bahari.

Kisha akarudi juu na akapiga kelele zaidi kuliko hapo awali na akazama tena.

Hii ilitokea mara 2-3 na kisha waziri akaamuru arudishwe tena ndani ya meli.

Mpambe alirudishwa ndani ya meli, mara hii hakulalamika wala kulia na safari ikawa na amani.

Kila mmoja alifurahia safari na wote walikuwa na amani.

Baada ya kumaliza safari, meli ilirudi bandarini.

Aliporudi, kabla ya kuondoka kwenye meli , sultan akaenda kumwona, Yule mwanahekima na kumuuliza, ulijuaje kwamba kwa kumtupa mtu huyo baharini, atatulia?

Yule mwanahekima alimjibu , “kwa sababu ya uzoefu wangu wa kwenye ndoa”, baada ya ndoa yangu, siku zote nilikuwa na hofu ya kumpoteza mke wangu na siku zote nilikuwa nikimlalamikia  na kama vile mtu huyo alivyofanya kwenye meli.

Siku moja mke wangu hakuweza kunivumilia tena aliniacha.

Kuishi bila yeye ilikuwa uzoefu wa kutisha kutoka kwangu.

Alirudi pale nilipomuahidi kwamba sitamlalamikia tena.

Kwa njia hiyo hiyo, mtu huyo alikuwa hajawahi kupima maji ya chumvi na hakuwahi kujua uchungu wa kuzama.

Lakini alipotupwa baharini na kurudishwa kwenye meli, hapo ndipo alipoelewa.

Umekuwa unatabiri mambo mengi sana kuhusu maisha yako, lakini je ni mambo mangapi uliyotabiri yametokea?

Ni mambo mangapi ambayo ulikuwa unayahofia, yanakunyima usingizi yametokea kweli?

Nafikiri ni machache sana, kama hata yapo.

Ukweli ni kwamba wewe sio mtabiri mzuri, na wala hutakuwa mtabiri mzuri kadiri siku zinavyokwenda.

Umekuwa ukijitabiria kwamba maisha yatakuwa magumu zaidi, kwamba utapata hasara kwenye biashara, kwamba utafukuzwa kazi, kwamba mambo hayataenda vizuri!!

Lakini haya yote huwa yanatokea?

Hayatokei na hata kama yakitokea sio kwa sababu umetabiri ila kwa sababu umeamua kukubaliana na kile unachotabiri.

Unatabiri kwamba utapata hasara kwenye biashara halafu unaendelea kuendesha biashara yako kwa mazoea, unaishia kupata kweli hasara.

Ninachotaka kukuambia leo ni kwamba chochote unachotabiri leo hakina maana, chochote unachohofia leo ni kupoteza muda wako.

Hata ungetabiri kiasi gani na kujijaza hofu kiasi gani hakuna mmoja wetu anayejua nini kitatokea kesho.

Na hii ni vizuri sana kwa sababu lengo lako kubwa ni kuishi vizuri leo, kufanya kile ulichopanga kukifanya leo, kwa ubora wa hali ya juu sana kama vile ndio unakifanya kwa mara ya mwisho na hutakuwa na haja ya kuhofu kuhusu kesho tena.

Kwa sababu ukiishi vizuri leo, unaandaa mazingira mazuri ya kuishi vizuri kesho. Ukifanya kazi yako kwa ubora leo unaandaa mazingira mazuri ya kufanya kazi yako vizuri kesho.

Ukimhudumia mteja wako vizuri leo, kwa huduma nzuri ambayo hajawahi kuipata sehemu nyingine yeyote, unafikiri kesho ataenda wapi?

Unaona mambo yalivyo mazuri sasa?

Huna haja ya kutabiri, huna haja ya kuhofia, weka nguvu zako kwenye kufanya kilicho bora leo, sasa hivi wakati bado una nafasi hiyo ya kufanya hivyo.

NA  KOCHA  MWL  JAPHET  MASATU, DAR  ES  SALAAM

JIUNGE  SASA  NA  DARASA  ONLINE  UJIFUNZE  KWA VITENDO

TUWASILIANE  KWA  WhatsApp +  255 716 924 136

 

TUJIFUNZE KUVAA VIATU VYA WENGINE KILA TUNAPOFANYA AU KUSEMA JAMBO.

Sisi binadamu huwa tuna hulka ya kutowafikiria wengine bali kujijali wenyewe tu na wanabinafsi wa hisia zetu. Hili limechangia migogoro mingi katika maisha ya watu iwe ni katika kuishi na watu, kuwaongoza watu au mahusiano. Binadamu wote ni sawa katika mjengo wa mwili kuwa wote wanapata maumivu katika kuumia kama wengine. Hakuna binadamu ambaye mwili wake hauna damu au nyama. Wote ni sawa na hili linafanya hata kufa tutakufa binadamu wote mbali na tofauti zetu za kirika, kikabila, kitaifa au kirangi.

Chuki na unyama ambao huwa unajitokeza katika jamii zetu ni zao la watu kutojali hisia za watu wengine na hawajui namna wanavyoweza kuvaa hivyo viatu. Inawezekana ni tukio la maonevu katika jamii, mauaji au utesaji ila wasijue namna hata na wao wanaweza kupitia hali hizo au kufanyiwa hivyo na huenda wakaumia kama wanavyowasababishia wengine maumivu au uchungu. Kuwatendea wengine yaweza kuwa ni rahisi pale ambapo mtu hajali namna wengine watakavyoumizwa na hayo.

Binadamu pia tuna hisia za furaha na huzuni. Pale mambo mabaya yanapojitokeza huwa tunaumia kihisia, tunapata majonzi, tunapata taabu katika kukabiliana nayo. Mabaya haya si kuwa yanafanywa na wanyama isipokuwa ni binadamu wenzetu ambao kwa namna moja wana watu wanaowazunguka, wenye hisia kama wengine na wenye miili kama wengine. Kutenda ubaya tu na kisha kuacha kama mtu hajaona ubaya alotenda ni kuzalisha machungu kwa wengine ambao nao huwezi jua ni kwa namna gani hujipanga kuachilia au ulipizaji wa kisasi.

Ni rahisi kutusi wengine, rahisi kutotenda haki kwa wengine na ni rahisi kutojali wengine katika makubaliano fulani. Utakuta ni hali ya kawaida katika jamii zetu huwa tunapanga muda fulani wa jambo kufanyika ila watu hatuendi hivyo na wakati mwingine hata bila kutoa sababu za msingi. Watu wanaozingatia huwahi kufika na kukaa sana wakisubiri wengine. Hatujui ni kwa namna gani hukwazika na hilo jambo, lakini utakuta huwa hatujali hilo kuwa namna wengine watajisikia kwa kuchelewa kwetu. Huenda tunafanya hivyo sababu hatujawahi kuvaa viatu vyao kuwa vipi ukiwahi sehemu ukaachwa ukingoja masaa mengi au pengine hata mtu anakuja kukuambia haji licha umesubiri masaa mengi.

Tunaumizwa na mambo mengi katika kuishi kwetu kwa kuwa na watu ambao hawajajifunza au hatujajifunza kuvaa viatu vya watu wengine. Kwa kukosa kujua kuvaa viatu vya wengine tumekuwa ni watu wepesi kuhukumu, kuwasema wengine na kuchukulia wengine wana mioyo migumu na si laini kama wengine. Hili linaumiza jamii nyingi na kuendelea kuzalisha watu wenye mioyo ya kikatili, visasi, chuki na wasio na upendo kwa wanaowazunguka. Ila falsafa inatualika sote kuanza kujifunza kuvaa viatu vya wengine kila tunapofanya jambo au kusema jambo. Tuangalie je ingekuwa ni upande watu tungelipokeaje au kulichukulia.  

KARIBU  UJIUNGE " DARASA   ONLINE "

KOCHA  MWL.  JAPHET  MASATU , DAR  ES  SALAAM

WhatsApps  + 255  716924136 /    + 255 755 400128 /  + 255 688 361539

EMAIL : japhetmasatu@gmail.com

Tuesday, June 1, 2021

KUJUA KUSUDI LAKO SEMA NDIYO , KUISHI KUISHI KUSUDI LAKO SEMA HAPANA.

VITU VIWILI VYA KUFANYIA KAZI KWENYE MAISHA YAKO.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa na kuacha alama hapa duniani, kuna vitu viwili vikubwa unavyopaswa kuvifanyia kazi. Nimeweza kuja na vitu hivi viwili baada ya kujifunza na kutafakari kwa kina na kuona jinsi watu wanahangaika na mambo mengi lakini hawapati matokeo yoyote makubwa.

Ukiamua kuachana na mengine yote unayohangaika nayo na kufanyia kazi haya mawili tu, utaacha alama kubwa hapa duniani.

Mambo hayo mawili ni KUJUA NA KUISHI KUSUDI LAKO na KUWA NA NDOTO KUBWA unazofanyia kazi kwenye maisha yako. Haya mawili tu ndiyo yanahitaji muda, umakini na nguvu zako zote ili uweze kufanya makubwa.

KUSUDI LA MAISHA YAKO.

Mark Twain amewahi kusema kuna siku mbili muhimu kwenye maisha ya mwanadamu, siku ya kuzaliwa kwake na siku anayojua kwa nini amezaliwa.

Kila mtu huwa anazaliwa, ndiyo njia pekee ya kuja hapa duniani. Lakini ni wachache sana wanaojua kwa nini walizaliwa na hao ndiyo wanaoleta matokeo makubwa na kuacha alama hapa duniani.

Ubaya ni kwamba kujua kwa nini umezaliwa ni wajibu wako mwenyewe, hakuna anayeweza kukufundisha wala kukuambia. Hata wazazi waliokuzaa hawajui kwa nini ulizaliwa. Walimu wanaokufundisha ndiyo kabisa wanaharibu, maana wanakulazimisha uwe kitu kingine na siyo wewe.

Unahitaji mabadiliko makubwa kwenye maisha yako ili uweze kujua kwa nini ulizaliwa, unahitaji kuvunja mazoea mengi uliyojenga kwenye maisha yako ili uweze kuisikiliza sauti ya ndani yako na kujua kwa nini uko hapa duniani.

Wengi hawajui kusudi la maisha yao kwa sababu wameamini kile ambacho jamii na mfumo wa elimu umewalisha kwa miaka mingi. Kama shule ilikuambia umefeli kwa sababu huna akili, unaamini hivyo kwamba huna akili. Wakati shule haiwezi kupima uwezo mkubwa ulio ndani yako, kitu ambacho shule inapima ni kukariri.





KUJUA KUSUDI, SEMA NDIYO KWA KILA KITU.

Ili uweze kujua kusudi la maisha yako unahitaji kurudi kwenye maisha ya utoto wako, na kusema ndiyo kwa kila kinachokuja mbele yako. Jaribu mambo mengi uwezavyo, fanya kila kinachokuvutia kufanya na kadiri unavyofanya hivyo utaona kuna vitu unapenda kuvifanya vizuri zaidi na watu wanavifurahia unapovifanya. Hapo ndipo utajua kusudi lako lilipo na kuweza kulifanyia kazi.






















Hivyo fanya zoezi hili rafiki yangu, kama bado hujajua kusudi la maisha yako, chagua kipindi utakachorudi kwenye utoto wako na sema ndiyo kwa kila kitu. Kila kinachokuvutia kufanya, kifanye. Tenga muda ambao utafanya majaribio mbalimbali kwenye maisha yako na kujifunza kwenye kila unachofanya.




KUISHI KUSUDI, SEMA HAPANA.

Baada ya kujua kusudi la maisha yako, sasa unahitaji kuweka umakini wako wote kwenye kuishi hilo. Hupaswi tena kuhangaika na mambo mengine nje ya kusudi hilo.

Muda na nguvu zako vina ukomo, usipoteze kuhangaika na mambo mengine. Kuna mazuri yatakayokuja kwako na yenye fursa ya kunufaika zaidi, lazima uweze kusema hapana kwa hayo mazuri ili uweze kupata yaliyo bora kupitia kuishi kusudi lako.

Ili kuishi kusudi lako, SEMA HAPANA kwa mambo mengine yote na baki kwenye kuishi kusudi lako tu.

Baada ya mimi kujua kusudi langu lipo kwenye kufundisha wengine kupitia uandishi na ukocha, nimekuwa nasema hapana kwa mengine yote isipokuwa kusudi hili.


Ukishajua kusudi lako, yapangilie maisha yako kwa namna ambayo kuishi kusudi hilo ndiyo kipaumbele kikubwa kwako na sema hapana kwa mengine yote ambayo hayahusiani na kusudi hilo.

Ni kwa njia hiyo ndiyo unaweza kuweka umakini, muda na nguvu za kutosha kwenye kusudi lako na liweze kuleta matunda mazuri kwako.

NDOTO KUBWA YA MAISHA YAKO.

Maisha yasiyokuwa na ndoto ni maisha ambayo hayana msukumo wa kuyaishi.

Kama unataka kuacha alama hapa duniani, lazima uwe na ndoto kubwa, lazima uwe na picha ambayo hakuna anayeiona na hata ukiwaambia wengine hawaamini kama inawezekana.

Ukishakuwa na picha hiyo kubwa, unapaswa kuifanyia kazi kila siku mpaka utakapoifikia. Unapaswa kuwa tayari kutoa kafara ya kila aina kwenye maisha yako ili kufika kwenye ndoto yako kubwa.